Tumkumbuke Madilu multi system

Tumkumbuke Madilu multi system

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
5,139
Reaction score
1,149

Jean de Dieu Makiese a.k.a. Madiluu alizaliwa May 28, 1952 katika jiji la Léopoldville ambayo ndio Kinshasa ya leo na kufariki dunia siku kama ya leo yani August 11, 2007.Madilu alianza kuimba rasmi 1969 akipitia bendi mbalimbali mfano Orchestre Symba, Orchestre Bambula ya Papaa Noel bila kuisahau Festival des Maquisards ya mzee Sam Mangwana. Baadae Madilu alianzisha bendi yake mwenyewe ikiitwa Orchestre Bakuba Mayopi.Lakini kote huko hakuna aliemfahamu madilu duniani mpaka alipoungana na mzee Franco ambapo ndipo mzee Franco akambatiza jina hili la Madilu System lililokuja kuwa maarufu ulimwengu mzima akijulika hivyo badala ya jina lake la asili yani Jean de Dieu Makiese.Akiwa na mzee Franco na TP OK JAZZ nyimbo ambayo ilimtoa madilu ilikua ni "Mamou" ambayo ilikuja kuwa nyimbo bora kwa mwaka 1984.Lakini hiyo ilikua ni nyimbo ya bendi ambayo madilu alishiriki tu kuiimba na kuifanya sauti yake isikike na kutambulika ulimwenguni na watu kumjua,lakini madilu alikuja kuuthibitishia ulimwengu kwamba anao uwezo na kipaji cha kutunga na kuimba mwaka 1986 alipotunga yeye mwenyewe wimbo unaotamba mpaka leo kwa bendi mbalimbali kuupiga kama copy "Pesa Position" na baadae wimbo "Mario" na kuendelea na nyimbo kibao ukiwemo "La Vie des Hommes" ambao waliufanya kwa pamoja ( duets) yeye na mzee Franco mwenyewe.

Baada ya kifo cha mzee Franco TP OK JAZZ ilisimama kufanya shughuli za muziki kwa mwaka mzima,lakini baadae TP OK JAZZ Ikarudi upya chini ya Madilu ambae alijaribu kuileta TP OK JAZZ pamoja na kutoa mchango mkubwa kuhakikisha inasimama.Baadae Madilu akarejea kuendeleza solo career yake kama yeye huku akiweka makazi yake ulaya zaidi kwenye miji ya Paris na badae Geneva,Switzerland lakini huku nyumbani Kinshasa akiendelea kuwa na kiwango kikubwa cha mashabiki pia.

Mwanzoni mwa mwaka 2007 sikumbuki sawasawa mwezi gani Madilu alirejea Kinshansa mara moja kwa lengo la kufanya shooting kwa ajili ya video za nyimbo zake.Akiwa katika harakati za kukamilisha kilichomrejesha Kinshasa then arudi zake kwake Ulaya siku ya ijumaa ya August the 10th 2007 Madilu alianguka ghafla na kukimbizwa hospitali ya chuo kikuu cha Kinshasa ambapo asubuhi ya siku iliyofuata yani August 11th,2007,Madilu alifariki dunia.

Madilu alikua kipenzi cha watu wengi hasa tabaka la watawawala wa nchi za AFRIKA kiasi cha kupata mialiko mingi ya kutumbuiza kwenye hafla za marais mbalimbali wa nchi za Afrika ya kati na magharibi.Mfano ni hii hafla iliyofanyika ikulu ya GABON ambayo ili ni ANNIVERSAIRE ya Mokonzi wa bakonzi le prezidaa OMAR BONGO na mkewe Mamaa EDITHA SASSOU NGUESSO ambae alikua ni binti wa rais wa Congo Brazzaville DENNIS SASAAOU NGUESSO,walikua wakisherehekea miaka kadhaa tangu waoane ambapo mkitazama vizuri mzee DENNIS SASSOU NGUESSO nae mtamuone hapo kwenye big Party ndani ya ikulu ya Gabon,mamaa Editha mtamuona hapo kwenye dancing floor akiwa amevaa gauni refu la kijana huku akicheza muziki wa madilu na mumewe Omar Bongo.Rais OMAR BONGO na Mkewe huyo nao kwa sasa wote ni marehemu.

Mungu awalaze pema wote watatu,Madilu,mzee Omar Bongo na mamaa Editha.


 
Last edited by a moderator:
Madilu alikuwa ni noma baada ya kifo cha Franco wataalamu wa muziki wa Congo walisema yeye ndo alikuwa mrithi wake.
 
