Tumeumbwa Ili iweje?

Tumeumbwa Ili iweje?

Wakuu habari za wasaa huu,

Leo nimeulizwa swali la ghafla na mdogo Wangu , nimeshindwa Nini cha kumjibu
Nikaona sio Vibaya niwashirikishe , pengine nikaambulia Jambo,

KUSUDI HASA LA BINADAMU KUWEPO DUNIANI NI NINI?

KWANINI TUMEUMBWA ?

nasema michango yenu karibuni👊
Tumeumbwa ili Tumjue Mungu, Tumpende, Tumtumikie na mwisho Tufike kwake Mbinguni (kwa mujibu wa mafundisho yetu Wkatoliki).
 
Maswali Kama haya ndio msingi wa dini kuanzishwa maana watu walijiuliza wakakosa majibu . Tumeumbwa Ili tufurahie uzuri wa Dunia na baadae tusepe Kwa Muumba.
Huko kwa Muumba kuko kweli? Tuna uhakika?
 
Nadhani ni upuuzi tu,bora tusingekuwepo.ukiangalia mauaji yanayotokea sehemu mbalimbali duniani na tabu nyingi zilizopo kwa baadhi yetu utagundua kuna kitu kama upendeleo hivi
Mauaji, upendeleo unafanywa na nani? Je ndio lengo la kuwepo hapa duniani ili tuuane, tusipeane haki?
 
Tumeumbwa Ili tufurahie uzuri wa Dunia na baadae tusepe Kwa Muumba.
Umemaliza mkuu, hilo ndilo kusudi la Mungu ila kuna muhuni sijui aliwaza nini akatengeneza Pesa, leo hii km huna Pesa utakufa na njaa huna Furaha, kusudi la Mungu wewe kua hapa duniani uishi kwa Furaha amani na upendo vitafuatia Ila dhumuni na lengo la kwanza la Mungu kumuumba mwanadamu aishi kwa Furaha

Ndio maana wanaita Happy New Year hakuna pahala utaona umeambiwa Love New Year wala Peace New Year wala Sad New Year
 
Mimi binafsi nimeumbwa ili nimuabudu Mungu.

Maana Mungu ni Mungu wa sifa
Kuabudu ni nini au ni mambo gani?Je ukiyagawa maisha yako kwa asilimia, Kuabudu kunachukua asilimia ngapi na je kwa asilimia ulizotenga katika maisha yako kwa ajili ya Kuabudu, ni kweli umeumbwa ili kumuabudu Mungu?
 
Eron musk,Bill gate,Jack ma, Bakhressa,Diamond,
Hawa wote wametumia karamq na vipawa waliovyopewa na Mungu,kujifanya Dunia Iwe Bora,kwa kutoa ajira,kubuni tekinolojia zinazosaidia wanadamu,ebu fikiria zisingekuwrpo smart phone,Ndege,magari,internet,
Na wewe tumia karama yako kuifanya Dunia Iwe Bora,
Sio kuishi kama ngombe au mbwa,kula,kunya,na kulala tu,
Bado swali liko pale pale, ili iweje? Maana hatuishi muda wote, sasa tumeletwa hapa ili iweje?
 
Bado swali liko pale pale, ili iweje? Maana hatuishi muda wote, sasa tumeletwa hapa ili iweje?
Ili tufurahie maisha ya dunia mwisho tukishachoka kuishi tukafukiwe shimoni, umefurahi?!
 
Bibafsi namshukuru sana aliyeniumba.
Nimeweza kuiona dunia na mambo yake.

Na nina uhakika baada ya kuishi hapa duniani kwa furaha tele nitaendelea na maisha mengine mazuri zaidi ya haya.
 
Ni ili uifanyie Dunia ipendeze na mwisho uwe mbolea ya Dunia. Ila ujitahidi kuacha photocopy kama ukumbusho.
 
Unauliza kama Atheist ama Believer?!! Cos sion ugumu wa hilo swali?!

Km Believer Tunaamini Mungu katuumba ili tumjue,tumtumikie tupate kufika kwake uko juu mbinguni

Km Atheist; Hamna alieumbwa ila bado tunaendelea kufatilia origin of life mzee
 
Back
Top Bottom