Tumshauri Msajili wa Vyama vya Siasa suala la dini nalo liwe 50/50 Tanzania

battawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
2,672
2,540
Wakati taifa letu linazidi kusonga mbele kidemokrasia,kuna kila dalili za kuvunjika kwa umoja wakitaifa ambao ndio msingi na tunu kuu ya Tanzania.
Aidha kuna dalili za ukabila na ukanda nazo zinajitokeza kwenye siasa zetu ,na kuna mawakala wanazipalilia humu nchini.

Kwa kuepuka mivutano isyokuwa ya lazima huko mbeleni kwa vizazi vijavyo
inatupasa tufikiri vyema ni namna gani mambo haya tunayawekea misingi isiyotetereka.

Kimsingi ,katiba yetu imeweka wazi kuwa uongozi wa nchi hii hautatolewa kwa kabila wala dini fulani, na kufanya hivyo ni makosa kisheria,
Iweje basi baada ya mtu kuchaguliwa kwa taratibu za kikatiba ya nchi atokee mtu aanze kuimba wimbo wa kabila, kanda au dini?
Jee Kufanya hivyo kwa kutuhumu nako si kosa kisheria?
Yawezekana katiba yetu inalazimika iongezewe meno ili kuzuia mtu kufanya hivyo kwa namna yoyote ile aidha kuzuia tuhuma za namna hii.
Lakini pia izingatiwe kuwa lisemwalo lipo,na kama halipo liko njiani laja.
Je Munadhani Dini na Ukanda au ukabila navyo vizingatiwe kwenye Vyama vyetu na Uongozi wa Serikali?

Mfano:-
- Waislamu wamekuwa wakilalamika sana nchini juu ya kuwepo upendeleo katika ajira za Umma. Waislamu pia hulalamika kuhusu kuchagulwa katika Elimu ya Juu kuwa nazo hutolewa kwa upendeleo wa dini.
-Mzee Jumbe,aliyekuwa Makamu wa pili wa Raisi Tanzania na Raisi wa Zanzibarpia naye alituhumu hilo kwenye kitabu chake ''The partner ship''
- Tundu lisu aliwahi kutuhumu Serikali ya awamu ya Magu. kuwepo na Harufu ya ukanda ya ziwa.
-Mwal. Nyerere aliwahi kutuhumu Zanzibar kuwepo upemba na unguja.
-Kule Zanzibar baada ya Uchaguzi 2 wa Jecha,Wana CCm walifanya maandamano siku ya kuapishwa Dr.Shein na Kubeba bango lililosema kuwa ''Machotara waondoke Zanzibar si kwao'',Hadharani .Hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi ya waliofanya vile,kwa maana hiyo ile ndio sera ya CCM.na wamebariki tendo lile.
-Huenda tuhuma hizi zikawa na Msingi fulani ,na kwa hiyo ziwekewe taratibu kabla hazijakuwa 'cronic' hasa kwa kizazi kijacho ambacho huenda kisiwe na busara kama za kwetu sisi tulio ishi na Nyerere


Kwa minajili Nashauri Sharti la kabila,dini,ukanda viwekewe mchanganuo kwenye katiba yetu na iwe jinai kwa mtu kutuhumu kwa njia hizo baada ya taratibu za kidemokrasia kutumika katika chaguzi zetu


Nawakilish
Tuchukuwe tahadhari na sumu ya Udini,Ukabila na Ubaguzi wa aina yoyote wa rangi na jinsia
Epuka Ubaguzi,Taifa litaangamia.
 
Back
Top Bottom