Tumshauri Dr. Joyce Ndalichako

kwa ushauri zaidi aende kwa yule jamaa mwenye mvi nyingi sana ambae wafwasi wake wanazungusha sana mikono nakumbuka ni kama yeye alikua haishi kuitaja wizara hii sizani kama atatoka patupu
 

Nimajungu na wivu wenu ti
 

Kwanza azui sera ya elimu bure fedha hizo zipelekwe kwenye kununua vitabu,walimu waboreshewe maslahi, maktaba, maabara na kurudisha heshima ya shule za serekali kama Umbwe na akina kibaha nasikitika kila kukicha shule kongwe zinazidi kuchoka
 
Bi.Joyce anza kutambua daraja la watu wenye masters na PhD ktk ngazi za mishahara ya walimu, tofauti ilivyo Sasa ambapo hakuna ngazi ya mshara kwa mtu wa elimu ya uzamili au uzamivu kwa kada hii. Tunahtaji walimu wabobezi ktk taaluma zao, hii italeta tija
 
ukweli elimu yetu inahitajii, kuwa reformed upya siasa imeharibu kabisa mfumo wa waalimu,
1. uboreshaji wa mitaala
2.vifaa vya kijifunzua na kufundishia.
3. kurudisha heshima kwa waali, kwa kuboresha maslai yao, na kuwalipa madeni yoote.
3. nyumbaa na madarasa ya waalimu.
4 kupeleka huduma zote za kijamii vijijini.
5.kufuta waraka kandamizi kwa waalimu.
6. matumizi mabaya ya raslimali watu, mwl ana digree anafundusha darasa la pili wakati afisa elimu, mkaguzi, mratibu elimu kata, mwl. mkuu anasartificate au diploma,inawapa wakati mgumu hata viongozikuwasimamia hawa nayite haya nikwaajili ya undugu na ujamaa,
 
Apuuzie wote wanaoaka kukifuta kiingereza kama lugha ya kufundishia!
Walimu wa shule za msingi waendelee kupata kozi za kiingereza na hisabati kwenye 'CLUSTERS' zao, maana tunajua haya masomo walimu wengi wanachapia!
REPEAT AGAIN: BORESHA KIINGEREZA NA HISABATI SHULE ZA MSINGI!
 

nakuunga mkono kiingereza
 
akatae ushauri WA waislamu waliomshinikiza mpaka wakamtoa NECTA
 
Pointi yako namba 6 ina ukweli kabisa. Ni jambo la kusikitisha kuona maofisa wa elimu katika ofisi ya elimu wilaya,wakaguzi na waratibu elimu kata wengi wao wana vyeti (certificates) tu wakati kuna walimu wengi wenye Shahada wapo madarasani. Mathalani katika halmashauri ya wilaya ya Masasi waratibu elimu kata karibu wote wana astashahada (cheti) na wachache wana stashahada wakati waraka wa elimu unataka waratibu elimu kata wawe na Shahada na walimu wakuu wawe na stashahada. Katika hili wanaokwamisha utekelezaji wa waraka huo ni waajiri na wakuu wa idara kwani hawataki kutekeleza kwa makusudi au kwa kuogopa kuwaondoa wale wasiokuwa na sifa na kuwaweka wenye sifa. Hili ni jipu linahitaji mtumbuaji kwani limewashinda wenye mamlaka.
 

Mkuu,utakuwa unaishi kwa misingi ya kijima kabisa.Kweli JF Imevamiwa.A nonsense comment.
Mleta uzi amekuja na idea nzuri sana,kama una hoja inayoweza kusukuma mbele elimu yetu,ni bora ukatoa.Kama hauna hoja si lazima uzungumze.Mshairi mmoja anasema,namnukuu"...nimekuwa nikijuta sana kwa kusema,lakini sijawahi kujuta kwa kukaa kimya..."
Tanzania ni kubwa kuliko kijiji unachoishi,na tumechanganyikana sana.Hatuwezi kuishi kwa staili unayoitaka.Kuna waislamu wamepanga nyumba za wakristo au wapagani na kinyumecho.Wakimbilie wapi kwa sera yako hiyo?
Jiheshimu uheshimiwe.
 

Uchokozi tu,
Huna lolote.
 
Ipite Comprehensive research itakayotueleza kwanini Kidato cha 5&6 ni kupoteza muda kwanini Sekondari isiwe miaka 5 then unakwenda polytechnic au university mojakwamoja.
 
Awaamuru necta wawalipe walimu posho zao za kusimamia mitihani ya taifa kidato cha iv 2015 punde tu shule zitakapofunguliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…