Mnyamahodzo
JF-Expert Member
- May 23, 2008
- 1,935
- 1,006
Nikiwa nasoma shule ya msingi tulifundishwa kuwa " jasusi ni mpelelezi anayevuka mipaka ya nchi kwenda nchi nyingine, kupeleleza au kuharibu kwa maslahi ya nchi yake." Tulifundishwa kuwa majasusi wengine ni vibaraka wa mabeberu. Hivyo tulitakiwa kuwa makini na mtu yeyote mgeni; tumwangalie anafanya nini halafu tukimbie kwenda kutoa taarifa upesi kwa mtu mkubwa yeyote tutakaye mwona karibu, balozi au mwenyekiti wa kijiji. Mwalimu wetu wa Siasa alituaminisha vyema namna vibaraka na majasusi walivyo watu wa hatari na wabaya. Kwa kweli, mgeni hawezi kupita kijijini kwetu bila taarifa kufika mbali na watu wakajua kuwa kuna mgeni anakuja au anapita. Kabla ya kuingia kijijini, kulikuwa na msitu mkubwa wa asili unaozunguka nusu ya kujiji upande wa mashariki hadi kusini magharibi, kaskazini kulikuwa na mapori kadhaa na uwanda mkubwa wa vichaka na nyasi. Kwa kuwa watoto ndiyo tuliokuwa tunakabidhiwa jukumu la kuchunga mbuzi na ng'ombe wachache, kushinda na kucheza porini ilikuwa jadi yetu hivyo tulikuwa wamwanzo kumwona.
Tukiwa mjini, ilikuwa vivyo hivyo. Kila mtu alikuwa anaona anawajibu wa kutoa taarifa au kumtilia shaka mgeni yeyote kabla ya kumzoea na kumfanya sehemu ya jamii. Ilitusaidia sana katika usalama wa nchi yetu. Ninawakumbuka watu waliojifanya wazambia kumbe ni wazimbabwe waliokamatwa pale Ikingula ( karibu na Makambako) walioshuka kwenye treni ya TAZARA kituo cha Chimala na wakawa wanatembea kwa njia za mkato kwenda Makambako. Ni wananchi waliowagundua. Walikuwa wanaongea kiswahili kizuri tu.
Mifano ni mingi. Hoja yangu, mpaka wageni wanaingia nchini na kutuhujumu tumetupia wapi ule uzalendo wetu?
Najua kuna wakati Polisi ukiwajulisha hilo wao wanafikiria kuwa ni fursa kwao kupata hela, fikiria juu ya wale wakongo na wanaijeria wa Kinondoni na Kigamboni, wasomali wa Kijitonyama, Mtoni Kwa Aziz Ally na Chang'ombe, etc