Madilu hakuna cha kuanguka wala nini. Ilikuwa ukimwi tu ndo uliomuua. Omar bongo na mkewe huo huo. Walikuwa womanisers saana hawa jamaa. Full stop
 
Mkuu Asante sana kwa uzi mzuri, nilitaka kuleta Historia yake humu ila nikaona ni vema nipekue kwanza kujirithisha kama kweli Hamna na kama zali nimekutana na huu wako, Asante Sana.

Hata hivyo nina swali, inasemekana kua Franco Lwambo Lwanzo Makyadi mpiga solo namba moja duniani alikua na uhusiano wa damu na Madiluu, kwamba eti Madiluu na Francoo walikua ni mtu na mjomba-ake, kuna ukweli kuhusu hili? KIM KARDASH
 
Mkuu @
Madilu hakuna cha kuanguka wala nini. Ilikuwa ukimwi tu ndo uliomuua. Omar bongo na mkewe huo huo. Walikuwa womanisers saana hawa jamaa. Full stop
lazamwa ni ukimwi kweli? Unajua hata Francoo alipokufa inasemekana ni huo huo ukimwi, yana ukweli haya?

Na mtu anaeumwa ukimwi anaweza kufa kifo cha ghafla bin vuuu?
 
Kuna siku nilimsikia Jose Mara anasema kua Madilu alikua na uwezo Mkubwa sana kiasi kwamba hata kama mkijipanga wasanii 100 kulia kwake na wengine 100 kushoto kwake kwa pamoja wakiimba atasikika yeye tu, Alikua na sauti ya hatari sana.
 
Akiwa na mzee Franco na TP OK JAZZ nyimbo ambayo ilimtoa madilu ilikua ni "Mamou" ambayo ilikuja kuwa nyimbo bora kwa mwaka 1984
Nyimbo iliyomtoa Madilu kwenye uimbaji ni "Non" 1983 Utunzi wa Franco wakiimba duet na Madilu. Hii ndiyo nyimbo ya kwanza toka kuingia OK Jazz 1980 alisikika na kuimba solo. Hizo nyingine zilifuata nyingi zikiwa utunzi wa Franco kama Mamou.
 
lakini baadae TP OK JAZZ Ikarudi upya chini ya Madilu
Kiongozi wa TP OK Jazz baada ya kufariki Franco alikuwa Le Poete Simaro Lutumba mpaka kuvunjika kwa bendi 1993 na baada ya hapo walianzisha Bana OK 1994 na Madilu ndio akaenda solo hadi umauti ulipomfika. Kwa utaratibu alijenga bendi yake "Multi-System" ambayoilikuja kufanya vizuri bahati mbaya ndio umauti ukamfika 2007.
 
Hata hivyo nina swali, inasemekana kua Franco Lwambo Lwanzo Makyadi mpiga solo namba moja duniani alikua na uhusiano wa damu na Madiluu, kwamba eti Madiluu na Francoo walikua ni mtu na mjomba-ake, kuna ukweli kuhusu hili?
Le Grand Maitre Franco hakuwa na undugu wowote na Madilu Sytem.
 
Madilu alikuwa ni noma baada ya kifo cha Franco wataalamu wa muziki wa Congo walisema yeye ndo alikuwa mrithi wake.
Sidhani kama kuna mtu anaweza kuwa mrithi wa Franco. Kuna ambao wameendeleza mziki wa Franco wakiwamo Madilu na Youlou (hawa wamesema hadharani na kuonyesha kimuziki kuwa ni watoto wa Franco kimuziki). Kuna bendi za Bana OK (Kinshasa), Bana OK International, na wengine. Kumbuka Franco alikuwa kiongozi, mpiga solo, muimbaji, talent hunter aliyeongoza bendi kubwa zilizowahi kutokea Congo. Hivyo viatu vyake ni vigumu kuvaliwa na mtu mwingine. Mtu ambaye alimkaribia Franco ndani na nje ya OK jazz ni kiongozi wa OK Jazz na Bana OK-Simaro Lutumba -familia ya Franco ilipo msimamisha huyu kuwa kiongozi wa OK Jazz wanamuziki karibu wote waliacha OK Jazz na wengi wakaanzisha Bana OK na baadae Bana OK International (Odemba International). Kwa wapenzi wa Madilu watakumbuka kitu kama Ofela, Dati petrol mtunzi wake alikuwa Mzee Lutumba (miaka 79 sasa na bado yuko active kiasi). Huwezi pia kumsahau Commander Josky Kiambukuta huyu ni sauti ya OK Jazz na mtunzi mahiri sana (1973-1993) nae bado anatoa moja moja.
 
Back
Top Bottom