Tumia Viagra Hii Ya Asili

Tumia Viagra Hii Ya Asili

Jamani eeeh...Kama una hangover usi-comment hadi ikuishe please. Soma hii makitu upate knowledge! Preta@ hebu kuja hapa please....

Njia bora ya kuondokana na uchovu (hangover) ni kunywa kiasi au kuacha kabisa unywaji pombe. Kamwe dawa ya hangover sio kuzimua kwa pombe asubuhi ya siku nyingine! Kama utashindwa kujizuia kunywa pombe na unataka kuondoa uchovu wa ulevi wakati wa asubuhi, ni vyema utengeneza na kunywa mojawapo wa juisi zifuatazo:


1. Sri lankan Soother

Blend kwa pamoja juisi ya balungi (grapefruit) 600ml (1 pint), juisi ya ndimu vijiko viwili vidogo (2 teaspoons) na jira (cumin) kijiko kimoja kidogo. Kunywa kabla na baada ya kunywa pombe. Juisi ya balungi na juisi ya ndimu pamoja na kuupa mwili vitamins mbalimbali na fructose pia husaidia kusafisha ini kwa maana ya kutoa na kuyeyusha sumu zitokanazo na pombe. Jira husaidia uyeyushaji na kusaidia mwili kushughulikia sumu.

2. Roman Relief

Blend pamoja juisi hizi: juisi ya baggage (250ml), juisi ya figiri (celery) 250ml na unga wa majani ya coriander (vijiko vidogo viwili). Cabbage ilikuwa mashuhuri kwa Warumi kama tiba ya kuzuia kulewa na hangover. Cabbage ina glutamine ambayo hukinga ini dhidi ya madhara ya alcohol. Figiri na coriander husaidia kupunguza madhara ya alcohol mwilini.

www.asiliyako.blogspot.com
 
Kujiamini kwa mwanaume lijali ni pale anapomtosheleza mwenzi au mpenzi wake wakati wa kufanya mapenzi. Na furaha ya mwanamke ni pale anapofikishwa kwenye utoshelevu anaoutarajia kutoka kwa mwanaume au mwenzi wake wakati wa kufanya mapenzi. Kutokana na uhitaji na shauku ya kutaka kuwafikisha wapenzi wao kwenye utoshelevu imewalazimu baadhi ya wanaume kutumia madawa ya kuongeza nguvu za kiume ikiwemo Viagra. Madawa hayo licha ya kuwa na athari kiafya kwa wanadamu hususan wanaume wanayoyatumia lakini pia imekuwa ni chanzo cha vifo vya baadhi ya wanaume wanaotumia madawa hayo hasa pasipo kufuata ushauri wa kidaktari. Si aghalabu kusikia matukio ya vifo vya wanaume kwenye nyumba za kulala wageni na watu wengi wamekuwa wakijiuliza nini tatizo au chanzo cha vifo hivyo. Wengine wamekuwa wakihisi pengine chanzo cha vifo hivyo ni kuzidiwa na dozi za mapenzi wakati wa kungonoka kutoka kwa wapenzi wao.
Watu wengi hawajui kwamba vyakula vyetu vya asili ni Viagra tosha kabisa ambavyo vikitumiwa katika mchanganyiko fulani wanaume wanapata msisimko wa kufanya mapenzi kwa maneno rahisi vyakula hivi vikitumiwa kwa kufuatisha mchanganyiko fulani ni Viagra tosha tena ya asili na iliyo salama kabisa kwa asilimia 100. Hapa nitakwenda kueleza baadhi ya vyakula au michanganyiko ya vyakula ambayo mwanaume akiitumia jongoo litapanda mtungi sawasawa na kuwafanya wenzi wao kuwa na furaha kwa kufikishwa wanapotaka wafikishwe.

Moja: Mwanamke mtengenezee mpenzi wako ‘Banana Milkshake’ mida ya jioni ili usiku akupandishe kileleni. Namna ya kutengeneza: Osha matunda ya strawberries kama 5-10, ondoa vikonyo vyake na kata katikati vipande viwili kila tunda. Menya ndizi mbivu 2-3 na kata kata vipande. Weka maziwa glasi moja kwenye blender na pia tia strawaberries na ndizi. Weka asali vijiko 2 vikubwa badala ya sukari. Funika blenda na tengeneza milkshake yako . Weka milkshake kwenye glasi na mpe mwenzi wako anywe taratibu. Hii licha ya kuongeza msisimko wa kufanya tendo la ndoa (libido) pia ni mahususi kwa kuzalisha homini za mapenzi (sex hormone production).

Pili: Changanya asali na unga wa iliki na na unga wa pilipili kiasi. Mwanaume tumia mchanganyiko huo na unaweza kuboresha zaidi kwa kula pamoja na yai moja la kuku wa kienyeji lililochemshwa kiasi (half boiled) kila siku hadi mambo yawe sawasawa.


Tembelea
http://asiliyako.blogspot.com/

Ushauri mzr sana. Asante imeeleweka vizuri tu.
 
Afadhali, wewe wauliza. Kwanini usiandike kila kitu kwa kiswahili tu? Mtu wakati somo linkolea halafu unakutana na kikwazo cha lugha.
mambo mengine hayana kiswahili ndugu. Mfano strawberry kiswahili utaita stroberi. Sasa hicho sio kiswahili bali kuchapia kiingereza. Nakushauri u-google utaona kwa picha.
 
Afadhali, wewe wauliza. Kwanini usiandike kila kitu kwa kiswahili tu? Mtu wakati somo linkolea halafu unakutana na kikwazo cha lugha.

Bado angeandika kwa kiswahili ingekuwa issue pia maana kiswahili chake ni stroberi, tufanye kama tumekutana na mchina inabidi tunaonyeshana kwa picha

strawberry_1694249043.jpg
 
mambo mengine hayana kiswahili ndugu. Mfano strawberry kiswahili utaita stroberi. Sasa hicho sio kiswahili bali kuchapia kiingereza. Nakushauri u-google utaona kwa picha.

Asante mkuu, ku Google mchina wangu unasumbua, lakini nilienda moo nikayapata.
 
Back
Top Bottom