Tumpongeze Jakaya Kikwete wenyewe

Tumpongeze Jakaya Kikwete wenyewe

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
17,848
Reaction score
17,268
Watanzania tusisubiri watu wengine watuambie uzuri wa Rais wetu Jakaya Kikwete. Kafanya mengi makubwa kwa taifa hili, kubwa nililoliona mimi ni watanzania kuendelea kubaki wamoja pamoja na kuongezeka kwa kiwango cha demokrasia nchini na uthubutu wake wa kutaka Tanzania kuwa na Katiba Mpya.

Jakaya alikuwa akihaha huku na kule duniani katika kututafutia watanzania nafuu ya maisha, alikerwa sana na hali ya umaskini wetu. Katika uongozi wake amejaribu kuwatumia watu wa makundi yote katika nafasi mbalimbali za kuiongoza nchi, kama vile wazee, vijana, wanawake, wasichana, wavulana, wasanii, waandishi wa habari na wasomi wa dini na makabila mbalimbali.

Kama sisi watanzania hatutauona mchango wake, basi tusubiri kusoma vitabu vilivyoandikwa na watu wengine kuhusu ubora wa rais wetu Kikwete siku zijazo. Dunia inamtunuku heshima sisi tunamtukana, dunia inamremba sisi tunamrembulia.

Mapungufu ya Kikwete katika utawala wake (kama yapo) yanaweza kuwa yamechangiwa tu na mambo yafuatayo:

1. Ubinadamu wake, hakuna mkamilifu (perfect) duniani

2. Chama chake: Amerithi chama chenye katiba, taratibu na kanuni ambazo yeye hawezi kuzibadilisha over-night ili kuendana na mahitaji ya sasa. Chama kinamuagiza, yeye anatekeleza

3. Watu waliomzunguuka: Amekulia na kulelewa ndani ya chama, chama kinatayarisha ilani, hivyo hakuwa na namna ya kuwaengua watangulizi wake wooote ndani ya chama hata kama anaona wanamkwamisha.

4. Watanzania tulioko: Ni lazima angetutumia watanzania tulioko katika uteuzi wa nafasi mbalimbali hata kama ni wavivu, wabadhilifu, mafisadi, magoigoi, na hatujitumi. Kanuni hazimruhusu kuazima watendaji kutoka nchi nyingine, zingemruhusu kama ilivyo kwa makocha wa timu za mpira labda angewaleta kutoka China, Uholanzi, Australia, Israel na kwingineko kuja kuwa wakuu wa wilaya na wakurugenzi wake.

5. Katiba yetu ya nchi: Inawezekana mapungufu tunayoyaona kwake yametokana na katiba tuliyonayo ambayo ilimruhusu kufanya vile alivyofanya.

6. Kurithi shida za watangulizi: Kama ukikuta nyumba za watumishi zimeuzwa na mtangulizi wako utafanya nini? itakubidi uanze kujenga nyingine badala ya kulalamika. Ukiwakuta wananchi ni maskini sana utawafanya nini ndani ya miaka 10 tu?

8. Ukubwa wa nchi yetu: Hata hivyo nchi yetu ni kubwa mno kijografia, kuihudumia kwa kiusalama, usafiri, na kiuongozi ni kazi kubwa kuliko nchi ndogo kama rwanda, burundi, malawi, djibuti, n.k.

Pamoja na haya amefurukuta vya kutosha na lazima kama taifa tumpongeze na tumpe moyo mtanzania mwenzetu kwa hili na tumsamehe kwa alichokibakisha kukikamilisha.

Hata hivyo, Heshima yake itaongezeka saaaaana nchini na duniani kote kama atausimamia uchaguzi mkuu kwa njia za wazi, haki, salama na bila mizengwe wala upendeleo, na kumkabidhi bila hiyana mshindi wa uchaguzi bila vurugu, vitisho wala vishawishi kutoka kwa wapambe wake anaowaacha nyuma.

Akifanya hivyo taifa litamzawadia JK heshima ya kuwa baba mdogo wa Taifa baada ya kaka yake JK Nyerere kuwa baba wa taifa. Atakwenda kupunzika kwa heshima bila bughuza kule Msoga.

