Tumkatae Mizengo Pinda na watendaji wa aina yake

Tumkatae Mizengo Pinda na watendaji wa aina yake

Ng'wamapalala

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
6,811
Reaction score
6,506
Mwaka 2008 baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu nafasi yake. Mizengo Pinda aliyeshika nafasi yake alitarajiwa kuja na moto mkali zaidi wa kiutendaji. Kuna baadhi ya Watanzania walishangilia sana ujio wa Mizengo Pinda.

Itakumbukwa kuwa Lowassa aliyeangushwa na kashfa ya mradi tata wa umeme wa Richmond, alishaanza kuonyesha machachari yake hasa katika kusimamia suala la elimu ambapo alihamasisha ujenzi wa shule za sekondari za kata na miradi mingine.

Pinda aliingia akiwa amevaa ngozi ya kondoo, huku akijiita mtoto wa mkulima. Leo ni miaka zaidi ya saba imepita, tunamwona Pinda halisi alivyo. Kuna kila dalili kwamba amepwaya katika nafasi hiyo.

Tofauti na walivyokuwa mawaziri wakuu wengine, Pinda hajaonyesha ubunifu katika mambo mbali mbali na kuyasimamia. Badala yake amekuwa mtu wa kuonekana wakati wa matukio huku ukitaka uongozi wake tuupime katika mzani wa upole na umasikini. Uongozi wa Tanzania hauwezi kupimwa pekee katika mzani wa upole na umasikini. Hatuwezi kuwa na kiongozi anayejivunia umasikini katika Taifa lenye mazingira ya market economy. Umasikini si turufu ya uongozi, bali kiongozi mzuri ni yule anayekerwa na umasikini badala ya kuutukuza na kuuenzi, ndiyo maana kila siku watanzania wengi wanatafuta njia ya kupambana na umasikini.

Kukitokea vurugu, wananchi wa Mtwara wameandamana, Waziri Mkuu Pinda anakwenda kutuliza, madaktari wamegoma, anakwenda kuzungumza nao, wenye malori na mabasi wamegoma, anakwenda kuwabembeleza.

Nchi hii ilipofika, hatuhitaji kiongozi atakayeridhisha watu bali kiongozi atakayetoa dira ya Taifa inayojari Taifa ili tuvuke na kufika salama kule wananchi wanataka Taifa lifike. Mchekeshaji maarufu duniani, Bill Cosby, aliwahi kusema; ''I don't know the key to success, but the key to failure is trying to please everybody''. Kwa lugha ya mashuleni kijijini Bariadi, alimaanisha kuwa, hajui njia ya kuyafikia mafanikio, lakini njia ya kutofanikiwa ni kumridhisha kila mtu.

Huu ni udhaifu, haiwezekani kiongozi ashughulikie matukio tu wakati anaweza kuboresha utendaji ili mambo yasiharibike. Kutokana na udhaifu huo, hata mawaziri walio chini yake hawawajibiki ipasavyo na wale wachache wanaowajika, anajitokeza na kuwapiga stop. Ndiyo maana hivi karibuni, Wabunge walimtaja kuwa mmoja kati ya mawaziri wanaopaswa kuwajibika kutokana na kushindwa kusimamia kazi zao.

Nilipatwa na mshangao baada ya kukutana vichwa vya habari vinavyosema ''WAZIRI MKUU PINDA AMUONYA VIKALI MAGUFULI'', vingine vilisema, '' SERIKALI YAMZIMA MAGUFULI''.

Ndani yake kulikuwa na habari inayosema,
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amemuonya Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli kwa mara nyingine tena kuacha tabia ya kufanya uamuzi wa jambo lolote bila kushirikisha pande zinazohusika.
Mbali ya karipio hilo, Waziri Mkuu amewataka viongozi wengine wa Serikali, kuepuka mfumo usio shirikishi katika uamuzi wao kwa kuwa unasababisha migogoro ndani ya jamii na usumbufu kwa Serikali.

