KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 3,117
- 5,321
Mwenyezi Mungu aendelee kusimama na kila mmoja na kusimama na Taifa letu. Ni imani yangu bado kila mmoja anakusudi la kweli katika kudumisha amani, kukuza umoja wa kitaifa na kusimamia misingi ya haki.
Katika mengi ,nami nawiwa kutoa mchango wangu wa machache .Kama mtanzania natambua mchango wangu ni muhimu katika ujenzi wa kweli wa Taifa. Mchango wangu utajikita katika kuangazia nia, kusudi na dhamira ya mhe.Rais katika maridhiano na ujumbe maalumu wa kumuelewa.
Katika hotuba yake ,sehemu ya hotuba hiyo Mhe. Rais alisema , namnukuu "Tumesema tuzungumze, lakini wengine wanakuja na masharti, 'mumuachie huyu, mfanye hili na hili'. Huu si utaratibu wa nchi inayoheshimu mamlaka yake."
Katikati ya maneno hayo Kuna ujumbe mzito wa kusudi na nia ya mhe.Rais kutaka kufanya mazungumzo ( maridhiano). Kusudi la Mhe. Rais ni kufanya maridhiano yenye kujenga upya Taifa, maridhiano yenye kuteta umoja wa kitaifa na maridhiano yenye kuleta uponyaji na amani ya kidumu na sio kufanya maridhiano na kikundi, mtu, Chama ,dini fulani n.k.
Mhe. Rais ana kusudi jema na dhamira yake ya kujenga upya imejengeka katika nia yake ya dhati ya kufanya maridhiano ya kweli. Uzi huu niliona kusudi na nia njema ya Mhe.rais na Leo naizungumzia nia hiyo ili wote tumuelewe Ushauri kwa vyama vya upinzani: Nia na dhamira ya Rais Samia ni njema , tutamkumbuka.
Binafsi nalielewa kusudi na nia ya Rais Samia katika maridhiano ni pamoja na:
1. Kuzungumza kwa lugha moja ya kuliimarisha na kulijenga Taifa katika umoja na mshikamano katika nyanja zote
2. Kupata njia Bora zaidi za utatuzi wa changamoto( za kisiasa, kiuchumi na kijamii) na zenye kuleta maelewano mazuri
3. Kufanikisha ujengaji mifumo Bora katika Taifa itakayosaidia upatikanaji wa haki, maendeleo ya Taifa, kujitegemea
4. Kulijenga Taifa katika misingi ya kujitegemea na kutegemea ilichonacho kuliko kutegemea wahisani na mikopo
5. Kutupatia katiba ambayo itakidhi nahitaji na matarajio ya vizazi vingi vijavyo .
6.kuweka misingi na mipaka ya miingiliano kati ya Taasisi na Taasisi na kila Taasisi kusimama katika misingi ya uanzishwaji wake.
Ukiniuliza kusudi na nia gani aliyonayo Mhe. Rais kuhusu maridhiano, Mimi naziona ni hizo na nimemuelewa mhe. Rais, sasa ni wakati wa kumuelewa ili Taifa lione matokeo ya nia hiyo.