Tumuenzi kwa vitendo, Sokoine marathon 2019

wandamba

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
510
839
Ni miaka 35 imepita tangu Kiongozi imara, jasiri, shupavu Edward Moringe Sokoine afariki Dunia kutokana na ajali mbaya ya gari.

Hakuna asiyejua uimara, uzalendo na uchapakazi wake Edward Sokoine na hasara ambayo Taifa ilipata kutokana na kifo chake.

Maadhimisho ya Mwaka huu ya kumbukizi ya kifo chake yanaanza kwa mbio za Sokoine (Sokoine Memorial Marathon) zitakazofanyika tarehe 6 Aprili, 2019 kuanzia mnara wa saa mpaka uwanja wa mpira wa Sheikh Amri Abeid Sokoine jijini Arusha.

Shime Watanzania twendeni tukamuenzi kwa vitendo Mzalendo Sokoine, twendeni tukajumuike na mgeni rasmi Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na Wasanii wa Bongo movies kwenye mbio hizo siku ya Jumamosi Aprili 6, 2019.

Kauli mbiu ya mbio hizi ni *"Tumuenzi kwa Vitendo, Utaifa Kwanza"*
FB_IMG_1554481057430.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom