Tumeshakufa tukafufuka tusiogope kujitoa kunahitajika

Tumeshakufa tukafufuka tusiogope kujitoa kunahitajika

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
24,984
Reaction score
61,200
Wasaalam ndugu zangu
Kwanza nataka niweke mambo mawili sawa
Mosi,Mimi ndege JOHN ndiye Yule Yule ambaye nimekuwa kwa muda mrefu nikitafuta majibu ya maswali jana,Leo na kesho na nashukuru mwenyezi Mungu nimeyapata majibu hayo na ndo maana Jf imekuwa sehemu muhimu Sana ya Mimi kujifunza nawapongeza Sana wote bila kujali itikadi zetu
Pili,nataka niweke wazi msimamo wangu wa kisiasa lakini pia niwashirikishe Jambo zuri Sana na kubwa

Mimi nilikuwa mwana CCM mzuri Tena mwenye vyeo vyake na katika uongozi wangu nimekutana na viongozi wakubwa wa chama.na hata Sasa hapa nilipo naandika maada hii nikiwa katika ofisi ya mjumbe wetu wa mtaa Ni mwanaccm mzuri Sana tumebadilishana naye mawazo kwa muda mrefu
Nilichogundua mpaka Sasa watanzania wengi Ni waoga kupindukia wanaogopa kupoteza nafasi zao za kazi,wanaogopa kukosa kazi,wanaogopa watanzania wenzao ambao Ni maaskari,wanaogopa kikosi maalumu,wanaogopa makomandoo.

Hata hivyo siwashangai kuwaogopa watu hao kwa sababu kiukweli hata Mimi nawaogopa ukitaka kuwaona wale majamaa angalia wakiwa wanawasindikiza wafungwa kwenda mahakamani wana Tisha Sana yaani nilikuwa sijui Kama serikali Ina watu wakubwa namna ile ma giant makubwa yameshiba yanapiga ngumi balaa wako pale ukonga wanafanana na kizazi Cha Goliath unaweza ukafikiri sio watanzania kwa jinsi walivyo weusi lakini kumbe wametoka hapahapa ndani ya nchi.

Kwenye maisha bhana tunatakiwa tupambe maisha yetu kwa kujitolea kusiko na mwisho tusifanye nao Vita badala yake tuendelee kujifunza na kufundisha watu kuhusu habari za uhakika.. watanzania Wana tatizo moja kubwa wengi hawana maarifa ya kutosha ya kujua yanayoendelea.tukaeni tuone namna gani elimu ya kisiasa inafikia wengi Tena kwa maneno machache

Namaanisha tuache stori stori na ujanja ujanja habari za matukio na mikutano haitasaidia kitu tunatakiwa tupate wasemaji ambao hawaongei Sana yaani kwao Ni vitendo dhidi ya maneno wachache mtakuwa mmenielewa.tusisubiri viongozi ambao tayari Ni mamilionea kuja kutusemea wakati Kuna vijana kibao ambao ugumu wa maisha unawagusa moja kwa moja kwa sababu hawana uhakika wa biashara zao,hawana uhakika na ajira, hawana uhakika na mahusiano yao ya kimapenzi kwa sababu tu UMASKINI.
namalizia kwa kusema hivi yesu alikufa Mara moja na akafufuka Mara moja lakini sisi tushauliwa Mara nyingi na tumefufuka Cha ajabu tunaogopa vitu visivyo umiza.tuacheni kila kitu Kama tunataka mafanikio kwa sababu tulivyovishika havina thamani Tena baada ya kipindi fulani kupita.
 
Huyu ndege JOHN kuna ka nafasi aliahidiwa lakini kamesha jazwa hivyo matumaini yamekata!
Ninachomshauri atulie,uasi kwa CCM hauwezi kukusaidia!
Upande wa pili ( opposition) ni kugumu sana bora ujipange ukisikilizia 2020 baada ya uchaguzi unaweza kuambulia ka uteuzi!
Sasa hivi hata namba 1 homa ya uchaguzi imeanza kumuingia! Rejea vimkutano vyake na makundi mbalimbali ili kuvuta huruma ya wapiga kura!
 
Ni Vigumu saana Kumuaminisha Kuwa Uongozi wa CCM unamsaada kwa Mlala hoi wa Kawaida! 58 Year bado tunaimba Maji, barabara, sijui Umeme, hovyo kabisa!
Hawawezi hawa wameshindwa, Watanzania pamoja na Kutojitambua hebu tuweni Serious kidogo! Tupo kama Wenda wa Zimu vile.
 
Huyu ndege JOHN kuna ka nafasi aliahidiwa lakini kamesha jazwa hivyo matumaini yamekata!
Ninachomshauri atulie,uasi kwa CCM hauwezi kukusaidia!
Upande wa pili ( opposition) ni kugumu sana bora ujipange ukisikilizia 2020 baada ya uchaguzi unaweza kuambulia ka uteuzi!
Sasa hivi hata namba 1 homa ya uchaguzi imeanza kumuingia! Rejea vimkutano vyake na makundi mbalimbali ili kuvuta huruma ya wapiga kura!
Mwambie sehemu salama kwa watu legelege ni ccm
 
Ndege unataka kuungana na mbuni na kanga maisha ya ardhini ilihali ww ni njiwa sijui mbaiwayu? Bora upiganie huko huko angani, ardhini kunahitaj uwe mgumu sana.
 
Naona akili zimerudi toka likizo maslai yenu yakiguswa mnakua Na akili.
 
Huyu ndege JOHN kuna ka nafasi aliahidiwa lakini kamesha jazwa hivyo matumaini yamekata!
Ninachomshauri atulie,uasi kwa CCM hauwezi kukusaidia!
Upande wa pili ( opposition) ni kugumu sana bora ujipange ukisikilizia 2020 baada ya uchaguzi unaweza kuambulia ka uteuzi!
Sasa hivi hata namba 1 homa ya uchaguzi imeanza kumuingia! Rejea vimkutano vyake na makundi mbalimbali ili kuvuta huruma ya wapiga kura!

Kadri siku zinavosonga vazi La kondoo linapanda thamani
 
Akaunti yako imehakiwa nini maana mpiga zumari wa kijani wa jiwe kuanza kulalamika ni maajabu ,maana nyie huwa ni wa kusifiatu ,pumba ,mchele vyote kusifia mpaka wagonjwa kwenye mafaili milembe na bugando ni kuwasifia tu .
 
Back
Top Bottom