political monger senior
JF-Expert Member
- Nov 26, 2020
- 1,873
- 6,136
TUMSIKILIZE POLEPOLE, LAKINI TUSISAHAU.
Enzi zile za Magufuli, Watu kama Jakaya walionekana ni Watu wazuri sana.
Kwa sababu Jakaya alikuwa nie ya Mfumo ambao 'ulichukiwa na wengi na kupendwa na wengi (walionyimwa fikra).
👉 "Bora enzi za Jakaya", Ni Kauli ambazo ungezisikia huku na kule.
Naam, kulikuwa na Ukatili wa kutisha..
Adadi Rajabu Meta, aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) na wakati huo akiwa Mbunge wa Muheza aliongoza Kamati ya Bunge ya Ulinzi na Usalama kufanya Uchunguzi wa matukio ya Uhalifu wa Kuteka, Kutesa na Kupoteza Watu. Kabla ya kusomwa Bungeni taarifa ile ilipeperushwa kusikojulikana. Ni nyakati za Magufuli.
Ni enzi za Magufuli ambapo baadhi ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu wenye mitazamo ya Upinzani walifukuzwa Vyuo kwa Maelekezo ya Humphrey Polepole, akiwa Katibu Mwenezi wa CCM na Mlezi wa Jumuiya ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu. Rekodi ikae hivyo kama ilivyo.
Hivi sasa wakati Humphrey Polepole akifichua maovu ya Utawala uliopo, ambayo nakubali ni kazi ya kizalendo sana na ni vema akaendelea nayo, bado napata shida na Watu wanaomuhusudu Humphrey Polepole.
Nataka kusema nini ???
"Humphrey Polepole asikilizwe lakini asisahauliwe. Binafsi bado sijaweza kupambamua malengo na makusudi ya Ndg. Humphrey Polepole,
Lakini mambo kadhaa yananipa picha fulani!
Kwanza, kitendo cha wasiojulikana kuvamia nyumbani kwa Ndugu yake, inatoa picha kwamba anawindwa.
Kwa tafsiri nyingine Humphrey Polepole tayari ni Muhanga wa Matukio ya kuteka, kutesa, kuua na kupoteza kwa sababu wafanyao hayo matukio wamemgusa (kwa kuvamia nyumba ya Dada yake wakimtafuta yeye).
Je! Anaowatuhumu, anaowashitaki kwa Umma ndio haohao wanaomtafuta ???
Wakati unajiuliza Swali hilo kumbuka haya matukio yalikuwako pia kwa kiasi kikubwa sawa na sasa enzi za Magufuli.
Pili, kitendo cha Humphrey Polepole kujificha na kutofahamika alipo, maana yake hayuko peke yake.
Naam! Mtu mmoja Humphrey Polepole hawezi kuwa peke yake halafu akajificha na akawa anarekodi video na kuzirusha kila Siku. Lakini kubwa zaidi ni taarifa anazotoa, sio taarifa za kichwa kimoja. Ni kundi.
Tatu, Ni kundi lisilo na nguvu. Na kwa hiyo 'labda linatafuta nguvu ya kuungwa mkono na umma' ambayo kwa Tazania inaweza isisaidie sana taifa kwa sababu umma wa nchi hii ni Umma mnyonge na taabani.
Ni Umma ' Vulnerable' usioweza kujitetea na kwa hiyo unahitaji kutetewa. Kundi hili la Humphrey Polepole lingekuwa na nguvu, kwa uchafu huu unaosemwa na Polepole, lingepaswa 'KUTENDA' na sio kupiga kelele mafichoni.
Mwisho, Tumsikilize Polepole. Anafanya kazi nzuri ya kizalendo, na wakati huohuo tusisahau kwamba, hatutapa Taifa la maana chini ya CCM, iwe ni ya Jakaya na Rostam, au Polepole na Gwajma.
Afrika inahitaji mifumo imara ya kitaasisi, na sio Watu Imara - Barack Obama.
Nawasilisha. Political monger..