Bila kujali itikadi za vyama na dini, watu wataenda Msoga kumuomba ushauri na tutakuwa na baba wa taifa mpya tutakayemtegemea kwa ushauri, sasa hivi hatunae tena mtu kama huyo nchini baada ya Nyerere kututoka. Wazee waliobaki sasa hivi hawalioni taifa na watu wake bali matumbo yao na familia zao kwa kupanda kwenye mgongo wa CCM hata kama hawaipendi ama kuiona inakosea.

Badala ya JK kuzunguuka na kuwaaga watanzania sisi watanzania tumuite na kumuaga rais wetu mpenda watu, tumhakikishie amani na utulivu na kuendeleza ujenzi wa barabara, shule, viwanja vya ndege, reli, vivuko,, n.k alivyovianza ili kutimiza ndoto zake.
 
Alihaha huku na kule kutafuta wawekezaji au washirika wa biashara zake na kuhakikisha anauza maeneo mengi ya nchi na Kuwa na maeneo makubwa ya mashamba yake na riz 2
Hapo tutamkumbuka sana au hutaki???
 
Kukua kwa demokrasia nchini, mtandao mpana wa barabara, ujenzi wa daraja la kigamboni, kujengwa daraja la malagalasi, kujenga barabara ya mabasi yaendayo haraka dar es salaam, kuboresha bandari, kujenga shule za msingi kila kijiji na sekondari kila kata, kujenga zahanati kila kijiji, kuanzisha mchakato wa kuandika katiba mpya nchini, kuchimba gesi, n.k kunaonesha utashi wa JK mdogo kutaka kufuata nyayo za JK mkubwa.

Ila alikumbana na matatizo mengi yaliyotokana na siasa za watangulizi wake akina Nyerere, Mwinyi na Mkapa za umaskini, ujinga na maradhi. Alikuta kilimo, reli, barabara, ndege, viwanda, elimu, na afya vyote vimekufa. Hata maisha ya wanajeshi wetu na polisi yalikuwa chini sana, walimu wanadai, n.k angefanya nini kwa miaka 10 yake? hebu tumpongezeni huyu mtu.

Mimi ni miongoni mwa watu ambao sijawahi kumsifu JK hata siku moja, lakini nilitafakari nikaona kuwa huyu mtu kuna kitu kikubwa kalifanyia taifa ambacho sisi hatukioni, lakini wenzetu wa nje wanakiona. Tukutane taifa tumpongeze kwa ahadi kuwa anamalizia kazi yake kwa kutuachia kiongozi aliyechaguliwa kwa haki na sio mizengwe.

Kwenye uchaguzi huu yeye awe kama baba mdogo wa taifa, sio matusi kama ya Mkapa, awaache wagombea na wapambe wao watifuane majukwaani, yeye abaki kuwa kimbilio la wote, awe hazina ya wote, awe source of wisdom, awe chaguo la wapenda haki na ukweli. Wazungu sio wehu kumtunuku JK PhD za heshima, kwanini hawakumtunuku mzee Mwinyi na Mkapa, Salmin na Shein?
 
Kukua kwa demokrasia nchini, mtandao mpana wa barabara, ujenzi wa daraja la kigamboni, kujengwa daraja la malagalasi, kujenga barabara ya mabasi yaendayo haraka dar es salaam, kuboresha bandari, kujenga shule za msingi kila kijiji na sekondari kila kata, kujenga zahanati kila kijiji, kuanzisha mchakato wa kuandika katiba mpya nchini, kuchimba gesi, n.k kunaonesha utashi wa JK mdogo kutaka kufuata nyayo za JK mkubwa. Ila alikumbana na matatizo mengi yaliyotokana na siasa za watangulizi wake akina Nyerere, Mwinyi na Mkapa za umaskini, ujinga na maradhi. Alikuta kilimo, reli, barabara, ndege, viwanda, elimu, na afya vyote vimekufa. Hata maisha ya wanajeshi wetu na polisi yalikuwa chini sana, walimu wanadai, n.k angefanya nini kwa miaka 10 yake? hebu tumpongezeni huyu mtu. Mimi ni miongoni mwa watu ambao sijawahi kumsifu JK hata siku moja, lakini nilitafakari nikaona kuwa huyu mtu kuna kitu kikubwa kalifanyia taifa ambacho sisi hatukioni, lakini wenzetu wa nje wanakiona. Tukutane taifa tumpongeze kwa ahadi kuwa anamalizia kazi yake kwa kutuachia kiongozi aliyechaguliwa kwa haki na sio mizengwe. Kwenye uchaguzi huu yeye awe kama baba mdogo wa taifa, sio matusi kama ya Mkapa, awaache wagombea na wapambe wake watifuane majukwaani, yeye abaki kuwa kimbilio la wote.

