Abby Newton
JF-Expert Member
- Nov 12, 2017
- 1,227
- 2,197
Mwaka 2018 Jamuhuri ya China walirekebisha Katiba yao na kumfanya Rais wao wa sasa Xi Jiping kuwa Rais wa maisha. Hawajafanya marekebisho haya kwa bahati mbaya bali ni kwa sababu Rais Jiping kaifanya China kupiga hatua kubwa kimaendeleo hali inayopelekea kukaribia kuipita Marekani na kuwa Taifa la kwanza kiuchumi Duniani.
Urusi nao watapiga kura siku chache zijazo kumuongezea muda Rais Putin ili aongoze hadi 2036. Urusi na China ni mataifa makubwa yaliyoendelea kila nyanja lakini wanafanya haya kwanini sisi tusifanye hasa baada ya kumpata Rais mwenye sifa tuliyoitaka kwa muda mrefu?
Wajerumani wenyewe Kansela wao bi Anjela Merkel ameongoza kwa miaka takribani 14. Tujiulize kwanini wao na sio sisi?
"Great people are not born every day". Baada ya kuondoka Nyerere sote tunajua ni jinsi gani nchi yetu iliparaganyika. Leo tuna Rais Jasiri, asiyependa Rushwa, ana hofu na Mungu, Mkali, anasimamia maadili ya watumishi, Ana maono, anapenda maendeleo,haogopi mabeberu, Mungu atupe nini Watanzania halafu eti tukubali kumuachia? Kwanini hatutaki kufundishwa na historia?
Wazungu kamwe hawatapenda kuona kiongozi kama Magufuli anaongoza kwa mda mrefu,kwani kawashika pabaya. Hawapi mda wa kupumua walizoea kutugeuza shamba la bibi. Nilazima tuwaonyeshe kwamba sio yeye anaetaka madaraka kwa nguvu bali ni sisi wananchi ndio tunamtaka atuongoze.
Magufuli ni lulu kama ilivyo kwa Xi Jiping, na Putin. Hawa ni viongozi wenye uzalendo wa hali ya juu na ni vigumu kuwapata wa namna hiyo kwa karne hii ya d.com.
Magufuli kafanya mengi mno kwa mda mfupi bado tunahitaji vingi kutoka kwake. Kumuacha aondoke ni sawa na kutema "Bublish" ikiwa bado na utamu.