Tuna cha kujifunza katika "echo chambers" na anguko la demokrasia ya kiliberali

Mzalendo_Mwandamizi

JF-Expert Member
Dec 12, 2007
1,117
4,764
Demokrasia ya kiliberali ni mfumo wa kidemokrasia ya serikali ambapo haki za raia na uhuru wake hutambuliwa na kulindwa, huku matumizi ya nguvu za kisiasa yakidhibitiwa na utawala wa sheria.

Hata hivyo, matukio ya hivi karibuni yanaashiria kulegalega kwa mfumo huo na pengine ishara kuwa unaelekea kufariki. Baadhi ya matukio hayo ni pamoja na Brexit, kupanda na kupanda kwa Donald Trump, siasa za Italia kuhusu vyama cha Lega na 5 Star Movement, "mafanikio" ya Marine Le Pen huko Ufaransa, Viktor Orban huko Hungary, Law and Justice huko Poland, nk

Kuna sababu mbalimbali kuhusu anguko hilo, moja ikiwa ni "echo chambers" neno linalomaanisha hali ya kutaka kusikiana wenyewe tu. By "wenyewe" namaanisha "watu wenye itikadi/imani/mtazamo nk unaoshabihiana."

Kwa muda mrefu siasa za kiliberali zilionekana kutawaliwa na "maongezi baina ya makundi yanayoelewana." Wapenda haki waliongea na wapenda haki, ilhali wabaguzi hawakuwa na muda na wapinga ubaguzi. Wanasiasa nao walikuwa bize zaidi na siasa, kama ambavyo tabaka la juu la wasomi, matajiri, wataalam, nk lilivyokuwa bize kuongea "wao kwa wao."

Matokeo yake, tabaka la walalahoi ambalo ndilo lenye wanufaika na wahanga wa maamuzi ya tabaka tawala, lilijiona limepuuzwa. Na walipojitokeza watu kama Trump kuongea moja kwa moja na kundi hilo, we all know what happened. Na tabaka hilo "likawapa middle finger" wanasiasa, wasomi, nk na kukumbatia ujio mpya.

Labda ni desperation lakini kwa minajili ya mada hii, tunachojua ni kwamba wimbi jipya la siasa za aina mpya linatishia uhai wa demokrasia ya kiliberali.

Mimi ni muumini wa maongezi ya kistaarabu (civilised conversations) kama Swiss Army knife ya kupata ufanisi tele wa demokrasia, na ninaamini kuna funzo muhimu kwa Tanzania yetu, ambayo kama ilivyokuwa kwenye demokrasia ya kiliberali, maongezi yametawaliwa na echo chambers.

Jukwaa la siasa hapa Jamii Forums ni mfano mzuri kabisa. Ni vigumu mno kwa mtu wa CCM na Chadema kufanya maongezi ya kistaarabu pasipo kuitana majina ya ajabu, kutukanana, na upuuzi kama huo.

Ni vigumu mno kwa mtu wa Chadema kuikosoa CCM hata kama kukosoa huko ni kwa manufaa kwa CCM, kwani kabla hajamaliza hoja yake ataitwa "nyumbu" au majina mengine yasiyopendeza.

Kwamba mwana-Chadema ni Mtanzania mwenye haki ya kusikilizwa, na pia anayelazimika kuikosoa CCM, kwa vile ndio yenye dhamana ya kuongoza nchi yetu kwa sasa, haina fursa katika mazingira haya tuliyonayo.

Mwana-CCM nae haruhusiwi kuzungumzia yanayohusu Chadema au vyama vingine vya upinzani, kwa sababu ni dhambi, jinai na uhaini.

What's even worse, wahanga wa matusi ya upande mmoja ndio mabingwa wa matusi kwa yeyote wasiyeafikiana nae. YULE YULE mwana Chadema aliyeitwa "nyumbu" na mtu wa CCM, akikutana na hoja asiyoafikiana nayo, anageuka MBOGO kwa matusi. Ovyo kabisa!

Na sie ambao chama chetu pekee ni Tanzania yetu (Yaani tusio na vyama) ndio wenye wakati mgumu zaidi. Ukiikosoa CCM unaitwa hivi, ukikosoa upinzani unaitwa vile. Si ajabu hata kutumia tu mifano ya Chadema na CCM ikaibua matusi. Ndio tulipofikia hapa.