Hivi deni la taifa limefika shilingi ngapi vile? na gharama ya hiyo miradi uliyotaja ni shilingi ngapi tena? mimi sijabobea katika hisabati naomba unisaidie
 
Hivi deni la taifa limefika shilingi ngapi vile? na gharama ya hiyo miradi uliyotaja ni shilingi ngapi tena? mimi sijabobea katika hisabati naomba unisaidie
Hata kama kuna wizi kwenye miradi hiyo watakuwa watanzania wenzetu waliopiga hela hiyo. Sasa Jakaya angepata wapi watendaji waadilifu? Angeleta waholanzi, wachina, wafaranza kukusanya kodi na kusimamia ujenzi wa barabara tungepiga kelele hadi tuanguke kifafa. JK kaunda TAKUKURU, kaongeza majaji, kaongeza polisi lakini wote hawafanyi kazi. Sasa yeye angefwanyeje? awe dikteta kama Kagame?
 
Nimekielewa. Lakini No. 1 hadi 6 ndizo zinatufanya tutake mabadiliko. No. Ubinadamu wa kudharau watendaji wachapakazi ukakubatia wazembe hatuutaki.

No. 2 hadi 6 sintufanya tuone kwamba hata akiingia Magufuli, hoja hizo ziko palepale, hivyo muarubaini ni kufuta mfumo huo na kuanza mpya kupitia UKAWA. Kumbe umeona kwanini watu wanataka mabadiliko eee!!! Mabadiliko ya hivyo hayawezi patikana CCM.
 
Kweli Kabisa Ndomana Juz Juz Hapa Kachukua Tuzo Ya Kiongozi Bora...Lakini Kosa Kubwa Ni Kumwacha Fisadi Wa Richmond Mpaka Sasa Hvi Bila Kumpeleka Selo,kikwete Hapo Umechoma Baba...Ulitakiwa Kuonyesha Mfano,escrow,epa Zisingetokea Bt Stl Ntabak Ccm #hapakazitu #umojaniushindi
 
Huyu aliyeamuru Richmond isainiwe???

Afu mbn Escrow hajafatilia ule mgao wa STANBIC BANK nao tujue kina nani waligawana wawajibishwe???
 
Hatuna muda mrefu tutautambua umuhimu wa Jakaya kikwete
 
Hata kama kuna wizi kwenye miradi hiyo watakuwa watanzania wenzetu waliopiga hela hiyo. Sasa Jakaya angepata wapi watendaji waadilifu? Angeleta waholanzi, wachina, wafaranza kukusanya kodi na kusimamia ujenzi wa barabara tungepiga kelele hadi tuanguke kifafa. JK kaunda TAKUKURU, kaongeza majaji, kaongeza polisi lakini wote hawafanyi kazi. Sasa yeye angefwanyeje? awe dikteta kama Kagame?

Ni watendaji wangapi wa JK wamefungwa gerezani hadi sasa kwa wizi wa pesa za miradi ya serekali hadi sasa?hata wale waliokamatwa ready handed wako mtaani wanapeta na uongozi wanagombea.nitajie watendaji waandamizi waliofungwa ama hata kupelekwa mahakamani kwa wizi wa fedha za miradi ya serikali zaidi ya sababu za kisiasa.JK hawezi kukwepa lawana jamani tuwe wakweli tu.maana wananchi walimuamini yeye na yeye akaajiri watendaji wake ambao hawana mikataba na wananchi kama JK alivyo na mkataba na wapiga kura wake
 
Hatuna muda mrefu tutautambua umuhimu wa Jakaya kikwete

Bora na wewe umeliona hilo. Hivi kati ya Lowassa na Magufuli nani anao uwezo wa kuwavumilia watanzania wanaoropoka ovyo kama anavyofanya Jakaya? Jakaya alitamani kuboresha kila kona kuanzia machinga, wakulima, wasanii, majeshi, ndege, barabara, bandari, utalii, nyumba na makazi, elimu, afya, n,k ameshindwa tu kutokana na ubovu wa wafuasi na watendaji na ukosefu wa fedha.

