Tumieni simu kukamata trafiki wakipokea rushwa

Tumieni simu kukamata trafiki wakipokea rushwa

Zeni2017

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2017
Posts
1,247
Reaction score
534
d9d2683b6c8282c69d74496d9d88cf11.jpg

Hizi simu zina camera sio kwa sababu ya kupigia picha za insta. Wala hizi simu hazina mitandao kwa ajili ya kufanyia umbea kwenye What's Up.

Polisi wanachukua rushwa barabarani na simu mnazo. Wakimuita mtu pembeni wachukueni video. Kama ni kumuandikia mtu faini wamuandikie hadharani.

Na nyie wakuu wa polisi hakikisheni polisi wenu wanaelewa kuwa ukeshia sio kazi yao. Polisi hakusanyi hela yeyote barabarani. Anandika faini tu.

Tukio lolote la uhalifu piga video weka kwenye mtandao. Ndivyo wanavyofanya wenzetu nchi zilizoendelea.
 
Hii ni kweli mkuu...inatakiwa tuwe pasu kwa pasu. Tutumie camera za Kwenye simu hata kwa manufaa ya taifa na maadili pia
 
Na pale wanapokupa notification ya 2011 nayo upige picha????
 
Litraffic limoja limeniboa sana leo.
 
Ukitumia simu inakua ngumu kidogo kwasababu lazima uishike katika angle fulani ili uweze kufotoa au kurekodi.

Nawashauri mnunue smartwatch ambayo unaweza kufotoa au ku record tukio saa ikiwa mkononi bila mtu kushtukia.

Kama unataka naweza kukuuzia kwa bei ya kutupa
 
Sawa ngoja kesho nianze hiyo kazi, nihakikishieni tu Usalama wa viatu vyangu kwa kuwa nitatembea sana.
 
Hizo picha unazipeleka wapi baada ya hapo? PCCB si nsio wanasema ni maelezo na sio ushahidi au utaambiwa sio rushwa bali ni moral mistake
 
Hizo picha unazipeleka wapi baada ya hapo? PCCB si nsio wanasema ni maelezo na sio ushahidi au utaambiwa sio rushwa bali ni moral mistake

Hata ukiziposti kwenye mtandao bosi wao atakuwa mavini kwa wakuu wake.
 
Chukulia video mia zienee fb polisi wanachukua rushwa bosi wao atakaa kimya?
 
ila Rushwa aisee yaaani nampa 5000/10000 badala ya 30,000 wacha tu rushwa iendelee tuuu hamna namna
 
Kama mkubwa kishasema ni za kubrashia viatu sisi tutafanyaje tena mjomba ?
 
ila Rushwa aisee yaaani nampa 5000/10000 badala ya 30,000 wacha tu rushwa iendelee tuuu hamna namna

Tatizo lako unafikiri mtoa rushwa hana hatia. Ili kukomesha hili suala tunatakiwa tuwe wanoko tuwapige picha wote polisi na mtoa rushwa. Wote wanaikosesha serikali mapato. Wote ni wezi.
 
Ukitumia simu inakua ngumu kidogo kwasababu lazima uishike katika angle fulani ili uweze kufotoa au kurekodi.

Nawashauri mnunue smartwatch ambayo unaweza kufotoa au ku record tukio saa ikiwa mkononi bila mtu kushtukia.

Kama unataka naweza kukuuzia kwa bei ya kutupa
Mawasiliano yako please naitafuta mnooo
 
Hiyo ya Traffic nayo unaita rushwa? Kwanza huwa tu wanatusaidia maana unampa elfu 5 unapona faini ya elfu 60. Mkianza kuwarekodi ndio watazidi kuwa wakali na mwisho mtanaanza kulalamika kuwa faini kubwa sana, mara traffic wamekuwa TRA n.k Tuache uongo Traffic huo msaada wa kibinadamu wa kukutaka msaidiane sio Rushwa hiyo tuite Takrima tu.

That's the spirit and I am not gonna say the big word.
 
Back
Top Bottom