Kilichonifanya kuduwaa na kushangaa zaidi ni pale Pinda aliponukuliwa akisema,

''Hatua zilizochukuliwa na Dk. Magufuli kufuta vifungu vilivyokuwa vikiruhusu asilimia tano zilifuata sheria, lakini tatizo lililojitokeza ni kutoshirikisha pande zinazohusika ili kushauriana na kupata uamuzi wa pamoja. Mbali ya kutoshirikisha pande hizo, uamuzi wa Dk. Magufuli ulikuwa wa ghafla kwa wasafirishaji kitendo ambacho kimewapa wakati mgumu wa utekelezaji, kwa sababu wafanyabiashara walikuwa wameingia mikataba na wateja wao''
Yaani Magufuli anayezilinda barabara zetu kwa kutumia sheria zilizopo ili zisife mapema anampiga stop eti ashauriane kwanza na wale wanaotakiwa kufuata sheria. Sheria ikishatungwa na kupitishwa haiwezi tena kutaka mashauriano ili kuifuata. Huu siyo muswada wa sheria.

Mizengo Pinda amesomea sheria na lazima aelewe kuwa sheria inapotungwa na kupitishwa, hakuna tena majadiliano. Kwa macho ya Mizengo Pinda, kosa la Magufuli ni kuilinda hiyo sheria bila kuwashirikisha wanaoivunja. Jamani, unapomkamata mwizi unamshirikishaje? Unashauriana naye nini ili mpate uamuzi wa pamoja kama siyo kuanza kujenga mazingira ya rushwa?.

Huyu ndiyo eti anataka awe Rais ili aweze kupambana na ufisadi achilia mbali makampuni makubwa ya kimataifa ambayo mengine yana dictate foreign policy za mataifa ya Magharibi. This is fun to say the least.

Kikubwa zaidi, Mizengo Pinda alishatamka hana nia ya kuwa Rais wa Tanzania kama alivyonukuliwa na Januari 25, mwaka 2012 akisema,

"Niliposema sitawania urais nilimaanisha hivyo na naomba watu wanielewe, urais si kazi ya kukimbilia kama kweli unataka kuwatumikia watu, kwa wale wanaotaka kwenda kuchuma sawa ni pazuri, lakini mimi naona ni mzigo, kuna wakati namwonea huruma Rais Kikwete maana kila kitu kigumu anaangushiwa yeye,"
Unaweza kusoma interview yake kupitia hapa,

Ni nini tena kimemtuma/kimemkuta atake kuwa mgombea Urais?. Watanzania tusikubali kufanywa wajinga na wanasiasa aina ya Mizengo Pinda. Lazima tuwakatae kwa nguvu zote.

Wanasiasa wa aina ya Mizengo Pinda hawafai, hawatufai na hawalifai Taifa. Ni bora waende kuangalia na kuendeleza mashamba yao ya zabibu na kuchunga ng'ombe.

ANGLI4.jpg

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwaongoza viongozi wa Kanisa la Anglican kutembelea shamba la zabibu na malisho ya ng'ombe kwenye shamba lake lililopo Zuzu Dodoma Februari 9, 2015. Baadhi ya viongozi hao ambao walikwenda kujifunza kwa lengo la kuanzisha shamba linalofanana na hilo Dodoma ni Askofu Dickson Chilongani wa Dayosisi ya Dodoma (wapili kushoto), Askofu Maimbo Mndolwa wa Dayosisi ya Tanga (kulia kwake) na kulia ni Re. Canon, Johnson Chinyongole ambaye ni Katibu Mkuu wa Kanisa hilo
 
Uchambuzi mzuri sana wa Ng'wamapalala.

Pinda ni furushi zito ambalo haliwezi kubebeka na jamii yoyote inayotaka maendeleo. Huwezi kuongoza na kupata mafanikio kama una compromise na sheria. Kwa ujumla uongozi wa Kikwete kwa kiasi kikubwa umeshindwa kwa sababu ya kutosimamia sheria na tamaa ya kutaka kumridhisha kila mtu.

