Tumpongeze Jakaya Kikwete wenyewe

Tumpongeze Jakaya Kikwete wenyewe

mwanzako dr slaa anaugulia laana ya jk shauri yako,
kumbuka dr alivyomzushia mengi jk 2010-2012, kusumbua uongozi wake kwa maandamano yasiyokuwa na kichwa wala miguu,mara nchi haitatawalika etc; leo hii yuko wapi na jk yuko wapi! Mungu hamtupi mja wake hata siku moja, so take care ndugu, jk ameitoa mbali nchi hii, amejaribu kuleta balance between ethnic groups, hassan leo hii anasoma kama vile john


Walioifikisha nchi hii hapa ni mafisadi na majizi na nitayashughulikia-magufuli
 
Alikuwa habagui dhehebu, alikuwa anaingia makanisani akiitwa kama vile anavyoingia misikitini, hata maaskofu walifikia kumuita ni chaguo la mungu, hawa maaskofu sio wajinga wala mataahira hata kidogo, very soon Jakaya will be an international agenda. All those who are responsible, kindly start the logistics on how to officially send-off our beloved present to his retirement end.
 
Wahandisi, wanasheria wetu, mwanasheria mkuu, usalama wa taifa, gavana, takukuru na wataalam wa umeme walikuwa wapi wasimshauri rais kuhusu richmond? Nakwambia tatizo letu ni kubwa sana kuliko kumtaja waziri na rais. Hawa wote waliwapotosha Waziri Mkuu na Rais wake kuhusu EPA, richmond, Escrow, n.k. Tangu lini rais na waziri mkuu wakatafuta mashine za kufua umeme bila kushauriwa?

Mbona unaandika maelezo mengi hivo..
Nauliza nani aliyeruhusu mkataba wa Richmond kuendelea?
 
He is Darling of the west!!!!! and under performer in his own country(Wazungu hawampendi mtu anayewabana)
your assumptions and perception may be right or wrong, you have no evidence based argument.
 
Hata kama kuna wizi kwenye miradi hiyo watakuwa watanzania wenzetu waliopiga hela hiyo. Sasa Jakaya angepata wapi watendaji waadilifu? Angeleta waholanzi, wachina, wafaranza kukusanya kodi na kusimamia ujenzi wa barabara tungepiga kelele hadi tuanguke kifafa. JK kaunda TAKUKURU, kaongeza majaji, kaongeza polisi lakini wote hawafanyi kazi. Sasa yeye angefwanyeje? awe dikteta kama Kagame?

Unataka kusema hata kusamehe wezi wa EPA tatizo ni ubinadam wake,katiba ya nchi,katiba ya chama au watu walimzunguka????JE TAKoKURU INAHUSIKA HAPO?
 
Hakika jk atabaki katika mioyo ya watanzania, kwa uvumilivu wake, kwa upendo wake kwa watu, kwa maendeleo yaliyopatikana, kwa huruma, utu na umakini wake katika uongozi. Mwaka 2010 hadi 2012 ilikuwa ni miaka ya majaribu makubwa sana kwake. Lakini kwa mkono wake mungu akayashinda. J

k ni one of the very popular african leaders internationally, na will remain even popular kwa watanzania wa hali ya chini ambao miaka kadhaa haikuwa rahisi kwao kusomesha lakini leo wanasomesha. Juzi morogoro ameshangiliwa kweli kweli kuliko hata magufuri jamhuri, pia mtwara.Mikoa ya magharib hasa tabora ambao kimsingi ulikuwa kama kisiwa umefunguliwa kwa barabara tano za kuunganisha mikoa mingine. Mungu akuzidishie raisi wetu, we lov u so much

Tuonyeshe uungwana kwa kumuandalia sherehe sisi watanzania wenyewe, tumpe zawadi zinazotoka mioyoni mwetu. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, ametupenda na sisi tumpende pia. Watu walidhani alikuwa anasafiri kwenda kustarehe huko nje, hapana, kwa watu wanaojuwa kusafiri kwa ndege wanafahamu namna kunavyochosha na kuhatarisha maisha, yeye alikuwa anajaribu kila namna kutafutia watu wake ahueni.

Mimi simjui wala hanijui wala hata kushikana naye mkono, lakini alinifanya niishi Marekani vizuri kwasababu ya sifa zake nzuri, huku wenzangu niliokuwanao kutoka Zimbabwe, Kenya, Uganda, Zambia na Msumbiji wakipata wakati mgumu kueleweka kule.

Hakika Jakaya hajatuangusha watanzania, na aendelee hivi hivi katika kusimamia uchaguzi mkuu kwa amani na bila upendeleo wowote, maana taifa letu ni zaidi ya CCM na UKAWA, Magufuli na Lowassa.