Matokeo yake watu wanaishia kuhadaiana wenyewe kwa wenyewe. Kupeana matumaini hewa. Kuwekeza nguvu kwenye matukio badala ya ajenda. Kujadili watu badala ya trends, essence, dynamics, na vitu kama hivyo.

Kilicho bayana ni kwamba kuzuwia kusikiliza hoja mbadala sio tu hakuzizuwii hoja hizo kuwa na impact bali pia kunachangia kupunguza options tarajiwa za kukabili changamoto mbalimbali.

Hizi "echo chambers" za kutaka msikilizane wenyewe kwa wenyewe zinaweza kuonekana mwafaka kwa wakati uliopo lakini kwa hakika zina athari kubwa tu kama ilivyotokea kwenye demokrasia ya kiliberali.

Ofkoz, kuna wenzetu ambao uwezo wao pekee wa kujibu au kujadili hoja ni kwa kutumia lugha chafu/matusi. Lakini ni wachache, hawana umuhimu katika discourses mbalimbali. Na hawa "dawa" yao ni rahisi: intelligence. Mtu mwenye matusi anaogopa sana mijadala inayofanyika intelligently. Chances are, atajiweka kando.

However, walengwa wa hoja yangu ni watu wenye uwezo mzuri kufanya nao conversations muhimu, na inasikitisha nao wanapokuwa mateka wa echo chambers, na kuishia ku-behave kama hao "mabingwa wa matusi."

Tafakari.

I stand to be corrected.
 
Baada ya kusoma, ningependa kuuliza. Je, tutegemee ujio wa mfumo upi baada ya kifo cha mfumo huu?
 
Mfumo wa MTU mmoja kuwa na nguvu na sauti kuliko wote hautoweza ivusha Africa, zaidi ya kuzalisha miungu watu na wengi kupotea kwenye umasikini
 
Hizi ni changamoto za kupima uimara /kufaa kwa Uliberali na bila shaka upande unaolinda Haki za raia zitashinda!
 
Chahali umeongea vizuri sana. Kwa sasa wengi tumetumbukia kwenye mtego wa imani zetu za kisiasa au itikadi kuliko hata kujari mustakabali wa Taifa letu.
Tuko tayari hata kudanganya ili mradi tupate kile tunachotaka, bila kujari gharama yake.

Mimi ni muumini mkubwa wa Pareto law...80/20. It is about those who make 20% to drive and make all the necessary changes we look forward to as a nation, matters. Tusiingie kwenye mtego eti wengi wape sababu wana siasa kwenye yale wanayoyaamini kila wakati wako wengi. Maana wanapata hapo chakula chao.
 
Demokrasia ya kiliberali ni mfumo wa kidemokrasia ya serikali ambapo haki za raia na uhuru wake hutambuliwa na kulindwa, huku matumizi ya nguvu za kisiasa yakidhibitiwa na utawala wa sheria.

Hata hivyo, matukio ya hivi karibuni yanaashiria kulegalega kwa mfumo huo na pengine ishara kuwa unaelekea kufariki. Baadhi ya matukio hayo ni pamoja na Brexit, kupanda na kupanda kwa Donald Trump, siasa za Italia kuhusu vyama cha Lega na 5 Star Movement, "mafanikio" ya Marine Le Pen huko Ufaransa, Viktor Orban huko Hungary, Law and Justice huko Poland, nk

Kuna sababu mbalimbali kuhusu anguko hilo, moja ikiwa ni "echo chambers" neno linalomaanisha hali ya kutaka kusikiana wenyewe tu. By "wenyewe" namaanisha "watu wenye itikadi/imani/mtazamo nk unaoshabihiana."

Kwa muda mrefu siasa za kiliberali zilionekana kutawaliwa na "maongezi baina ya makundi yanayoelewana." Wapenda haki waliongea na wapenda haki, ilhali wabaguzi hawakuwa na muda na wapinga ubaguzi. Wanasiasa nao walikuwa bize zaidi na siasa, kama ambavyo tabaka la juu la wasomi, matajiri, wataalam, nk lilivyokuwa bize kuongea "wao kwa wao."

Matokeo yake, tabaka la walalahoi ambalo ndilo lenye wanufaika na wahanga wa maamuzi ya tabaka tawala, lilijiona limepuuzwa. Na walipojitokeza watu kama Trump kuongea moja kwa moja na kundi hilo, we all know what happened. Na tabaka hilo "likawapa middle finger" wanasiasa, wasomi, nk na kukumbatia ujio mpya.