Hakuna kiongozi anayeweza kumrudhisha kila mtu, ukiona kiongozi anaridhisha kila mtu yaani wanaoibiwa waridhike, wanaoiba waridhike, utambue kiongozi huyo ni mnafiki maana haiwezekani wewe mtu mmoja upende kuiba na uchukie kuiba.

Combination ya Pinda na Kikwete ilikuwa mbaya kabisa maana wote wana hulka zinazolingana, kutopenda kusimamia sheria na kupenda kumridhisha kila mtu.

Tanzania has lost nearly 8 years to no national direction and directional leadership.

Tumevumila udhaifu wa Pinda kwa karibia miaka 8, halafu eti anataka kuwa Rais. Kwa nchi zenye uongozi madhubuti, Pinda hakustahili kuwa hata Mkuu wa Mkoa.
 
kiongozi makini ni yule anayefanya maamuzi kwa hekima. moja ya mawaziri wanaoitia hasara serikali kwa maamuzi yake ni dk magufuli kuna madeni makubwa ya fidia yaliyotokana maamuzi tata kiongozi makini ushirikisha wataalam na washauri katika maamuzi tatizo watu wengi wanaompinga mh pinda ni mafisadi wezi wa mali ya umma ambao wanakimbilia ikulu kwenda kufanya ujangili
 
Pinda ni aina ya viongozi ambao maamuzi yao huegemea zaidi kuonekana mtu mwema...

Kwa kifupi si kiongozi aliye na uthubutu...
Kiongozi anayeona aibu kutetea sheria za nchi huku akiogopa kuliathiri kundi fulani hafai hata kidogo katika kutetea maslahi ya taifa.

Nafasi ya viongozi wa aina hii ni kwenye makanisa ni misikitini.

Mizengo Pinda hatufai na hafai kuliongoza taifa.
 
Wananchi wampe nafasi Stephen Wassira
Hoja siyo wananchi wampe nafasi Stephen Wassira bali Stephen Wassira ndiyo awape nafasi wananchi wamchambue na kumpima katika mizani ya utendaji mahili wa ofisi ya Rais.
 
Ni wapu.mbavu tu ndio wanaweza kusema kuwa pinda anafaa kuwa rais wa nchi hii.
Pinda ni zigo zito lisilobebeka,bora nikalipigia kura jiwe kuliko kumpigia kura yangu Pinda
 
siku moja Wasira naye kwenye pati kaukasi alisema kama mbunge hawezi kumpinga rais kwasababu ni rais wake!!. pia ni mlalamishi sana. kwenye mchango wake mjadala wa escrow akasema ''kuna mtu tajiri anaetaka urais anatuvuruga''. juzi kavaa koti vibaya anamlalamikia membe. hii miwatu lalamishi na yakutia hurumahuruma ni yakuikataa kabisa.
 
kiongozi makini ni yule anayefanya maamuzi kwa hekima. moja ya mawaziri wanaoitia hasara serikali kwa maamuzi yake ni dk magufuli kuna madeni makubwa ya fidia yaliyotokana maamuzi tata kiongozi makini ushirikisha wataalam na washauri katika maamuzi tatizo watu wengi wanaompinga mh pinda ni mafisadi wezi wa mali ya umma ambao wanakimbilia ikulu kwenda kufanya ujangili
unafikiri pinda aneweza kupambana na mafisadi iwapo anawaogopa TATOA?
 
Ni wapu.mbavu tu ndio wanaweza kusema kuwa pinda anafaa kuwa rais wa nchi hii.
Pinda ni zigo zito lisilobebeka,bora nikalipigia kura jiwe kuliko kumpigia kura yangu Pinda
Mkuu,

Hoja yako inapoteza maana kwa watu wenye fikra pana unaposema bora kwenda kulipigia kura jiwe. Watu wenye fikra pana watakaposoma hoja yako watashindwa kutofautisha mawazo yako na mtu asiyejitambua.

Kama maana yako ndiyo hiyo, basi na wewe umepotea kifikra!
 
Uchambuzi mzuri sana wa Ng'wamapalala.

Pinda ni furushi zito ambalo haliwezi kubebeka na jamii yoyote inayotaka maendeleo. Huwezi kuongoza na kupata mafanikio kama una compromise na sheria. Kwa ujumla uongozi wa Kikwete kwa kiasi kikubwa umeshindwa kwa sababu ya kutosimamia sheria na tamaa ya kutaka kumridhisha kila mtu.

Hakuna kiongozi anayeweza kumrudhisha kila mtu, ukiona kiongozi anaridhisha kila mtu yaani wanaoibiwa waridhike, wanaoiba waridhike, utambue kiongozi huyo ni mnafiki maana haiwezekani wewe mtu mmoja upende kuiba na uchukie kuiba.

Combination ya Pinda na Kikwete ilikuwa mbaya kabisa maana wote wana hulka zinazolingana, kutopenda kusimamia sheria na kupenda kumridhisha kila mtu.

Tanzania has lost nearly 8 years to no national direction and directional leadership.

Tumevumila udhaifu wa Pinda kwa karibia miaka 8, halafu eti anataka kuwa Rais. Kwa nchi zenye uongozi madhubuti, Pinda hakustahili kuwa hata Mkuu wa Mkoa.

Yeah,

You have pretty nailed it
 
Mwaka 2008 baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu nafasi yake. Mizengo Pinda aliyeshika nafasi yake alitarajiwa kuja na moto mkali zaidi wa kiutendaji. Kuna baadhi ya Watanzania walishangilia sana ujio wa Mizengo Pinda.

Itakumbukwa kuwa Lowassa aliyeangushwa na kashfa ya mradi tata wa umeme wa Richmond, alishaanza kuonyesha machachari yake hasa katika kusimamia suala la elimu ambapo alihamasisha ujenzi wa shule za sekondari za kata na miradi mingine.

Pinda aliingia akiwa amevaa ngozi ya kondoo, huku akijiita mtoto wa mkulima. Leo ni miaka zaidi ya saba imepita, tunamwona Pinda halisi alivyo. Kuna kila dalili kwamba amepwaya katika nafasi hiyo.

Tofauti na walivyokuwa mawaziri wakuu wengine, Pinda hajaonyesha ubunifu katika mambo mbali mbali na kuyasimamia. Badala yake amekuwa mtu wa kuonekana wakati wa matukio huku ukitaka uongozi wake tuupime katika mzani wa upole na umasikini. Uongozi wa Tanzania hauwezi kupimwa pekee katika mzani wa upole na umasikini. Hatuwezi kuwa na kiongozi anayejivunia umasikini katika Taifa lenye mazingira ya market economy. Umasikini si turufu ya uongozi, bali kiongozi mzuri ni yule anayekerwa na umasikini badala ya kuutukuza na kuuenzi, ndiyo maana kila siku watanzania wengi wanatafuta njia ya kupambana na umasikini.

Kukitokea vurugu, wananchi wa Mtwara wameandamana, Waziri Mkuu Pinda anakwenda kutuliza, madaktari wamegoma, anakwenda kuzungumza nao, wenye malori na mabasi wamegoma, anakwenda kuwabembeleza.

Nchi hii ilipofika, hatuhitaji kiongozi atakayeridhisha watu bali kiongozi atakayetoa dira ya Taifa inayojari Taifa ili tuvuke na kufika salama kule wananchi wanataka Taifa lifike. Mchekeshaji maarufu duniani, Bill Cosby, aliwahi kusema; ‘’I don't know the key to success, but the key to failure is trying to please everybody’’. Kwa lugha ya mashuleni kijijini Bariadi, alimaanisha kuwa, hajui njia ya kuyafikia mafanikio, lakini njia ya kutofanikiwa ni kumridhisha kila mtu.

Huu ni udhaifu, haiwezekani kiongozi ashughulikie matukio tu wakati anaweza kuboresha utendaji ili mambo yasiharibike. Kutokana na udhaifu huo, hata mawaziri walio chini yake hawawajibiki ipasavyo na wale wachache wanaowajika, anajitokeza na kuwapiga stop. Ndiyo maana hivi karibuni, Wabunge walimtaja kuwa mmoja kati ya mawaziri wanaopaswa kuwajibika kutokana na kushindwa kusimamia kazi zao.

Nilipatwa na mshangao baada ya kukutana vichwa vya habari vinavyosema ‘’WAZIRI MKUU PINDA AMUONYA VIKALI MAGUFULI’’, vingine vilisema, ‘’ SERIKALI YAMZIMA MAGUFULI’’.

Ndani yake kulikuwa na habari inayosema,

Kilichonifanya kuduwaa na kushangaa zaidi ni pale Pinda aliponukuliwa akisema,

Yaani Magufuli anayezilinda barabara zetu kwa kutumia sheria zilizopo ili zisife mapema anampiga stop eti ashauriane kwanza na wale wanaotakiwa kufuata sheria. Sheria ikishatungwa na kupitishwa haiwezi tena kutaka mashauriano ili kuifuata. Huu siyo muswada wa sheria.

Mizengo Pinda amesomea sheria na lazima aelewe kuwa sheria inapotungwa na kupitishwa, hakuna tena majadiliano. Kwa macho ya Mizengo Pinda, kosa la Magufuli ni kuilinda hiyo sheria bila kuwashirikisha wanaoivunja. Jamani, unapomkamata mwizi unamshirikishaje? Unashauriana naye nini ili mpate uamuzi wa pamoja kama siyo kuanza kujenga mazingira ya rushwa?.

Huyu ndiyo eti anataka awe Rais ili aweze kupambana na ufisadi achilia mbali makampuni makubwa ya kimataifa ambayo mengine yana dictate foreign policy za mataifa ya Magharibi. This is fun to say the least.

Kikubwa zaidi, Mizengo Pinda alishatamka hana nia ya kuwa Rais wa Tanzania kama alivyonukuliwa na Januari 25, mwaka 2012 akisema,

Unaweza kusoma interview yake kupitia hapa,

Ni nini tena kimemtuma/kimemkuta atake kuwa mgombea Urais?. Watanzania tusikubali kufanywa wajinga na wanasiasa aina ya Mizengo Pinda. Lazima tuwakatae kwa nguvu zote.

Wanasiasa wa aina ya Mizengo Pinda hawafai, hawatufai na hawalifai Taifa. Ni bora waende kuangalia na kuendeleza mashamba yao ya zabibu na kuchunga ng’ombe.

ANGLI4.jpg

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwaongoza viongozi wa Kanisa la Anglican kutembelea shamba la zabibu na malisho ya ng’ombe kwenye shamba lake lililopo Zuzu Dodoma Februari 9, 2015. Baadhi ya viongozi hao ambao walikwenda kujifunza kwa lengo la kuanzisha shamba linalofanana na hilo Dodoma ni Askofu Dickson Chilongani wa Dayosisi ya Dodoma (wapili kushoto), Askofu Maimbo Mndolwa wa Dayosisi ya Tanga (kulia kwake) na kulia ni Re. Canon, Johnson Chinyongole ambaye ni Katibu Mkuu wa Kanisa hilo

Acha uongo wewe na wachangiaji wako ambao wote mpo timu moja, ivi unafikiri Pibda utamlinganisha na huyo wa kwenu?
 
kiongozi makini ni yule anayefanya maamuzi kwa hekima. moja ya mawaziri wanaoitia hasara serikali kwa maamuzi yake ni dk magufuli kuna madeni makubwa ya fidia yaliyotokana maamuzi tata kiongozi makini ushirikisha wataalam na washauri katika maamuzi tatizo watu wengi wanaompinga mh pinda ni mafisadi wezi wa mali ya umma ambao wanakimbilia ikulu kwenda kufanya ujangili

