Abtali Mwerevu
JF-Expert Member
- May 5, 2013
- 773
- 668
Kumekuwa na malalamiko mengi ya wafanyabiashara kuwa, wanauza pesa nyingi lakini mwisho wa biashara hawaoni kitu. Lawama imetupiwa katika maeneo mengi, lakini eneo mojawapo ni eneo la uchawi wa chuma ulete.
Inaaminika kwamba, uchawi wa chuma ulete ni aina ya uchawi ambao mtu huja dukani kwako, akanunua kitu fulani kisha akakupa pesa ambayo huwa na uwezo wa kupora pesa zako zingine. Zipo hadithi zinazosema kuna watu wana hela ambapo akikupa, hela hiyo inamrudia punde tu anapoondoka dukani kwako! Na wapo wengine wenye pesa zinazovuta pesa zingine!
Kama unafanya biashara na una wasiwasi pesa unazopata zinapotea katika mazingira usiyoyaelewa, unahisi unaibiwa kwa uchawi wa chuma ulete, tiba ni mkaa. Tiba hii ni komesha na imekuwa ikitumiwa na wafanyabiashara wengi kwa muda mrefu.
Namna ya kufanya
Chukua kipande kidogo sana cha mkaa, kidogo kama harage. Kiweke mahali ambapo huwa unatunza pesa zako pale unapopewa na wateja unapouza bidhaa zako. Unapokiweka, tamka maneno haya, “NAONDOA UCHAWI WA CHUMA ULETE KWA KIPANDE HIKI KIDOGO CHA MKAA.” utatamka siku ya kwanza pekee unayoweka kipande chako cha mkaa. Kikipotea, unapoweka kipande kingine utatamka maneno hayohayo.
Baada ya kufanya hayo, endelea na biashara yako. Pesa zako haziwezi kupotea labda ujichanganye mwenyewe katika mahesabu unaporudisha chenji. Endapo urudishaji chenji ni changamoto kwako, unashauriwa kutumia kikokotoo cha kununua au kilichomo katika simu yako.
Kufahamu kama dawa imefanya kazi
Unaweza kupima kama umefanikiwa kwa kuandika katika daftari kila mteja anayenunua. Unapofunga biashara yako, hesabu pesa ulizouza, kisha linganisha na idadi ya pesa uliyoandika katika daftari, endapo viwango vitaendana, umeweza kukomesha tatizo. Kama utaona kwamba viwango haviendani, siku inayofuata, kuwa makini katika kuandika kila unachouza na pesa uliyopewa, unapofunga hesabu zako, hesabu zitaendana na utakuwa umekomesha tatizo.
Weka mkaa, andika hesabu zako na utagundua hakuna tena upotevu wa pesa. Kumbuka kuwa makini katika hesabu hasa unaporudisha chenji, na jitahidi katika siku za majaribio ya dawa, uuze wewe mwenyewe.
Fahamu Mengi, Jiunge Katika Group Letu la WhatsApp Hapa