Asalam Aleykum wana jukwaa.
Leo nimeona niongelee hili suala la baadhi ya viongozi ambao kwa upande wangu nawaona kama hawana uwezo na wengi wana nafasi walizo nazo huenda kutokana na kubebwa na mfumo au kikundi cha watu au mtu fulani.
Hivi unakuwaje kiongozi mkubwa halafu unachoweza kuongea na watu wako pasipo kusoma ni ile kutoa salamu tu na kutaja majina yako?
Binafsi huwa nakosa kabisa hata hamu ya kusikiliza hotuba za hivyo maana huwa hazina mvuto.
Hivi kweli viongozi wetu wa sasa hawawezi kupita kwenye nyayo za watangulizi wao kama kina JK 1&2, JPM n.k.
Yote kwa yote, mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi. Nasubiri kwa hamu kuona kampeni zitakavyokuwa.
Ombi langu kwa raia wenzangu, naomba tuangalie wale wanaoongea kutoka moyoni kwa uchungu na uzalendo kama alivyokuwa Hayati JPM, 2015.
Napenda watu kaliba ya Mh. John Heche, Mh. Tundu Antipas Lissu, Mh. Humphrey Polepole, Mh. Jaffo, Wakili Msomi Mwabukusi, Pdr. Kitima, Ask. Mwanamapinduzi n.k.
Wengine naona wamepoa sana kama maandazi ya mhogo yaliyolala.
Jamani mnapokuja kuongea na sisi raia wenu, wenye changamoto nyingi za kila namna, basi changamkeni ili tusisinzia wekati mnatuhutubia. Tufurahie hata kwa kuwasikiliza tu.