Alikuwa anaiona tanzania kwanza kabla ya kuziona tofauti zetu za vyama na dini na makabila. Dialogue was his greatest tool, he was able to accomodate wapinzani several times kule Ikulu akitafuta suluhu nao, nani anaweza hilo?
 
Tuonyeshe uungwana kwa kumuandalia sherehe sisi watanzania wenyewe, tumpe zawadi zinazotoka mioyoni mwetu. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, ametupenda na sisi tumpende pia. Watu walidhani alikuwa anasafiri kwenda kustarehe huko nje, hapana, kwa watu wanaojuwa kusafiri kwa ndege wanafahamu namna kunavyochosha na kuhatarisha maisha, yeye alikuwa anajaribu kila namna kutafutia watu wake ahueni. Mimi simjui wala hanijui wala hata kushikana naye mkono, lakini alinifanya niishi Marekani vizuri kwasababu ya sifa zake nzuri, huku wenzangu niliokuwanao kutoka Zimbabwe, Kenya, Uganda, Zambia na Msumbiji wakipata wakati mgumu kueleweka kule. Hakika Jakaya hajatuangusha watanzania, na aendelee hivi hivi katika kusimamia uchaguzi mkuu kwa amani na bila upendeleo wowote, maana taifa letu ni zaidi ya CCM na UKAWA, Magufuli na Lowassa.

Mimi bado nakupinga kwamba JK alikwenda ughaibuni kwa ajili ya kuhangaikia unafuu wa maisha ya watanzania......
 
Je kuhusu rushwa??
Je kuhusu deni la taifa
Je kuhusu maliasili zetu
Hii ni udhibitisho tosha kama yeye ni wakupongezwa km unavyosema.In fact,kama wengine watampongeza basi ni dhahiri hawajui the other side of the coin
 
mdau mbona unapotajiwa madhira ya utawala wa JK unamkwepesha na kuwapa lawama wateule wake,labda nikusaidie tu rais ni TAASISI sio JK,kama kuna PM bogus basi taasisi iliyomteua,kama kuna mawaziri mizigo taasisi ya urais inahusika,usimrembe saaana huyo JK na kumtenganisha na taasisi ya urais,hizo sifa unazompa nzuri ni kwa sababu ya taasisi ya urais na hata mbaya anapewa coz of taasisi,umemtetea kwa fact ya ubinadam,nasema JK anahukumiwa au analaumiwa kwa muktadha wa taasisi ambayo ni urais na si kama yeye BABA RIZIWAHIDA
Umesema vema, kwa-ajili ya matakwa ya checks and balance rais hawezi kufanya yote peke yake, ndani yake kuna waziri mkuu, katibu mkuu kiongozi, makamu wake, mawaziri wasaidizi, makatibu, usalama, wataalamu wa kila sekta, n.k.

Pia liko bunge na Mahakama, hivi vyoooote vikifanyakazi kwa ajili ya wananchi na kwa mujibu wa sheria sifa zooote zitamwendea rais wa nchi, kwa bahati mbaya watu na taasisi zote hizi zinategemeana. Rais amefanya kazi yake vema, shida ilikuwa bunge, mahakama, polisi, chama chake, mawaziri, makamu, katibu mkuu kiongozi, usalama, majaji, takukuru, wasomi wetu na wananchi wenyewe.

Kama wananchi hawataki kulipa kodi halisi kwa kugomea mashine za EFDs rais angefanya nini hapo?, kama washauri wa rais wanamdanganya na kumpotosha rais yeye angejuaje? Mfano, kama wasaidizi wake na wataalamu wake wa IT wanapomdanganya rais mchanamchana kuwa zile picha za mikutano ya ukawa ni feki na za kuungaunga yeye unategemea aseme nini hapo hali yeye hakuwepo kwenye mikutano na wala sio mtaalamu wa computer?

Ninachosema mimi ni kuwa Kikwete dhamira yake kwa taifa na watu wake ilikuwa safi sana, kama kuna mtu hakufanya kazi yake ipasavyo tumsake na kumkamata hata kama akiwa mtoto wa rais. tuwahoji wasaidizi wa rais wote, usalama, takukuru, wakuu wa wilaya na mikoa, wahandizi, makatibu wakuu, majaji, wafanyakazi, polisi, DPP, wabunge, n.k kwanini ama walimpotosha rais, hawakutimiza wajibu wao au wametuibia kwa kutumia nyazifa zao? maana rais alikuwa akiwategemea wao kwa namna moja au nyinginge kwa ushauri na kiutendaji. Majibu yao watakayotupa ndiyo yatakayotuambia kama rais alihusika au la?
 
Of course, japo jamaa kapiga, anastahili some credits.
 
your assumptions and perception may be right or wrong, you have no evidence based argument.

