Matukuta Jr
JF-Expert Member
- Apr 29, 2013
- 207
- 27
Hii HADUBINI YA TBC inakuwa na taarifa za kutoa machozi kila wakati kwa habari ambazo wanazirusha.
Jana kwenye Taarifa ya habari kwenye sehemu ya Hadubini kulikuwa na habari ya mtoto Ester Musa aliyeanguka kwenye mti wa muembe 16 September 2016 na kufikia kichwa.(Mimi nimeiona taarifa hii mchana wa leo kwenye Dira ya Mchana)
Alipoteza fahamu kwa siku 7 na baada ya hapo akafanyiwa operesheni ya kichwa kwa kuuweka ubongo sawa na kisha kuuondoa mfupa wa kichwani na kuuhifadhi tumboni kwa kusubiria operesheni nyingine baada ya kidonda cha kichwani kipone.
Operesheni hiyi inategemea kufanywa 17 January 2017, mtoto Ester nadai wakati mwingine anasikia maumivu makali ya kichwa na hata akilala kuna wakati ule mfupa uliohifadhiwa tumboni una mchoma.
Ester anaishi na Mama yake Mkubwa lakini cha kushangaza wazazi wake waligoma kuzipokea hizo taarifa na kusema wao wanamtaka mtoto wao akiwa mzima.
Toka siku aliyopata ajali ya kuanguka mtini si Baba au Mama yake Ester aliyetoka Singida kuja kumuona mwanao au hata kutuma hela ya matibabu.
Ester anasoma shule ya msingi na anatamani kuendelea na masomo yake, amesema anatamani sana kuwa Mwalimu hapo baadae.
Matibabu ya Ester katika Operesheni hiyo yanagharimu kiasi cha SHILINGI LAKI NANE(800,000) hivyo anaomba msaada wetu sisi Watanzania na mtu mwingine yoyote yule.
TBC wametoa akaunti ya kumchangia
Taarifa hii binafsi imegusa sana hisia zangu, imenitoa na machozi kwa namna mtoto Ester alivyokuwa anaongea.
Hakika HUJAFA HUJAUMBIKA!