Tumwambie mumewe ukweli au?

Tumwambie mumewe ukweli au?

caxton

Senior Member
Joined
May 8, 2015
Posts
145
Reaction score
157
Wakuu,

Kuna staff hapa kwenye shirika letu ni mke wa mtu ameshikwa live akifanya mapenzi na jamaa mmoja hivi ambae ni mume wa mtu pia ofisini bahati mbaya aliewashika ni bosi wao ambae ni Raia wa Canada. Walisubiri staff wengine waondoke ndipo wakaanza kufanya ndani ya chumba cha ofisi, unfortunately huyu mCanada akarudi ofisini alisahau kitu akaona taa zinawaka kwenye chumba kingine akaamua aangalie kama bado kuna mtu, ndio akawafuma wakifanya zinaa.

Kwa sasa tumewasimamisha wakati uchunguzi ukiendelea kama sheria za kazi zinavyotaka na policy ya shirika pia, tayari walishaleta barua za kujieleza. Hivi karibuni mume wa huyu mama kaja kuniona kupata undani wa tatizo la mkewe, alitaka kujua ni kwanini tumemsimamisha mkewe kazi na tumetumia vigezo gani.

Bahati mzuri/mbaya malalamiko yake ameweka kwenye maandishi kwa njia ya barua ni mzee wa kikoloni hivi very conservative. Nikamwambia nitakujibu kwa barua pia utaikuta kwa secretary siku flani.Sasa wakuu miim kama Human Resources business partner wa hapa kwetu nalazimika kutunza siri za staff, tumelichanganua na wenzangu wakadai hatuwezi kumficha mume jambo zito kama hili.

Hivyo bado sijaridhika na majibu ya viongozi wenzangu hivyo nije kwenu wana JamiiForums kupata opinion zaidi maana humu nna uhakika kuna viongozi maofisini na kuna wasomi wengi tunaweza kuchanganua kwa pamoja suala hili. Mara ya mwisho nilikuwa na tatizo la kikazi kama mjuavyo idara ya Human Resources ina changamoto nyingi nikaja hapa kuomba ushauri nikapata msaada mkubwa sana.

Naomba nisieleweke vibaya, yapo mambo ya kikazi yana vikao vyake hayahitaji kuja hapa ila kuna yale ya kikazi ambayo yamekaa kijamii kama hili yenyewe nimeamua niwe nawashirikisha kwa mawazo.

Swali;
Nimjibu mume kwamba mkewe alishikwa akifanya mapenzi ofisini?

Mkewe kaja kazini Jana na kunipigia magoti kwamba nimdanganye mumewe kuwa amesimashwa kaingizia kampuni hasara.Kwamba mimi ndio nimeshikilia ndoa yake kwa sasa, kwamba akiachika na umri huo ataenda wapi?Situation ni very tricky na mwisho sijui EXCOM itaamua nini kuhusu hawa watu wawili

Your opinion please

NB:
Kama wahusika wa hili sakata wamo humu ndani, I do regret in advance for inconvenience caused in one way or another.
 
Dhambi ya uzinzi hata kwenye Biblia ndio imeruhusiwa watu kuachana. Huyo mwanamke ni mpumbavu, kama alitaka kufanya uzinzi angeweza kufanya hata Gesti ila sio ofisin kwa mtu. Ipo siku ataweza mleta mwanaume kitandani kwa mmewe.
Mimi nashauri mume aambiwe ukweli, ukweli ukijulikana utasaidia kufumbua tatizo lako, kufumbatia maji kama jiwe ni ujinga. Mpeni tu ukweli, siku zote ukweli unaleta haki na Na uongo haudumu.
 
Kama story hii ni ya kweli basi huyo mama ni mpuuzi na hastahili kuonewa huruma ama kufichiwa siri. Kama alijua alichokuwa anakifanya ni kibaya, kwa nini alikubali kufanya hivyo tena ndani ya ofisi? Si basi wangekwenda hata hotelini au guest house?

Halafu huyo mume wake inakuwaje anakuja kutaka kujua kwa maandishi ni kwa nini mmemsimamisha kazi mke wake? Kwani nyie kama ofisi mna uhusiano gani na huyo Bwana mpaka awatake maelezo kiofisi? Mjibu kwa urahisi huyo mume kwamba sababu zilizofanya mke wake asimamishwe ni za kiofisi na anayezijua ni mke wake, hivyo akamuulize mke wake. Huyo mume kwenu ni third party na hana haki ya kujua ni kwa nini mmemchukulia hiyo hatua mke wake. Amuulize mkewe.

Tiba
 
Barua ya kumsimamisha kazi (heading yake) inasemaje? Kwa sababu usije ukamdanganya Mr. wake akadai kopi au wanoko wameshampa kopi sasa anataka uthibitisho kutoka kwako maelezo yakapishana au mmewasimamisha bila maandishi? Eleza Mkuu
 
Pole kwa huu mtihani mgumu. Hilo la kumwambia ukweli mume liepuke hasa ukitilia maanani mke kishakupigia magoti umsitiri kwenye ndoa yake. Ila kama mume yumo humu ndio siri ya mkewe kuhusu kusimamishwa kazi imeshavuja.
 
caxton

Fata utaratibu na misingi ya kazi yako inataka nini coz umewasilisha kikazi ...but kwa ziada hauna sababu ya kuficha lolote baada ya hapo lolote ufichalo likaleta madhara wewe utahusika
 
Last edited by a moderator:
Pole kwa huu mtihani mgumu. Hilo la kumwambia ukweli mume liepuke hasa ukitilia maanani mke kishakupigia magoti umsitiri kwenye ndoa yake. Ila kama mume yumo humu ndio siri ya mkewe kuhusu kusimamishwa kazi imeshavuja.

