Tumshauri wote jamani, mimi nimeshindwa

Tumshauri wote jamani, mimi nimeshindwa

poa tu

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2016
Posts
1,173
Reaction score
1,657
Rafiki yangu kaoa miaka takribani minne hivi iliyopita ila yeye na mkewe wapo mikoa mbalimbali kutokana na ajira. Tangu mwishoni mwa mwezi jana nimeanza kuhisi jambo tofauti kwa huyu jamaa. Yupo stressed, kabadili tabia za unywaji vileo (analewa mno), utendaji wake kwenye kazi unadorora. Baada ya wiki kadhaa za kumpeleleza leo kaamua kunifungukia yanayomsibu, ipo hivi:

Mwaka 2015 akiwa kikazi mkoa fulani alikutana na binti fulani ambaye ndio kwanza alikuwa kamaliza mafunzo ya taaluma fulani. Akiongozwa na pepo la michepuko akatumbukia uzinzini na kabinti haka (karembo ka haja) hadi bibie akapata ujauzito. Swahiba kamaliza majukumu yake, karudi kituoni kwake huku akifanya siri nzito suala hili. Amelea ujauzito hadi mtoto kazaliwa na ana mwaka na miezi sasa bado ilikuwa siri (hakuwahi hata kunidokeza).

Sasa tatizo likaanza mwezi uliopita. Ule mchepuko umeangukiwa na nyota ya jaha umepata kazi na kupangiwa kituo anachofanya kazi shemeji yangu huyu (mke wa jamaa yangu huyo). Balaa la mwaka ni kwamba mchepuko umefanikiwa kupata makazi nyumba HIYO HIYO aliyopanga shemeji na funga kazi ni kuwa kuna kila dalili ya kuwa shemeji na mchepuko wameelewana sana tu (mashosti) ila hawafahamiani kabisaa.

Jamaa alikuja kung'amua hali halisi baada ya kutumiwa meseji na mkewe kuhusu "shoga" yake mpya. Kuna meseji imeniacha hoi hyo Whatsapp inasema "baby jamani huyu shost yangu ana katoto mmefananaaa, halafu kachangamfu nakapendaaa" meseji imembatanishwa na picha mujarabu kabisa ya kijana wetu (hata mimi nimekiri), what a coincidence!!! Huyu shemeji yangu bado hajabahatika kupata mtoto achilia mbali ujauzito.

Waungwana kuna vitu ombeni tu muishie kuviona Bongo movie. Sasa sijui hata namshauri nini, hizi ni lawama maana hapa najua litalofuata ntaambiwa nilikuwa nafahamu vyema. Hapa ukizingatia juzi tu nimesuluhisha ugomvi wao kuhusiana na jamaa kugoma kwenda wakati wa sikukuu zilizopita wakati likizo anayo.
 
Wakati mwingine nasikia kuwa "Mwenyezi Mungu hafichi uchafu".

Mwambie apambane na hali yake kama alivyokuwa ana mbaolojia huko kwa siri.
 
Mwambie auze hio nyumba.asingizie anadaiwa na akutumie wewe umsaidie kuuza hio nyumba.
 
Nanyi mmezidi kufungua zipu zenu hovyo jamani poo! Mwambie anywe mpaka akate roho mbavu kabisa maana kipindi anazinzika hatukuepo na hakutushirikisha ....
 
Kama Dini inamruhusu avute ndani na kuoa huyo "shosti" wa mke wake ili nyumba ijae furaha na baraka. Mwanaume hatishiwi Nyau. Vijana wa siku hizi mnatuangusha sana .
 
uongo huu! halafu tumshauri wote yuko wapi? kaomba ashauriwe?
 
Swali jepes ni kwamba huo mchepuko unajua kama jamaa kama ameoa?
If Yes then ampigie simu amwambie tu ukwel nyumba uliyopanga uko na mke mwenzio
Kama mchepuko smart utaelewa na atahama kama sio smart bas ndio atajua kwann China wana Mwaka mpya wao.
 
Back
Top Bottom