Mama yangu alipatwa na kisa kama chako. Mwenyewe anasema katika maamuzi magumu aliyowahi kuyafanya kwenye maisha yake ni kuamua kuachana na Baba yangu bila hata ya mzee kusema rasmi waachane. Walikuwa wameshanileta duniani na mama mpaka kesho nadhani atakuambia kwamba mzee wangu ndo mtu aliyepanga kuolewa naye lakini ndo hivyo, mwenyewe anasemaga "ndo maisha hayo utafanyaje?". Japokuwa anakiri kuwa mzee wangu hakuwahi kumuahidi kwamba atamuoa lakini mwenyewe anasema baada ya kuwa na mahusiano na mtu kwa muda wa miaka minne na kuzaa nae mtoto alifikiria kwamba wataoana. Kumbe mwenzake alikuwa anafikiria vingine.
Sio siri maisha yetu wakati nakua yalikuwa magumu kinoma ila Mungu anajua yule mwanamke alipigana kadri ya uwezo wake. Nakumbuka siku moja mama alirudi nyumbani na mshahara wake akatuita mimi na wadogo zake na ndugu na zangu tuliokuwa bado tunasoma akagawa ile hela yote kwenye ada na tuition na madeni ya chakula. Jioni ilipofika mama inabidi aende kazini (shift ya usiku hospitalini) ikabidi akope tena ili apate nauli ya kwenda kazini, wakati huo nauli ya kwenda mji unaoitwa Pongwe kutoka Tanga mjini ilikuwa shilingi 100 nadhani.
Long story short, hamna mtu ninae mthamini kwenye maisha yangu kama Mama yangu. Naomba sana Mungu aniweke duniani na anipe mafanikio ili nimtimizie Mama yangu ndoto zake zote za maisha.Kwa kweli hata kwenye maisha naheshimu sana wanawake haswa wa kiafrika maana wengi wao wanapitia hizi changamoto kwenye maisha yao.
Sina ushauri wa kukupa lakini labda unaweza kurelate with your situation. Keep your head up, fight, and do what's best for your child, trust me we never forget.
P.S. - Mimi na mzee wangu tupo cool tu, alikuja kuniomba radhi baadae kwa kutokuwepo kwake kwenye udogo wangu.