Tumeshindwa.....Tuibomoe, Tuijenge Upya Tanzania!....! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumeshindwa.....Tuibomoe, Tuijenge Upya Tanzania!....!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by IsangulaKG, Nov 10, 2011.

 1. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #1
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Huu utakuwa mfululizo wa Makala ya Uchambuzi wa Jinsi Ambavyo Serikali Imeshindwa Kutekeleza Majukumu yake ; Hapa ni Intro tu:

  Mwaka Fulani mkulukulu, akiwa katika msululu mrefu wa magari yaliyokuwa yakipita kwa mbwembwe na Ving'ora katika barabara hii ya vumbi yakiwaongezea wanakijiji uwezekano wa kuugua mafua kwa kuwatimulia vumbi huku yakiacha alama za matairi barabarani ambazo zilitoa nafasi kwa watoto wadogo waliokimbilia barabarani na kugombania nafasi ya kunusa harufu ya diesel kwenye alama za matairi .Kupitia dirishani mkulukulu akaona wanakijiji takribani watano hivi wameinama porini katika mkao ule wa kushusha mzigo kwenye shimo, pembeni alikuwepo mwingine aliyekuwa akisugua 'nyuma yake' kwenye jiwe lililokaa kama ‘v' inayoangalia chini, ikiashiria alikuwa akiswafi nyuma yake baada ya kushusha mzigo kichakani,mkulukulu bila hata kusimama alisononeshwa sana na hali ile ya kuona watu wazima ,tena wenye familia na wenye umri wa kitwa 'baba mkwe' wakijisaidia vichakani. Mawazo haya na sinema hizi zilizidi kuzunguka katika akili yake, hata alipokuwa nyumbani kwake. Alilinganisha mtammbo wa kisasa uliosimikwa maliwatoni kwake ambao ni ‘self sensing' kwamba huitaji kubonyeza popote, ukimaliza haja zako mtambo wenyewe utagundua kuwa umemaliza na kuvuta mzigo wako ukiusafirisha kwenda kwenye sehemu ya kuhifadhia ama kwa kimombo, ‘septic tank' na baadae kusafirishwa hadi baharini ambako hutoa protini kwa viumbe vilivyomo ambavyo wavuvi wakivinasa na kuviuza pale sokoni jirani na kwa mkulukulu, mfanyakazi wa mkulukulu atanunua na kumuandalia huku akiweka vokolombwezo kibao na baada ya mkulukulu kushiba atamshukuru mfanyakazi wake kwa kusema ‘samaki wa leo alikuwa mtamu' huku akisahau kuwa utamu ulitokana na protini aliyoshusha maliwatoni ambayo muda si mrefu ataenda tena kushusha baada ya kushiba ......

  Kesho yake alipofika ofisini , akampigia simu mkuu wa bajeti na kuagiza litengwe fungu kwa ajili ya kujenga maliwato za kisasa katika kijiji kile ile kuwaepusha watu wazima adha za kupigwa chabo na wakwe zao, adha ya kuchomwa na miba vichakani wakati wa burudani ya kujisaidia, adha za kutengeneza vidonda katika 'nyuma zao' kwa kutumia vipande vya miti, majani au mawe kujiswafi baada ya haja. Mkuu wa bajeti akampigia mtunza hazina huku akitaja kiwango cha juu kuliko alichoagiza mkulukulu , huku akikiita, ‘chai'. Mweka hazina naye akaandika cheki ya kiwango kikubwa kuliko alichotaja mkuu wa bajeti ili naye apate ‘chai'. Mafaili yote yakaenda kwa mkuu wa bajeti akaidhinisha fungu la kujenga maliwato kumi za kisasa kabisa katika kijiji kile.
  Kwa kuwa ilikuwa miezi kadhaa kabla ya kampeni za uchaguzi kuanza, mkulukulu aliomba mkuu wa bajeti amtume mtu akanunue matofali na kuyaweka katika eneo zuri linalostahili kujengwa maliwato pale kijijini na kusubiri wakati wa kampeni. Naam wakati wa kampeni ukawadia na katika mojawapo ya ziara yake ya kampeni mkulukulu alipofika pale kijijini, akawaambia wananchi kwa sauti ya mbwembwe,akina mama waliokuwa wamepewa tisheti na vitenge vyenye picha ya mkulukulu na chama chake wakipiga vigelegele japo miguuni baadhi yao hawakuwa hata na kandambili ‘Serikali yetu ina wajali wananchi wa kijiji hiki, mmemona matofali,mchanga na simenti na sasa naagiza ujenzi wa maliwato za kisasa uanze mara moja"! Vigelegele, nderemo na vifijo vikatawala nakuzima kabisa sauti za watoto wachanga waliokuwa wanakosa hewa kutokana na kubanwa migongoni mwa mama zao na vitenge vya ‘Chagua mkulukulu' . Sauti vifijo na vigelegele zikawastua ndege waliokuwa katika vichaka hapo jirani wakifurahia mizigo iliyowekwa jana pasipo kujua kuwa pengine huo ndiyo utakaokuwa mlo wao wa mwisho iwapo ujenzi wa maliwato za kisasa ungekamilika leo.......


