kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Waangalizi wengi wa uchaguzi hasa barani Afrika wanakuwa ni watumishi wa umma walioteuliwa na Serikali zao kuja kujifunza namna uchaguzi ulivyoendeshwa lakini pia kupata mbinu mpya za kuwashauri watawala namna ya kushindi chaguzi zijazo.
Ni mara chache sana waangalizi wa nje wasiotokana na mfumo wa serikali kuruhusiwa kuingia nchi yenye uchaguzi kwa shughuli za uangalizi. Kwa waangalizi wa ndani ambao wengi wao ni asasi za kiraia mara nyingi ufungwa na tamaduni, taratibu na misismamo ya kisiasa ya wagombea.
Kuwategemea waangalizi hawa kwenda kinyume na matakwa ya regime iliyopo ni vigumu kwa sababu kwa asilimia kubwa awalindwi na sheria bali ukingiwa kifua na watawala waliopo.
Kwa tafsiri hii, MWANGALIZI SAHIHI WA UCHAGUZI NA ANAYEWEZA AKAELEZA UKWELI WA KILICHOTOKEA NI MWANANCHI PEKEE.
Hivyo kwa anayetaka kujua uchaguzi ulikuwa huru na haki wauliza wapiga kura, angalia nyuso zao, sikiliza majadiliano yao, angalia mienendo yao ukiona wanajadili chini chini, ukiona awashangilii bali wanaendelea na shughuli zao basi jua hakukuwa na uhuru wala haki.