Mkuu read papers and do little research don't come here with an empty brain,everybody knows that he is Darling of the west!!!!!! and that is True
 
Hakika jk atabaki katika mioyo ya watanzania, kwa uvumilivu wake, kwa upendo wake kwa watu, kwa maendeleo yaliyopatikana, kwa huruma, utu na umakini wake katika uongozi. Mwaka 2010 hadi 2012 ilikuwa ni miaka ya majaribu makubwa sana kwake. Lakini kwa mkono wake mungu akayashinda. Jk ni one of the very popular african leaders internationally, na will remain even popular kwa watanzania wa hali ya chini ambao miaka kadhaa haikuwa rahisi kwao kusomesha lakini leo wanasomesha. Juzi morogoro ameshangiliwa kweli kweli kuliko hata magufuri jamhuri, pia mtwara.
Mikoa ya magharib hasa tabora ambao kimsingi ulikuwa kama kisiwa umefunguliwa kwa barabara tano za kuunganisha mikoa mingine.
Mungu akuzidishie raisi wetu, we lov u so much

Watanzania wa hali ya chini watamkumbuka sana jk kwa kuwaongezea umasikini. kuwauzia gesi Wachina
 
Kama kafanya makubwa hivyo, inakuwaje sasa hivi watu wanaona kwamba CCM haitakiwi kabisa? Wako tayari kumkumbatia papa kuliko kuendelea na CCM. I am sorry, rekodi yake ni mbaya kutosha.
 
tutamkumbuka kama kiongozi aliyetumia masaa mengi angani kuliko marubani wengi hapa nchini!
 
Umefugwa na jamaa wa Msola au ni poyoyo.I can't understand how a sensible person can ever think of thanking baba Amina.For what.Kuirudisha Tanzania kwenye ujima?!Wazee kutolipwa mafao yao?Umene usio wa uhakika?!Huduma za afya zisizo ridhisha?!An inflation of 80%?!Kuharibu elimu?!Kufumbia macho ufisadi?!Kutowajibisha viongozi wazembe?!Kuharibu mfumo wa kilimo?!

Kuchangia watoto wetu kuwa mapoyoyo?!Kuua usafiri wa reli na hivyo kupandisha bei ya bidhaa?!Kufukarisha watanzania?!Kwa lipi hasa,bwana kaa kimya usitukane Watanzania.Nina hasira sana,ngoja ninyamaze,nisije nikaongea maneno mabaya moderator akanifungia.

Wahandisi, wanasheria wetu, mwanasheria mkuu, usalama wa taifa, gavana, takukuru na wataalam wa umeme walikuwa wapi wasimshauri rais kuhusu richmond? Nakwambia tatizo letu ni kubwa sana kuliko kumtaja waziri na rais. Hawa wote waliwapotosha Waziri Mkuu na Rais wake kuhusu EPA, richmond, Escrow, n.k. Tangu lini rais na waziri mkuu wakatafuta mashine za kufua umeme bila kushauriwa?
 
Hiyo ni kazi ya polisi, takukuru, DPP, mahakama na wananchi. Wewe ulitaka rais ndo awakamate wahalifu? Tuwalaumu polisi, takukuru, DPP, majaji na sisi wananchi wenyewe kwa kunyamazia uhalifu.

Acha kuzunguka zunguka wote hawa uliowataja wana msimamizi mmoja tu mwenye mkataba na wapiga kura naye ni Raisi wa Jamhuri.kama rais asipoonesha kwamba hana mzaha/huruma na ubadhirifu na wizi wa mali za umma hata angepata malaika kama watendaji wake bado wangevurunda tu
 
Umefugwa na jamaa wa Msola au ni poyoyo.I can't understand how a sensible person can ever think of thanking baba Amina.For what.Kuirudisha Tanzania kwenye ujima?!Wazee kutolipwa mafao yao?Umene usio wa uhakika?!Huduma za afya zisizo ridhisha?!An inflation of 80%?!Kuharibu elimu?!Kufumbia macho ufisadi?!Kutowajibisha viongozi wazembe?!Kuharibu mfumo wa kilimo?!

Kuchangia watoto wetu kuwa mapoyoyo?!Kuua usafiri wa reli na hivyo kupandisha bei ya bidhaa?!Kufukarisha watanzania?!Kwa lipi hasa,bwana kaa kimya usitukane Watanzania.Nina hasira sana,ngoja ninyamaze,nisije nikaongea maneno mabaya moderator akanifungia.
Kwa maana hiyo kipaumbele chake ungetaka kiwe kujenga mahabusu na magereza mengi ili afunge woote walioharibu elimu, kilimo, afya, reli, n.k. asivae suti ila avae kombati awakimbize wahalifu wote nchini, atembee na kiboko mahakamani achape majaji wanaoendesha kesi polepole. Huo ni upoyoyo katika kufikiri
 
Back
Top Bottom