  Sina haja ya kukufanya ucheke hapa, bali najaribu kujenga hoja yangu ambayo utatambua nini ninachosema ukiungana nami katika sehemu ya pili ya makala hii...
   
 2. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Okay! nasubiri hiyo ya pili hapa nimemaliza.
   
 3. t

  thedon JF-Expert Member

  #3
  Nov 10, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 461
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 45
  Naisubiri kwa hamu Part II
   
 4. doctorz

  doctorz JF-Expert Member

  #4
  Nov 10, 2011
  Joined: Aug 10, 2010
  Messages: 907
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tanzania ni rahisi kui unda upya bila ya kuibomoa. Ni kuwaelimisha wananchi haki zao (CIVIL WRIGHTS). Ukienda vijijini, ambako watanzania wengi wanaishi, bado hawajui haki zao na wajibu wa serkali yao juu yao. Tujitahidi kuwaelimisha wananchi hili. Kuna udikteta wa aina mbili. Udikteta wa kiongozi na washikaji wake na mwingine ni ule wa chama kimoja kushika hatamu kwa muda mrefu. Huu wa pili ni mbaya zaidi kwani unajificha nyuma ya Demokrasia. Lakini unadumaza maendeleo. Hadi sasa hamna upinzani wa kweli kugombania haki za walala hoi. Hadi kitokee chama chenye mwelekeo huo...... Watanzania tupo kwenye mikono ya udikteta wa CCM.
  Great spirits have always encountered violent opposition from mediocre minds...   
 5. lukatony

  lukatony JF-Expert Member

  #5
  Nov 10, 2011
  Joined: Mar 25, 2011
  Messages: 428
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  mkuu makala zako ulizokusudia zaweza kuwa nzuri!maana hii yenyewe imekaa vizuri!jitahidi kuandika kwa uwazi kabisa then utakuwa umesaidia jamii
   
 6. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #6
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,070
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  wengine kwa kusoma tu wavivu kweli.
  napita
   
 7. k

  king kong Senior Member

  #7
  Nov 10, 2011
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 106
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mpaka ibomoke ili tuijenge na kuheshimiana.
   
 8. Puppy

  Puppy JF-Expert Member

  #8
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 2,276
  Likes Received: 662
  Trophy Points: 280
  Tungoje kidogo idondoke ili tujenge kwa tofali mpya
   
 9. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #9
  Nov 10, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Imejengwa vibaya! msingi wake ni wa matope!lazima ibomolewe ili ijengwe vizuri
   
 10. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #10
  Nov 10, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,821
  Likes Received: 10,116
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda sana naamini itakpomalizika itakua inafanana na Mna of the People (just prediction)
   
 11. f

  firehim Member

  #11
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii makala nitaifuatilia. Twambie itakuwa inatoka lini.


  Tanzania mpya inawezekana.
   
 12. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #12
  Nov 10, 2011
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Tena tuibomoe wenyewe ili tuijenge upya wenyewe bila kusaidiwa na kiumbe yyt.
   
 13. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #13
  Nov 10, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,996
  Likes Received: 2,651
  Trophy Points: 280
  Hii makala sintoikosa hata kidogo ntahakikisha naisoma kila toleo,Ahsante sana mkuu.
   
 14. 2

  21DEC2012 Senior Member

  #14
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 116
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  umetumia akili kama Michael Scofield ''Wentworth Miller'' kwenye Prison Break.
  Naisubiri Part II.
   
 15. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #15
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Tunahitaji Kuubomoa msingi wa Ubepari na Ukabaila uliojengeka juu ya misingi ya Ujamaa
   
 16. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #16
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Inakuja wiki ijayo....Kaa mkao wa kula
   
 17. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #17
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Itakuwa inatoka Kila wiki (Jumamosi/Jumapili) Hapa Hapa..
   
 18. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #18
  Nov 10, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Tutangoja hadi lini...Tuwarithishe wanetu uharibifu uliotokana na Tamaa za wenzetu wa kizazi hiki Hiki?
   
 19. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #19
  Nov 11, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Nimeshapost Supplement ambayo ni mwendelezo wa Sehemu ya Kwanza.....Usikose kufuatilia Uongozi wa Mkulukulu na Hatima ya Nchi yetu
   
 20. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #20
  Nov 11, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  tunaisubiri sana hiyo part pili mwana wane. Nalog off
   
Loading...