Habari zenu
Natumaini mnaendelea vizuri na maisha na mategemeo yenu ya kumiliki kiwanda cha size yoyote.
Mimi kama nilivyoeleza hapo juu ninahusika na kuandika proposal paper kwa ajili ya yeyotr anayetaka kuomba mkopo katika taasisi yoyote inayohusika na utoaji mikopo iwe ni midogo hadi mikubwa. Kwa kuwa kazi yangu ingine ni kuunda mashine za aina mbalimbali kwa ajili ya viwanda vidogo na vikubwa, nimegundua watu wengi wanalalamika kikwazo kikuu cha kuanzisha kiwanda cha ukubwa wowote ni MITAJI. Na mitaji hii ni ngumu kuipata ila mpaka upate mkopo. Na mkopo huupati tu hivihivi hadi uwashawishi kwamba una uwezo wa kuurudisha. Kuwa na collateral pia ni usumbufu hivyo ukiwa na document inayoelezea vizuri jinsi utakavyorudisha pesa yao, inarahisisha kuwashawishi watoa mikopo kukupa mkopo na ukizingatia siku hizi pia kuna mikopo inatolewa bila kuwa na dhamana km ile ya CBA Bank
Mimi ninaandika mchanganuo wa biashara kuwawezesha wakopesshaji kujua ni kiasi gani wanatoa lakini ni jinsi gani pesa yao inarudi. Proposal ninazoandika zinahusisha mchanganuo wa gharama na maelezo mengine yanayohusu kupata mkopo wa kuanzisha kiwanda kidogo hadi vikubwa mfano viwanda vidogo vya kutengeneza Sabuni, Mkaa mbadala, Mikate, Chaki, kuchakata madini ya Copper, Sukari, Vitambaa nk au viwanda vikubwa vya kutengeneza bidhaa mbalimbali
Gharama ya kuandikiwa proposal paper inategemea na ukubwa wa mtaji wa hicho kiwanda unachotaka kuombea mkopo.
Paper hiyo inahusisha:
-Maelezo ya biashara
-Maelezo ya mhusika
-Maelezo ya kiwango cha mtaji
-Mchanganuo wa mgawanyo wa mtaji
-Maelezo ya vifaa na mashine zitakazohitajika kununuliwa
Mchanganuo wa matumizi
-Mchanganuo wa faida
-Mchanganuo wa urudishwaji wa mkopo
-Na maelezo mengine muhimu
1. Mtaji kuanzia Tsh. 100,000 - 500,000 - Paper unaandikiwa kwa Tsh. 50,000
2. Mtaji kuanzia Tsh. 501,000 - 2,500,000 - Paper unaandikiwa kwa Tsh. 150,000
3. Mtaji kuanzia Tsh.2,501,000 - 10,000,000 - Paper unaandikiwa kwa Tsh.250,000
4. Mtaji kuanzia Tsh. 10,001,000 - 50,000,000 - Paper unaandikiwa kwa Tsh. 350,000
5. Mtaji kuanzia Tsh. 50,001,000 - kuendelea- Paper unaandikiwa kwa Tsh. 500,000
Watu wengi waliofanikiwa wamefanikiwa kwa kupitia mikopo. Wafanyabiashara waliobaki nyuma wanalalamika mitaji lakini wenye kuthubutu ndio wanaotumia mikopo. Uzuri ni kuwa siku hizi taasisi nyingi za mikopo wanafikiria kutoa mikopo bila collateral hivyo hii ndio nafasi ambayo watu wengi wanaipenda. Usidanganywe, hakuna biashara inayoanzishwa isiyohitaji mtaji wa fedha
Kundi la walengwa wa kuandikiwa document hizi ni mtu yeyote anayetaka kuanzisha kiwanda kidogo au kikubwa, vikundi vya vijana, wanawake, SACCOS, wafanyabiashara, NGOs nk
Wasiliana nasi. Namba iko hapo juu