Ilifikia mahali akaachana na ilani ya chama ambayo haitekelezeki akaanza kuwaona watanzania na mahitaji yao halisi na akafanya yeye kama yeye. Ona alivyowatuma akina Kinana na Nape kuzunguuka nchi nzima kuwaponda mawaziri mizigo lakini wapi, watendaji walikuwa wanamuangusha Jakaya na akikuwa anawabadili kila siku ili kutafuta nafuu lakini wapi, aliwapeleka semina elekezi watendaji wote kule ngurdoto lakini wapi.

Ukweli ni kwamba Jakaya alikuwa na uchungu na nchi yake isonge mbele lakini katiba chama ya nchi na watendaji vilimkwaza. Kama katiba ingemruhusu kuwa dikteta wa kuchapa viboko huwenda angefanya hivyo kwa mawaziri wabovu, hasa baada ya kumpoteza chapakazi wake hodari ndugu Lowassa kama waziri mkuu wake na kumpata Pinda ambaye alikuwa mpole kupita kiasi. kama katiba ingemruhusu huwenda angeteua watu kutoka hata vyama vya upinzani kwenye serikali yake ili kuongeza ufanisi.
 
Naunga hoja mkono...kwa sababu ktk upungufu wetu ndipo unapoona ukamilifu wetu
 
Kukua kwa demokrasia nchini, mtandao mpana wa barabara, ujenzi wa daraja la kigamboni, kujengwa daraja la malagalasi, kujenga barabara ya mabasi yaendayo haraka dar es salaam, kuboresha bandari, kujenga shule za msingi kila kijiji na sekondari kila kata, kujenga zahanati kila kijiji, kuanzisha mchakato wa kuandika katiba mpya nchini, kuchimba gesi, n.k kunaonesha utashi wa JK mdogo kutaka kufuata nyayo za JK mkubwa. Ila alikumbana na matatizo mengi yaliyotokana na siasa za watangulizi wake akina Nyerere, Mwinyi na Mkapa za umaskini, ujinga na maradhi. Alikuta kilimo, reli, barabara, ndege, viwanda, elimu, na afya vyote vimekufa. Hata maisha ya wanajeshi wetu na polisi yalikuwa chini sana, walimu wanadai, n.k angefanya nini kwa miaka 10 yake? hebu tumpongezeni huyu mtu. Mimi ni miongoni mwa watu ambao sijawahi kumsifu JK hata siku moja, lakini nilitafakari nikaona kuwa huyu mtu kuna kitu kikubwa kalifanyia taifa ambacho sisi hatukioni, lakini wenzetu wa nje wanakiona. Tukutane taifa tumpongeze kwa ahadi kuwa anamalizia kazi yake kwa kutuachia kiongozi aliyechaguliwa kwa haki na sio mizengwe. Kwenye uchaguzi huu yeye awe kama baba mdogo wa taifa, sio matusi kama ya Mkapa, awaache wagombea na wapambe wao watifuane majukwaani, yeye abaki kuwa kimbilio la wote, awe hazina ya wote, awe source of wisdom, awe chaguo la wapenda haki na ukweli. Wazungu sio wehu kumtunuku JK PhD za heshima, kwanini hawakumtunuku mzee Mwinyi na Mkapa, Salmin na Shein?

Hivi Magufuli anaposema anataka awakomboe watanzania
anamaana gani kweli? Tumezama? na anaposema anataka kuleta Mabadiliko, kwani nini kimetokea kweli? embu nikumbushage!!
 
Ni watendaji wangapi wa JK wamefungwa gerezani hadi sasa kwa wizi wa pesa za miradi ya serekali hadi sasa?hata wale waliokamatwa ready handed wako mtaani wanapeta na uongozi wanagombea.nitajie watendaji waandamizi waliofungwa ama hata kupelekwa mahakamani kwa wizi wa fedha za miradi ya serikali zaidi ya sababu za kisiasa.JK hawezi kukwepa lawana jamani tuwe wakweli tu.maana wananchi walimuamini yeye na yeye akaajiri watendaji wake ambao hawana mikataba na wananchi kama JK alivyo na mkataba na wapiga kura wake
Hiyo ni kazi ya polisi, takukuru, DPP, mahakama na wananchi. Wewe ulitaka rais ndo awakamate wahalifu? Tuwalaumu polisi, takukuru, DPP, majaji na sisi wananchi wenyewe kwa kunyamazia uhalifu.
 
