Tumsaidie kupata ndugu wa baba yake

Kilangi masanja

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
4,371
4,847
Habari zenu wapendwa katika bwana.
Ninajitokeza kwenu kuomba msaada kwa jambo hili.

Ninarafiki yangu aitwaye Makubi Madukwa Nyumbi,yeye ni mzaliwa wa wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi.Marehemu Baba yake Mzazi alikua akiitwa Mzee Peter Madukwa Nyumbi ambaye alikua ni mwajiriwa wa jeshi la wananchi wa Tanzania ( TPDF),alifariki mwaka 1993 huko huko wilayani Nachingwea na kuzikwa huko .

Marehemu hakuwahi kuwapatia taarifa za ni wapi hasa chimbuko la ukoo wake ulipo au ni akina nani hasa ndio ndugu wa damu upande wa ubabani kwa rafiki yangu kama vile mashangazi, babamkubwa ,babu, bibi na wengineo.

Kwa sasa rafiki yangu ametimiza miaka 26 hivyo marehemu alimuacha akiwa mdogo sana na mama wa rafiki yangu ni Mwera mtu wa Lindi.Sasa basi rafiki yangu amekua na shauku kubwa la kutaka kuwajua ndugu zake upande wa marehemu baba yake Mzee Peter Madukwa Nyumbi ila anakosa pa kuanzia.

Kwa yeyote yule ambaye anaweza kuwa na taarifa kuhusu ukoo tajwa hapo juu tunaomba awasiliane nasi kupitia namba 0783848802 au email masanjatinyali@gmail.com.

Kwa kuongezea ni kwamba marehemu alikuwa akifanyia kazi jijini Dar es Salaam kabla ya nduguze kumsihi aache kazi arudi usukumani ndipo alipoamua kuomba uhamisho na kuelekea Nachingwea mkoani Lindi .
 
Habari zenu wapendwa katika bwana.
Ninajitokeza kwenu kuomba msaada kwa jambo hili.Ninarafiki yangu aitwaye Makubi Madukwa Nyumbi,yeye ni mzaliwa wa wilaya ya nachingwea mkoani Lindi.Marehemu Baba yake Mzazi alikua akiitwa Mzee Peter Madukwa Nyumbi ambaye alikua ni mwajiriwa wa jeshi la wanawanchi wa Tanzania ( TPDF),alifariki mwaka 1993 huko huko wilayani nachingwea na kuzikwa huko .Marehemu hakuwahi kuwapatia taarifa za ni wapi hasa chimbuko la ukoo wake ulipo au ni akina nani hasa ndio ndugu wa damu upande wa ubabani kwa rafiki yangu kama vile mashangazi babamkubwa ,babu bibi na wengineo .Kwa sasa rafiki yangu ametimiza miaka 26 hivyo marehemu alimuacha akiwa mdogo sana na mama wa rafiki yangu ni Mwera mtu wa Lindi.Sasa bhasi rafiki yangu amekua na shauku kubwa la kutaka kuwajua ndugu zake upande wa marehemu baba yakeMzee Peter Madukwa Nyumbi ila anakosa pa kuanzia ,kwa yeyote yule ambaye anaweza kua na taarifa dhidi ya ukoo tajwa hapo juu tunaomba awasiliane nasi kupitia namba 0783848802 au email masanjatinyali@gmail.com.
Kwa kuongezea ni kwamba marehemu alikuwa akifanyia kazi jijini Dar es Salaam kabla ya nduguze kumsihi aache kazi arudi usukumani ndipo alipoamua kuomba uhamisho na kuelekea Nachingwea mkoani Lindi .
WASUKUMA WENZANGU TUSAIDIANE KATIKA HILI

Kutaja jina si kitu.angalau angesema eneo pia,mkoa na wilaya tungeanzia hapo.huku kwetu tuna mikoa mitano yote tunaikalia waSukuma,tupo wengi sana na koo zetu ni nyingi,ila angepata japo uelekeo wa atokako baba yake tutajaribu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom