Tumkatae Mizengo Pinda na watendaji wa aina yake

Tumkatae Mizengo Pinda na watendaji wa aina yake

Bado mnafikiria Pinda! Hana issue huyu. Hafai.
 
Acha uongo wewe na wachangiaji wako ambao wote mpo timu moja, ivi unafikiri Pibda utamlinganisha na huyo wa kwenu?
Mkuu,

Huyo wa kwetu ni nani?

Ingekuwa vizuri ukabainisha uwongo wangu ili ulisaidie pia jukwaa katika mjadala kuhusiana na msingi wa hoja yako.
 
pinda anachafuliwa na mafisadi ambao wanaona hawana mahala pa kuponea lazima tukiri mnyongeni lakini haki yake mpeni pinda ni wise man hata kama haumpendi labda tofauti ya kimaslahi lkn ukweli utabaki hivyo
 
Kiongozi anayeona aibu kutetea sheria za nchi huku akiogopa kuliathiri kundi fulani hafai hata kidogo katika kutetea maslahi ya taifa.

Nafasi ya viongozi wa aina hii ni kwenye makanisa ni misikitini.

Mizengo Pinda hatufai na hafai kuliongoza taifa.
Kuna wale pia wanaodai kulinda/kutetea sheria kwa kuvunja sheria, hawa pia hawatufai!
 
kwa wale wanaomtetea Pinda kama mnataka Tanzania iwe na uongozi wa ovyo kwa miaka mingine mitano au kumi ijayo tuchagueni Pinda. Pinda akiwa rais basi tuombe tuwe na waziri mkuu mchapakazi, lakini ikitokea waziri mkuu naye akawa aina ya Pinda, mambo yatakuwa ovyo kuliko ilivyo sasa.
 
kiongozi makini ni yule anayefanya maamuzi kwa hekima. moja ya mawaziri wanaoitia hasara serikali kwa maamuzi yake ni dk magufuli kuna madeni makubwa ya fidia yaliyotokana maamuzi tata kiongozi makini ushirikisha wataalam na washauri katika maamuzi tatizo watu wengi wanaompinga mh pinda ni mafisadi wezi wa mali ya umma ambao wanakimbilia ikulu kwenda kufanya ujangili

Sijui the exact definition ya neno fisadi uliyonayo, lakini kwa Pinda kuwa rais no with capital letters NO, sijui ni ujangili gani hujaona Pinda akiwa Pm, jamani itoshe tu kusema Tanzania is too large for Pinda, it's unfortunate that we can't turn back the time, if that was possible Pinda should have stayed away. Ni mtizamo wangu, Pinda doesn't have what it takes to be the president of this country.
 
Tangu uhuru nch hii haijawahi kupata waziri mkuu bomu kama mizengo kayanza pita pinda.CCM tumebaki na mtu makin mmoja tu nae ni stephen WASIRA
 
Pinda mimi na familia yangu yote pia ukoo wangu hatuwezi kumpa kura zetu.
 
Tangu uhuru nch hii haijawahi kupata waziri mkuu bomu kama mizengo kayanza pita pinda.CCM tumebaki na mtu makin mmoja tu nae ni stephen WASIRA

hakuna mahala nimesema pinda awe rais mi mwanaccm ninayetambua kanuni muda wa kampeni bado ila nimesema pinda is a wise man ni mtulivu ni mwaadilifu sana wanaotaka pinda aonekane ni fisadi ni mafisadi wanaomwonea wivu
 
siku moja Wasira naye kwenye pati kaukasi alisema kama mbunge hawezi kumpinga rais kwasababu ni rais wake!!. pia ni mlalamishi sana. kwenye mchango wake mjadala wa escrow akasema ''kuna mtu tajiri anaetaka urais anatuvuruga''. juzi kavaa koti vibaya anamlalamikia membe. hii miwatu lalamishi na yakutia hurumahuruma ni yakuikataa kabisa.

Huyu hapa stivin wasira masatu
 

Attachments

  • 1423985017953.jpg
    1423985017953.jpg
    16.6 KB · Views: 83
Uchambuzi mzuri sana wa Ng'wamapalala.

Pinda ni furushi zito ambalo haliwezi kubebeka na jamii yoyote inayotaka maendeleo. Huwezi kuongoza na kupata mafanikio kama una compromise na sheria. Kwa ujumla uongozi wa Kikwete kwa kiasi kikubwa umeshindwa kwa sababu ya kutosimamia sheria na tamaa ya kutaka kumridhisha kila mtu.

Hakuna kiongozi anayeweza kumrudhisha kila mtu, ukiona kiongozi anaridhisha kila mtu yaani wanaoibiwa waridhike, wanaoiba waridhike, utambue kiongozi huyo ni mnafiki maana haiwezekani wewe mtu mmoja upende kuiba na uchukie kuiba.

Combination ya Pinda na Kikwete ilikuwa mbaya kabisa maana wote wana hulka zinazolingana, kutopenda kusimamia sheria na kupenda kumridhisha kila mtu.

Tanzania has lost nearly 8 years to no national direction and directional leadership.


Tumevumila udhaifu wa Pinda kwa karibia miaka 8, halafu eti anataka kuwa Rais. Kwa nchi zenye uongozi madhubuti, Pinda hakustahili kuwa hata Mkuu wa Mkoa.

Nakubaliana na wewe mia kwa mia. Binafsi nimetokea kuamini kuwa moja ya majanga makubwa yanayolikabili taifa hili sasa ni kuosimamia sheria. Miaka kama 3 iliyopita katika mkoa mmoja, Diwani wa chama tawala alihamasisha vijana wafanyabishara kuvunja sheria za nchi. Watendaji katika eneo hilo waliwafungulia mashataka hao vijana pamoja na diwani wao. Diwani alipoona mambo yameharibika, alikimbila kwa Mkuu wa Mkoa kuomba msaada. Mkuu wa Mkoa alimwita Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa Halmashauri na watendaji wengine kuwaamrisha kufuta haraka hayo mashataka. Katika mkoa huo huo, watendaji waliwakamata watu kutoka nchi jiarani walioingia nchini kwetu bila kufuata utaratibu na kuvuna maliasili za nchi yetu. Watu hao walikabidhiwa Polisi ili kuendelea na taratibu za kisheria. Mkuu wa Mkoa aliingilia kati na kuamuru waachiwe, eti kudumisha mahusiano mazuri na nchi jirani! Katika mazingira kama hayo, kuna sheria tena? Pathetic; to say the least!.
 
tatizo la vijana wa ccm mko busy kulumbana wenyewe kwa wenyewe mmejigeuza adui ndani ya adui matokeo kashfa mwatoa nyie mwajisafisha wenyewe utakuta mtu yuko busy kutafuta ya kiongozi ndani ya chama kuliko kuwa busy kutafuta madhaifu ya upinzani tatizo maslahi binafsi
 
Back
Top Bottom