Dr Magufuli anaangushwa na wenye mamlaka ya juu akiwemo huyo Pinda kwa lengo la kujipatia zaiiidi ya 10% kwa kuliibia taifa hili na sisi wananchi kwa ujumla! Magufuli yupo sahihi na anasema waziwazi kabisa "...mimi nasimamia sheria zilizotungwa ndani ya Bunge! Sheria hazifutwi kwenye majukwaa ya siasa, zinafutwa ndani ya Bunge!" "...Mimi kama msimamizi wa barabara siwezi kutia saini boti zipite kwenye barabara hizi kwenda Mwanza hatuna barabara za kupitisha uzito wa tani hizo labda watengeneze za kwao au wapitie Kenya!" Hizo kesi/hasara unazozizungumza wewe zimetengenezwa na wakubwa wa Dr Magufuli! Ova
 
Sheria hazina hekima bali kutunga sheria ndiyo kunatakiwa hekima. Sheria ikitungwa, kinachobaki ni utekelezaji.

Wanasheria wa serikali na mahakama zetu zimejaa wala rushwa na kwa maana hiyo, usishangae sana pale serikali inaposhindwa kesi mahakamani. Wanasheria wa serikali wanahongwa ili kuleta utetezi dhaifu katika msingi wa serikali kushindwa kesi.

Hujasikia hata Rais Kikwete na yeye akishangaa kwa nini serikali kupitia DPP na TAKUKURU wanashindwa kesi kila mara mahakamani.
 
Ama kweli siasa ni mchezo mchafu leo hii mnatumika na kudiriki kumchafua Mizengo Pinda kisa tu mnamuhofia kwenye mbio zenu za urais si busara hata kidogo mleta mada posho unayopewa na mgombea wako isikutie wehu ukaendelea na uchafu kama huu vinginevyo utalaaniwa na mungu kwa kusema uongo na kuchafua watu mitandaoni.Acha tabia hii chafu
 
Dr Magufuli anaangushwa na wenye mamlaka ya juu akiwemo huyo Pinda kwa lengo la kujipatia zaiiidi ya 10% kwa kuliibia taifa hili na sisi wananchi kwa ujumla! Magufuli yupo sahihi na anasema waziwazi kabisa "...mimi nasimamia sheria zilizotungwa ndani ya Bunge! Sheria hazifutwi kwenye majukwaa ya siasa, zinafutwa ndani ya Bunge!" "...Mimi kama msimamizi wa barabara siwezi kutia saini boti zipite kwenye barabara hizi kwenda Mwanza hatuna barabara za kupitisha uzito wa tani hizo labda watengeneze za kwao au wapitie Kenya!" Hizo kesi/hasara unazozizungumza wewe zimetengenezwa na wakubwa wa Dr Magufuli! Ova

Sheria gani anazosimamia magufuli mara kwa mara amekuwa akifanya maamuzi ya hovyo kwa kukurupuka kabisa na kuitia serikali hasara kwa kulipa fidia mbalimbali.Uvunjwaji hovyo wake wa nyumba za watu bila kufuata sheria kwa kisingio cha kutanua barabara kumeugharimu sana serikali kwa kulipa fidia na tumeshuhudia ukamatwaji wa meli ya samaki bila kufuata sheria serikali imeshitakiwa mahakamani tumeshindwa kesi pamoja na rufaa bado tukashindwa tumeamriwa tulipe fidia ya sh.billion 2 kwa wamiliki wa meli kwa uzembe wake wa kufanya maamuzi kwa kukurupuka bila kufuata sheria hiyo ni hasara kubwa hicho kiasi cha pesa tungewekeza mfano kwenye huduma mbalimbali za kijamii kama kununua madawati kwa ajili ya mashule,kujenga vituo vya afya na nyumba za walimu kwa hapo tu tungekuwa tumepunguza kwa kiasi kikubwa cha changamoto hizo kwenye jamii badala yake mipesa yote hiyo tumelipa fidia wamiliki wa meli ya samaki kwa sababu ya maamuzi magumu yasiyo makini kwa kukurupuka bila kufuata sheria.Swala lingine la Magufuli ni ufisadi wake wa kuuza nyumba za serikali kwa bei ya kutupa wakati akiwa waziri wa ardhi,nyumba na makazi wakati wa utawala wa serikali ya awamu ya tatu rais akiwa Benjamin Mkapa hivyo alikuwa waziri je akiwa rais si atauza kila kitu hata mbuga za wanyama pamoja na rasilimali zingine za nchi.Alafu msisahau Magufuli ni mgonjwa wa moyo amewekwa valve mara kwa mara amekuwa akienda ujerumani kwa matibabu shughuli za mikiki mikiki kama za urais haziwezi Afya mgogoro ndiyo maana kwa kipindi hiki amepwaya sana .Tuwe makini sana urais ni taasisi nyeti inahitaji mtu mwenye Afya njema,busara na hekima katika maamuzi yake,muaminifu na muadilifu katika kuongoza taifa.
 
