Tumia Viagra Hii Ya Asili

Jamani eeeh...Kama una hangover usi-comment hadi ikuishe please. Soma hii makitu upate knowledge! Preta@ hebu kuja hapa please....

Njia bora ya kuondokana na uchovu (hangover) ni kunywa kiasi au kuacha kabisa unywaji pombe. Kamwe dawa ya hangover sio kuzimua kwa pombe asubuhi ya siku nyingine! Kama utashindwa kujizuia kunywa pombe na unataka kuondoa uchovu wa ulevi wakati wa asubuhi, ni vyema utengeneza na kunywa mojawapo wa juisi zifuatazo:

1. Sri lankan Soother

Blend kwa pamoja juisi ya balungi (grapefruit) 600ml (1 pint), juisi ya ndimu vijiko viwili vidogo (2 teaspoons) na jira (cumin) kijiko kimoja kidogo. Kunywa kabla na baada ya kunywa pombe. Juisi ya balungi na juisi ya ndimu pamoja na kuupa mwili vitamins mbalimbali na fructose pia husaidia kusafisha ini kwa maana ya kutoa na kuyeyusha sumu zitokanazo na pombe. Jira husaidia uyeyushaji na kusaidia mwili kushughulikia sumu.

2. Roman Relief

Blend pamoja juisi hizi: juisi ya baggage (250ml), juisi ya figiri (celery) 250ml na unga wa majani ya coriander (vijiko vidogo viwili). Cabbage ilikuwa mashuhuri kwa Warumi kama tiba ya kuzuia kulewa na hangover. Cabbage ina glutamine ambayo hukinga ini dhidi ya madhara ya alcohol. Figiri na coriander husaidia kupunguza madhara ya alcohol mwilini.

www.asiliyako.blogspot.com
 
Samahani haya matunda ya strawberries ni yepi

Afadhali, wewe wauliza. Kwanini usiandike kila kitu kwa kiswahili tu? Mtu wakati somo linkolea halafu unakutana na kikwazo cha lugha.
 
Ushauri mzr sana. Asante imeeleweka vizuri tu.
 
Afadhali, wewe wauliza. Kwanini usiandike kila kitu kwa kiswahili tu? Mtu wakati somo linkolea halafu unakutana na kikwazo cha lugha.
mambo mengine hayana kiswahili ndugu. Mfano strawberry kiswahili utaita stroberi. Sasa hicho sio kiswahili bali kuchapia kiingereza. Nakushauri u-google utaona kwa picha.
 
Afadhali, wewe wauliza. Kwanini usiandike kila kitu kwa kiswahili tu? Mtu wakati somo linkolea halafu unakutana na kikwazo cha lugha.

Bado angeandika kwa kiswahili ingekuwa issue pia maana kiswahili chake ni stroberi, tufanye kama tumekutana na mchina inabidi tunaonyeshana kwa picha

mambo mengine hayana kiswahili ndugu. Mfano strawberry kiswahili utaita stroberi. Sasa hicho sio kiswahili bali kuchapia kiingereza. Nakushauri u-google utaona kwa picha.

Asante mkuu, ku Google mchina wangu unasumbua, lakini nilienda moo nikayapata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…