Mdogo wangu mtoto wa aunt amekuja kwangu leo asubuhi akilalamika Kwamba mwanaume aliyekuwa anampenda ghafla amekata Kamba baada ya yeye kuwa mjamzito. Anadai mwanaume hataki hata kumuona japo hajakataa mimba. Hata a mwambie anaumwa hawezi kuja kumuona lakini yupo mji huo huo.
Anadai amelia mpaka amechoka. Anapomuomba matumizi huyu mwanaume huwa anatoa hivyo hivyo kwa shida Ila akimuomba awe karibu nae hataki anamwambia ana matatizo ya kifamilia hivyo yakiisha atakuja nyumbani waishi wote.
Mdogo wangu anaumia kisaikolojia kama mjuavyo mambo ya mimba halafu ameachwa peke yake hapo ndani hata akiumwa Hana wa kumpikia hata chai. Amewaelezea ndugu lakini mwanaume akiulizwa anasema nampa matunzo na hakuna tatizo ni mimba tu inamsumbua.
Nimemuuliza historia ya huyu mwanaume akadai amezaa watoto wa2 wanaotambulika kila mmoja na mama yake na aliwahi kufunga ndoa na mwanamke mwingine ambaye hawana mtoto na walishagombana hawapo pamoja mda mrefu sana.
Yeye alichoamua ni kuvumilia ajifungue salama maana machozi amelia sana kisha akishajifungua tu amplekee mwanaume mwanae atajua atamleaje ili iwe fundisho maana kazi yake ni kuzaa hapa na pale akijua wanawake watalea. Anadai maumivu aliyopitia kisaikolojia ni nazito sana hivyo yupo tayari kuitwa mnyama au mwenye roho ngumu.
Binafsi hili limeniwia zito sana imebidi nimwambie apumzike kwanza tutaongea badae ili angalau nisije kukurupuka.
Wadau kama ni nyie mngemshaurije Huyu binti mwenye maumivu makali moyoni?