Tumetoka mbali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumetoka mbali

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Lizzy, Jan 2, 2010.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Tumetoka mbali
  Nlidhani tutafika mbali
  Lakini kumbe najidanganyaaa
  Waweza nieleza
  Wapi nilikosea
  Maneno yako yanichanganyaaa


  Nilikukubali…Hukunijali
  Nilikupenda… Ukanitenda
  Hata kama marafiki … naomba uache unafiki
  Sema nini wewe ulitaka… Zaidi ya mimi kunipata
  Taratibu hunny ungenambia
  Nisije jidanganya utaponikimbia
  Nakupenda baby mara nyingi ulinambia
  Naumia sasa na sijui nani ntamlilia
  Maisha yangu mimi umeyatia doaaa
  Sijui nani tena atakayenitoaaa
  Maumivu nnayoyasikiaaaa


  Mapenzi… mapenzi ni kitu gani
  Nsipopata toka kwako….. yangu ntampa nani
  Urafiki ndio tulipoanzia....kufika katikati tukapotea njia
  Kama nimekosa naomba msamaha
  Nakuahidi sitokuletea karaha
  Kama kukupenda…mimi nilikupenda
  Na japo wanitesa sitoacha kukupenda
  Nikisoma sielewi ….Sababu kwako sijiwezi
  Chakula nacho kinarudi ….Kulia mimi sina budi
  Kwaajili yako nliahidi kutopenda tena
  Sababu nlijua nshapata wangu wakufa na kuzikana
  Siwezi acha kulia ….Sababu naumia
  Kama kwako nimeshindikana
  Wapi mi ntawezekana
   
 2. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii kitu utadhani imeandikwa na rafiki yangu wa miaka mingi ambaye ametendwa hivi karibuni baada ya kumpenda binti kupindukia.
   
Loading...