Mkuu BAK, kwani ofisi ina wajibu gani wa kumwambia mume kwanini mke amesimamishwa kazi? Huyo mume si amuulize mkewe? Hivi kesho mjomba mtu akija akaandika barua kutaka kujua kijana wake anayefanya kazi pale analipwa shilingi ngapi huyu HR atakuja tena hapa kutuuliza afanyaje? Huyu HR naye nina wasiwasi na qualifcations zake!!!!

Tiba
 
atanieleza leo nikifika nyumbani,yaani anafanya umalaya ofisini kwake alafu ananidanganya mimi
 
Pole kwa huu mtihani mgumu. Hilo la kumwambia ukweli mume liepuke hasa ukitilia maanani mke kishakupigia magoti umsitiri kwenye ndoa yake. Ila kama mume yumo humu ndio siri ya mkewe kuhusu kusimamishwa kazi imeshavuja.
Bro, mumewe kapeleka malalamiko akihitaji malalamiko kwa maandishi, na itabidi wamjibu kwa maandishi pia.

Now, wakidanganya na Jamaa akaamua kufuatilia kwenye vyombo husika, ni issue nyingine kubwa sana. Besides, i'm sure huyo bi Mkubwa atakuwa kajaribu sana kumueleza mzee kilichotokea but he didn't buy it, ndio maana kawatega kwa maandishi tena.
 
Kama story hii ni ya kweli basi huyo mama ni mpuuzi na hastahili kuonewa huruma ama kufichiwa siri. Kama alijua alichokuwa anakifanya ni kibaya, kwa nini alikubali kufanya hivyo tena ndani ya ofisi? Si basi wangekwenda hata hotelini au guest house?

Halafu huyo mume wake inakuwaje anakuja kutaka kujua kwa maandishi ni kwa nini mmemsimamisha kazi mke wake? Kwani nyie kama ofisi mna uhusiano gani na huyo Bwana mpaka awatake maelezo kiofisi? Mjibu kwa urahisi huyo mume kwamba sababu zilizofanya mke wake asimamishwe ni za kiofisi na anayezijua ni mke wake, hivyo akamuulize mke wake. Huyo mume kwenu ni third party na hana haki ya kujua ni kwa nini mmemchukulia hiyo hatua mke wake. Amuulize mkewe.

Tiba

huo ndio ushaur wa kiutu uzima na hawez kuja tena ofisin wapambane na mume wake wala sio ww atakachoambiwa na mke wake ndio hicho
 
Mkuu mume hana mamlaka yoyote ya kufuatilia kilichojiri kati ya mwajiriwa (mkewe) na mwajiri. Wanaweza kuamua kumpotezea pia kwamba kama mwajiri hawana obligation yoyote ya kumwambia sababu ya mkewe kusimamishwa kazi.

Bro, mumewe kapeleka malalamiko akihitaji malalamiko kwa maandishi, na itabidi wamjibu kwa maandishi pia.

Now, wakidanganya na Jamaa akaamua kufuatilia kwenye vyombo husika, ni issue nyingine kubwa sana. Besides, i'm sure huyo bi Mkubwa atakuwa kajaribu sana kumueleza mzee kilichotokea but he didn't buy it, ndio maana kawatega kwa maandishi tena.
 
Poleni san!
Mume hana haki ya kuuliza kwa nini mke wake kasimamishwa kazi kwa kuwa siyo mwajiri wake na wala sio mmiliki. Mkataba wa kazi unamjua mwajiri na mwajiriwa. Kama huyo mwajiriwa ndo analalamika ungekuwa na haki ya kumweleza kosa lake. In short hayo wakaulizane nyumbani wao wenyewe. Yeye mume anakuuliza kama nani! Ana uhusiano gani na nyie! Aache kiherehere!
Kwa kuzingatia ubinadamu wa kawaida kabisa kila binadamu anastahili kuonewa huruma! Umri wake kwa kweli kama umeenda anahitaji huruma ya kufichiwa hii siri! Sio lengo langu kuubariki ubazazi alioukuwa anafanya lengo ni kunusuru pia familia. Baadhi ya wengi wanaofanya kazi mafisini wanakumbwa na madhila haya. Ama kwa kupenda ama kushawishiwa ama hata kulazimishwa kwa sababu mbalimbali. So ni uamuzi wenu ama mzalishe watoto yatima ama muamue kuokoa familia hii!
Itoshe kumwambia kuwa mke wa huyu mzee anayetaka kuwa juu ya Shirika lenu kuwa mkewe hakukidhi viwango na matakwa ya kampuni, na shirika haliko tayari kuendelea na watu wa aina yao.
 
Watu wengine ni kichefuchefu. Akiachika ataenda wapi? Huyo mama wa ajabu kweli. . .aende kwa huyo aliyekuwa anazini nae ofisini.

Anyway, kwasababu ni ishu za kazi ni vizuri ukweli ukasemwa ili yasitokee matatizo mengine mbeleni. Maana unaweza ukasema umdanganye huyo mumewe alafu nae akatafuta namna nyingine ya kupambana na nyie kwa nia ya kumtetea mkewe bila kujua ukweli wa mambo. Bora ajue, maisha yaendelee.
 
Mkuu mume hana mamlaka yoyote ya kufuatilia kilichojiri kati ya mwajiriwa (mkewe) na mwajiri. Wanaweza kuamua kumpotezea pia kwamba kama mwajiri hawana obligation yoyote ya kumwambia sababu ya mkewe kusimamishwa kazi.
Well, nadhani kila ofisi ina utaratibu wake, na according to the story inaonyesha hiyo ofisi wako obliged kufanya hivyo, ndio maana wamemuahidi watamjibu na wameshajadili namna ya kumjibu pia.
 
Back
Top Bottom