Labda ni desperation lakini kwa minajili ya mada hii, tunachojua ni kwamba wimbi jipya la siasa za aina mpya linatishia uhai wa demokrasia ya kiliberali.

Mimi ni muumini wa maongezi ya kistaarabu (civilised conversations) kama Swiss Army knife ya kupata ufanisi tele wa demokrasia, na ninaamini kuna funzo muhimu kwa Tanzania yetu, ambayo kama ilivyokuwa kwenye demokrasia ya kiliberali, maongezi yametawaliwa na echo chambers.

Jukwaa la siasa hapa Jamii Forums ni mfano mzuri kabisa. Ni vigumu mno kwa mtu wa CCM na Chadema kufanya maongezi ya kistaarabu pasipo kuitana majina ya ajabu, kutukanana, na upuuzi kama huo.

Ni vigumu mno kwa mtu wa Chadema kuikosoa CCM hata kama kukosoa huko ni kwa manufaa kwa CCM, kwani kabla hajamaliza hoja yake ataitwa "nyumbu" au majina mengine yasiyopendeza.

Kwamba mwana-Chadema ni Mtanzania mwenye haki ya kusikilizwa, na pia anayelazimika kuikosoa CCM, kwa vile ndio yenye dhamana ya kuongoza nchi yetu kwa sasa, haina fursa katika mazingira haya tuliyonayo.

Mwana-CCM nae haruhusiwi kuzungumzia yanayohusu Chadema au vyama vingine vya upinzani, kwa sababu ni dhambi, jinai na uhaini.

Na sie ambao chama chetu pekee ni Tanzania yetu (Yaani tusio na vyama) ndio wenye wakati mgumu zaidi. Ukiikosoa CCM unaitwa hivi, ukikosoa upinzani unaitwa vile. Si ajabu hata kutumia tu mifano ya Chadema na CCM ikaibua matusi. Ndio tulipofikia hapa.

Matokeo yake watu wanaishia kuhadaiana wenyewe kwa wenyewe. Kupeana matumaini hewa. Kuwekeza nguvu kwenye matukio badala ya ajenda. Kujadili watu badala ya trends, essence, dynamics, na vitu kama hivyo.

Kilicho bayana ni kwamba kuzuwia kusikiliza hoja mbadala sio tu hakuzizuwii hoja hizo kuwa na impact bali pia kunachangia kupunguza options tarajiwa za kukabili changamoto mbalimbali.

Hizi "echo chambers" za kutaka msikilizane wenyewe kwa wenyewe zinaweza kuonekana mwafaka kwa wakati uliopo lakini kwa hakika zina athari kubwa tu kama ilivyotokea kwenye demokrasia ya kiliberali.

Ofkoz, kuna wenzetu ambao uwezo wao pekee wa kujibu au kujadili hoja ni kwa kutumia lugha chafu/matusi. Lakini ni wachache, hawana umuhimu katika discourses mbalimbali. Walengwa wa hoja yangu ni watu wenye uwezo mzuri kufanya nao conversations muhimu wanapokuwa mateka wa echo chambers, na kuishia ku-behave kama hao "mabingwa wa matusi."

Tafakari.

I stand to be corrected.
Nilijua tu ni lazima uwataje chadema,halafu acha unafiki wewe una chama,na chama chako ni CCM ndo maana uliandika Kitabu cha kumsifia Dikteta uchwara Magufuli kinauzwa kwenye mtandao wa kbuuk .
Ungekuwa unaipenda Tanzania ni lazima ungekaa kwenye kundi la watanzania wanaoonewa,kuteswa,kusimangwa,kutekwa kuuawa na kupotezwa ambao wengi wao ni CHADEMA,unajitahidi sana kuficha uhalisia wako,lakini ni mjinga tu anayeweza kukuamini wewe,mtu anayeipenda Tanzania kama unavyojinadi usingekubali kuona CCM ikifanya ujambazi na kuivuruga nchi huku ukila Burger Scotland na kutucheka kuwa CHADEMA hatujiwezi kwenye ujasusi na tumewekewa wabunge ma spies mmoja akiwa wa mikoa ya Nyanda za juu Kusini,kama unaijua hiyo siri kwanini usingekisaidia chama na kumshinda nyoka CCM anayeiangamiza Tanzania ambayo unadai kuipenda?
Acha unafiki,endelea kula Burger Scotland, achana na Tanzania yetu.
 
Nimeelewa sana, hasa baada ya jana Waziri Mkuu wa England Theresa May kushinda kura za kuwa na imani nae
 
Back
Top Bottom