Tumshukuru mungu kwa kutuepusha na aibu ya mashindano ya “CAF champion league” 2019/2020

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Jan 30, 2012
1,989
1,177
Katika mashindano ya “CAF Champion League” 2019/2020 Tanzania iliingiza timu mbili ambazo ni Yanga FC na Simba Sc.

Kutokana na mafanikio ya Simba Sc katika msimu uliopita wa mashindao haya, watanzania wengi walikuwa wakitamani au kuomba Tanzania iingize timu mbili katika round ya 16 (Group stage) kama ilivyozoeleka sasa kwa nchi kama Morocco, Tunisia, Algeria, Zaire (Congo DRC) na Misri (Egypt).

Kutokana na maandalizi hafifu ya timu za Yanga FC na Simba Sc zilishindwa kufikia ndoto za watanzania wengi huku timu toka katika nchi zenye misukosuko ya kiuchumi kama Zimbabwe (Platinum FC) na Misukosuko ya kiusalam kama Sudan (Al Ahal) zikiingiza timu mojamoja katika round ya 16 (Group stage).

Zikiwa timu zote zimeshacheza michezo minne katika kila kundi, inaonekana dhahiri kwamba “CAF Champion League” 2019/2020 ni tofauti kabisa na ile ya 2018/2019 kwani timu zote ukiondoa Al Ahal ya Sudani tulizoshangaa zimeingiaje round ya 16 (Group stage) mfano Zesco ya zambia, Platinum, timu mbili za Angola na hata AS Vita ya Congo DRC zimekutana vipigo vitakatifu nyumbani na ugenini.

Kwa mtizamo wangu, watanzania yamkini wanatakiwa wakatoe sadaka za shukrani misikitini au makanisani kwa kuiepusha nchi na aibu kubwa kama timu zetu za Simba Sc na Yanga FC zingefika round ya 16 ya “CAF Champion League” 2019/2020.

Baada ya kila timu kucheza michezo mine, yatokeo yanasimama kama ifuatavyo

CAF.png
 
Katika mashindano ya “CAF Champion League” 2019/2020 Tanzania iliingiza timu mbili ambazo ni Yanga FC na Simba Sc. Kutokana na mafanikio ya Simba Sc katika msimu uliopita wa mashindao haya, watanzania wengi walikuwa wakitamani au kuomba Tanzania iingize timu mbili katika round ya 16 (Group stage) kama ilivyozoeleka sasa kwa nchi kama Morocco, Tunisia, Algeria, Zaire (Congo DRC) na Misri (Egypt).

Kutokana na maandalizi hafifu ya timu za Yanga FC na Simba Sc zilishindwa kufikia ndoto za watanzania wengi huku timu toka katika nchi zenye misukosuko ya kiuchumi kama Zimbabwe (Platinum FC) na Misukosuko ya kiusalam kama Sudan (Al Ahal) zikiingiza timu mojamoja katika round ya 16 (Group stage). Zikiwa timu zote zimeshacheza michezo minne katika kila kundi, inaonekana dhahiri kwamba “CAF Champion League” 2019/2020 ni tofauti kabisa na ile ya 2018/2019 kwani timu zote ukiondoa Al Ahal ya Sudani tulizoshangaa zimeingiaje round ya 16 (Group stage) mfano Zesco ya zambia, Platinum, timu mbili za Angola na hata AS Vita ya Congo DRC zimekutana vipigo vitakatifu nyumbani na ugenini. Kwa mtizamo wangu, watanzania yamkini wanatakiwa wakatoe sadaka za shukrani misikitini au makanisani kwa kuiepusha nchi na aibu kubwa kama timu zetu za Simba Sc na Yanga FC zingefika round ya 16 ya “CAF Champion League” 2019/2020.

Baada ya kila timu kucheza michezo mine, yatokeo yanasimama kama ifuatavyo

View attachment 1321605
Vp Esperance?
 
Bado sioni sababu ya watanzania kutoa shukrani, kwasababu kitendo cha timu zetu za Tanzania kufanikiwa kuingia hatu ya makundi ingesaidia kuongeza point kwa nchi yetu. Na la pili kuna kiwango cha pesa kinatolewa na CAF kwa timu zilizofanikiwa kuingia hatua ya makundi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom