Tumpongeze Maige kabla ya kumsulubu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumpongeze Maige kabla ya kumsulubu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mpayukaji, Apr 27, 2012.

 1. mpayukaji

  mpayukaji JF-Expert Member

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  [​IMG]


  • [​IMG][​IMG][​IMG][​IMG]

  Taarifa ya kufumka siri za utajiri wa kutisha wa waziri kijana wa Maliasili na Utalii Ezekiel Maige zinapaswa kutufanya tumpende na ikiwezekana tumsaidie kumfikisha mbele ya vyombo husika ingawa vyombo vyenyewe vinatia shaka.
  Kwanza, Tanzania ina akina Maige wengi kiasi cha kushindwa hata kujua idadi yao. Tuwape mfano, hao vijana wengi mnaowaona Mipakani, Viwanja vya ndege, Uhamiaji, Benki kuu, Bandari, mita za mafuta na kwingineko ni akina Maige sema hawajafichuliwa.
  Pili akina Maige wana wazazi wao waliowatengeneza. Hawako peke yao hawa. Wanaweza kufanya kila watakalo kuuza wanyama, unga, madini hata watanzania na hakuna anayewagusa. Hii ndiyo siri ya kila kitu nchini kujiendea bila yeyote kujali hasa uhujumu na ufisadi.
  Kama vijana kama Maige wana ukwasi kiasi hicho, hao baba zao wana ukwasi kiasi gani? Hapa hatujaongelea wale wageni wetu akina Chavda ambao Idd Simba aliwahi kusema kumi tu wanamilki uchumi wa Tanzania. Kimsingi hao ndiyo wenye fweza maana akina Maige ni vijikuadi na limbukeni vinavyohongwa kupitisha mizigo na mambo ya wakubwa wenyewe. Tumpongeze Maige kabla ya kumsulubu.
   
 2. KOMBESANA

  KOMBESANA JF-Expert Member

  #2
  Apr 27, 2012
  Joined: Jun 18, 2009
  Messages: 862
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  haya pongezi kwa Mheshimiwa Maige kwa kutuelezea habari za malori anayomiliki na nyumba na mikopo ya dola za kimarekani huu ni mfano wa kuigwakw awote wanaoabudu ufuska na ufisadi
   
Loading...