Augustine Moshi
JF-Expert Member
- Apr 22, 2006
- 2,556
- 1,394
Huwa inasemwa mwanasiasa ni mtu anayeweza kuzungumza kwa saa nzima bila kusema kitu. Yaani ukimsikiliza anahutubia saa nzima baadaye ukitafakari alisema nini unagundua kitu. Hicho ni kipaji.
Webometrics rankings za Julai mwaka huu zinaonyesha UDSM ni ya 42 Afrika, Nairobi ni ya 13 na Makere ni ya 14. Wametuacha mbali sana wakati miaka ya nyuma tulikuwa mbele yao. Kwa nini?
Viongozi wa UDSM na wa Elimu Tanzania walipoulizwa kulikoni wamesema “tumeyapokea na tutayafanyia kazi”. Haya ni majibu yasiyoonyesha kuwepo kwa mpango wowote wa kufanya vema zaidi. Ni ya kisiasa. Tutoke huko; tutoe majibu yanayoelezea, angalau kwa kijumla, ni hatua gani zitachukuliwa.
Wako wasomi wa kutosha UDSM. Idara nyingi zimejaa PhD holders, tena PhD zao zikiwa za kutoka vyuo vizuri sana. Staff profile ya UDSM is as good as any.
Tunakwama wapi? Ni kwenye ICT department ya UDSM na mipango ya motisha kwa wasomi. ICT department haihuishi website mara kwa mara, na kuna link nyingi sana ambazo aidha hazifunguki au hazina kitu chochote. Acheni uvuvi website maintainers wa UDSM! Mnaaibisha chuo na taifa. Tunadharauliwa sana kutokana na uvuvi na uzembe wenu. Resign if you are not a fit and proper person.

Viongozi wa chuo wabuni utaratibu wa kuwapa motisha wasomi ili watoe machapisho kwenye majarida ya maana (they should publish in indexed journals). Mfano, you give TZS 1.0 million (or so) for a singly authored paper in a journal that is indexed by SCOPUS, TZS 0.5 million for being part of two authors for such a journal and TZS 100,000 for being part of more than two authors of a SCOPUS indexed journal. Huu ni mfano tu.
Nia yangu ni kusema maendeleo sio lelemama. Hayaletwi na maneno ya kirahisi tu kama “tumeyapokea na tutayafanyia kazi”. Lazima viongozi wawe na tabia ya kusema “tumeyapokea na tutafanya hiki na hiki na hiki” They should outline a plan. They don’t do that because they have no plan, and that is unacceptable.
Ili kufisha kawaida hizi mbaya, itabidi tuanze kwa kuviacha vyuo vyetu view huru. Nusu ya Baraza la Chuo (University Council) iteuliwe na serikali na nusu wawe ni wasomi na wafanyakazi wa chuo wanaopigiwa kura. Mwenyekiti wa Baraza ateuliwe kwa kura za members wengine wote wa Baraza. Kisha Baraza liteue vingozi wote wakuu kwa njia ya applications and interviews. Siyo kisiasa.