Teh!

Sometimes unaweza ukadhani unambomoa mtu, kumbe unamjenga vilivyo mbele ya macho na masikio ya Wanajamii.

Binafsi (ambaye ni muumini wa siasa,maadili na mienendo ya Pinda), uzi huu umenibariki na kuniongezea Imani kubwa juu ya Mh.Pinda. Naomba kabisa nieleweke hivyo.

Pamoja na disqualifications ambazo mtoa uzi kazitoa,lakini sehemu kubwa sana ya uzi huu IMEMBARIKI mtoto wa Mkulima(hope wengi mko mashahidi wa jambo hili).

My take; Pinda anauwezo mkubwa sana kifikra na kiutendaji. ALIPOSEMA HANA HAMU YAKUGOMBE,ALIMAANISHA HIVYO TOKA MOYONI.

Lakini marakadhaa nimewaeleza humu ndani kuwa,nimefuatilia nyendo na habari kadhaa kutoka ndani ya CCM & Jamii yote ya Watanzaia kwa Ujumla, nimegundua kuwa PINDA ameandaliwa na kushawishiwa na aina ya watu wenye nia njema na Taifa hili(wakiwamo wazee kadhaa na makada wa CCM).

Sina nia ya kuweka ligi hiyo au kupinga na mtu humu ndani,lakini niwasihi mfanye uchunguzi,mtabaini hilo.

All in all, time is coming and it (time) has never lied.

Over!
 
Ama kweli siasa ni mchezo mchafu leo hii mnatumika na kudiriki kumchafua Mizengo Pinda kisa tu mnamuhofia kwenye mbio zenu za urais si busara hata kidogo mleta mada posho unayopewa na mgombea wako isikutie wehu ukaendelea na uchafu kama huu vinginevyo utalaaniwa na mungu kwa kusema uongo na kuchafua watu mitandaoni.Acha tabia hii chafu

Mkuu;
wala usipanic, dunia imekuwa kijiji na kila mtu yupo huru kuvuruga vyovyote anavyoviona sahihi kwake. Lakini,mwisho wa siku, ni hekma ya Mungu ndiyo hutenda kazi.

Nakuhakikishia Pinda hawezi kuchafuliwa ktk macho ya watanzania wenye nia njema na Taifa hili kwa style ya kina Ng'wapalala wafanyavyo hivi.

Nimeipenda sana speech ya MAKONDA ile juzi akiwaeleza watanzania kuhusu uchafu & udhaifu wa Lowasa.

Yaani kama mtu ni #kimeo , huwez hata kupepesa macho kumtukana. Lakini mtu kama yu Imara(kwa namna ya kina Pinda), lazima akili ikuzunguke kuwa nikwanamna gani,kwa kashfa ipi au kwa udhaifu upi nimchafue mtu huyo. Ndo maana jamaavijana wa akina Lowasa, Membe(kama bado wapo) na wengineo huja kujificha na kubwabwaja yakwao humu ndani.Maana waziwazi wataumbuka kwa roho zao mbaya na vijiba vyao vya roho.

Nadhani watazichota vilivyo mwaka huu(kama walivyoshauriwa na MAKONDA!!).
 
Back
Top Bottom