Kukua kwa demokrasia nchini, mtandao mpana wa barabara, ujenzi wa daraja la kigamboni, kujengwa daraja la malagalasi, kujenga barabara ya mabasi yaendayo haraka dar es salaam, kuboresha bandari, kujenga shule za msingi kila kijiji na sekondari kila kata, kujenga zahanati kila kijiji, kuanzisha mchakato wa kuandika katiba mpya nchini, kuchimba gesi, n.k kunaonesha utashi wa JK mdogo kutaka kufuata nyayo za JK mkubwa. Ila alikumbana na matatizo mengi yaliyotokana na siasa za watangulizi wake akina Nyerere, Mwinyi na Mkapa za umaskini, ujinga na maradhi. Alikuta kilimo, reli, barabara, ndege, viwanda, elimu, na afya vyote vimekufa. Hata maisha ya wanajeshi wetu na polisi yalikuwa chini sana, walimu wanadai, n.k angefanya nini kwa miaka 10 yake? hebu tumpongezeni huyu mtu. Mimi ni miongoni mwa watu ambao sijawahi kumsifu JK hata siku moja, lakini nilitafakari nikaona kuwa huyu mtu kuna kitu kikubwa kalifanyia taifa ambacho sisi hatukioni, lakini wenzetu wa nje wanakiona. Tukutane taifa tumpongeze kwa ahadi kuwa anamalizia kazi yake kwa kutuachia kiongozi aliyechaguliwa kwa haki na sio mizengwe. Kwenye uchaguzi huu yeye awe kama baba mdogo wa taifa, sio matusi kama ya Mkapa, awaache wagombea na wapambe wao watifuane majukwaani, yeye abaki kuwa kimbilio la wote, awe hazina ya wote, awe source of wisdom, awe chaguo la wapenda haki na ukweli. Wazungu sio wehu kumtunuku JK PhD za heshima, kwanini hawakumtunuku mzee Mwinyi na Mkapa, Salmin na Shein?

He is Darling of the west!!!!! and under performer in his own country(Wazungu hawampendi mtu anayewabana)
 
Hakika jk atabaki katika mioyo ya watanzania, kwa uvumilivu wake, kwa upendo wake kwa watu, kwa maendeleo yaliyopatikana, kwa huruma, utu na umakini wake katika uongozi. Mwaka 2010 hadi 2012 ilikuwa ni miaka ya majaribu makubwa sana kwake. Lakini kwa mkono wake mungu akayashinda. Jk ni one of the very popular african leaders internationally, na will remain even popular kwa watanzania wa hali ya chini ambao miaka kadhaa haikuwa rahisi kwao kusomesha lakini leo wanasomesha. Juzi morogoro ameshangiliwa kweli kweli kuliko hata magufuri jamhuri, pia mtwara.
Mikoa ya magharib hasa tabora ambao kimsingi ulikuwa kama kisiwa umefunguliwa kwa barabara tano za kuunganisha mikoa mingine.
Mungu akuzidishie raisi wetu, we lov u so much
 
nchi imeozaaaa

mwanzako dr slaa anaugulia laana ya jk shauri yako,
kumbuka dr alivyomzushia mengi jk 2010-2012, kusumbua uongozi wake kwa maandamano yasiyokuwa na kichwa wala miguu,mara nchi haitatawalika etc; leo hii yuko wapi na jk yuko wapi! Mungu hamtupi mja wake hata siku moja, so take care ndugu, jk ameitoa mbali nchi hii, amejaribu kuleta balance between ethnic groups, hassan leo hii anasoma kama vile john
 
Huyu aliyeamuru Richmond isainiwe???

Afu mbn Escrow hajafatilia ule mgao wa STANBIC BANK nao tujue kina nani waligawana wawajibishwe???
Wahandisi, wanasheria wetu, mwanasheria mkuu, usalama wa taifa, gavana, takukuru na wataalam wa umeme walikuwa wapi wasimshauri rais kuhusu richmond? Nakwambia tatizo letu ni kubwa sana kuliko kumtaja waziri na rais. Hawa wote waliwapotosha Waziri Mkuu na Rais wake kuhusu EPA, richmond, Escrow, n.k. Tangu lini rais na waziri mkuu wakatafuta mashine za kufua umeme bila kushauriwa?
 
Back
Top Bottom