Tumetoka mbali Sana, lakini hanithamini!

Tumetoka mbali Sana, lakini hanithamini!

Maskini pole sana ila fanya mpango na wewe uanze kufanya yako maana huyo kaishaonesha nia kwamba hakuhitaji
 
Fanya yako,jipange uondoke huyo hakutaki kashahadaika na ulimwengu atakutafutia kila aina ya sababu. Jipange kama ulikuwa hujajipanga akikuletea kashfa ondoka zako siri ya maisha anayeijua muumba
 
mama S, mna mtoto bali hamna ndoa? Wewe unajishughulisha na nini?

Huo ni ulimbukeni wake, komaa na umwambie "hatoki mtu hapa" umemvumila tangu zero to hero, sasa anaona wewe sio size yake.
 
Last edited by a moderator:
Huyo kachanganyikiwa na pesa, anahitaji msaada wako, anakoelekea huenda hajitambui. Hivyo wa kumsaidia ni wewe mwenyewe uliotoka naye mbali. Wengine wapya watambamiza halafu atakuja kurudi kwako yuko hoi. Usikate tamaa haraka ndio changamoto za maisha hizo.
 
Amemharibu vipi? maana ndio leo nasikia mtu anaharibika......hebu fafanua

Huoni kasema ndie mwanaume wake wa kwanza inamaana kwamba ndie kamtoa bikra pili kamtumia kwa miaka 5 yote leo hii anamuona sio si uharibifu huo!!??
 
Nimekua kwenye mahusiano kwa miaka mitano sasa na mpenzi wangu ambae ni mpenzi wangu wakwanza;maisha yalikuwa magumu lakini tulipambana na niliamini kwamba ipo Siku mambo yatakuwa sawa tuu kwa uwezo wa mwenyezi mungu baada ya miaka miwili kweli mwezangu alipata kazi nzuri maisha yakabadilika cha kushangaza toka apate kazi amekuwa akiniambia maneno ambayo siyaelewi "sio lazima mpaka ufe na Mimi; fanya yako "lakini tatizo ni kwamba bado na mpenda;lakini pia nahisi nikotayari kuendelea na maisha yangu please naombeni ushauri na nimezaa nae:
come to me mama s i will cure you baby..
 
Pole, bado una safari ndefu sana katika maisha, piga moyo konde songa mbele
 
Kusoma hujui picha huoni na masikio hayasikii eeeh

Dada ujue ukipenda unakuwa kipofu pia kiziwi. Muda wa kutosha unahitajika ili macho na masikio yazibuke. Hapo ndipo mtu anaweza kufanya maamuzi yanayofaa.
 
nazidi ku-prove men settle to love akiwa 'comfortable' kimaisha...hii ukisubiri mje lia kivulini wote SIIAMINI aisee,wamngoja mtu weee afu anaolewa mwenzio,hehhe i choose to be the latter...poleh dada...pick up ur self and move on
 
Huna kazi ??? Ujasiliamali je?? Achana naye atakupa donda tumbo huyo!!
 
ndo maisha mkuu, ila kama unampenda endelea maana alichokiunganisha mungu, lazima kitimie
 
wakipata hela huwa wanatafuta wa kutumia nae, inauma kweli jamani. Kawaida yao hao mama S, we kama waweza kufanya yako we fanya kama umefikia mwisho wa uvumilivu wako
 
Last edited by a moderator:
nazidi ku-prove men settle to love akiwa 'comfortable' kimaisha...hii ukisubiri mje lia kivulini wote SIIAMINI aisee,wamngoja mtu weee afu anaolewa mwenzio,hehhe i choose to be the latter...poleh dada...pick up ur self and move on

umeona hapo, wacha watafute tu tutakutana kwenye kutumia
 
Back
Top Bottom