::
Tumependana ndiyo!
Tusichukiane kwa makosa yanayopita.
::
Tumependana ndiyo!
Tusionyeshane jeuri hakuna mkubwa katika kupenda.
::
Tumependana ndiyo!
Usisahau niliyofanya ukakumbuka ambayo sikufanya.
::
Tumependana ndiyo!
Usinipe mitego ya kujaribu upendo wangu,naweza kuteleza nisiinuke tena.
::
Tumependana ndiyo!
Usinipe mgongo mapema,huo uamuzi una wakati wake haulazimishwi.
::
Tumependana ndiyo!
USINIVUNJE MOYO,,UKIUVUNJA VUNJA KILA KIPANDE KITAOKOTWA NA MWENZAKO,LAWAMA ZAKO KWAMBA NILIKUTENDA ZITAKOSA BARAKA.
=
Mmh, mmnamuenzi Chinuua Achebe?
Malenga wetu..ndio tukupe hongera au?
Haya mapenzi yanaua ~sosi Muumin Mwinjuma
Naam, chambilecho, Ngabu.
Ujumbe wako kuntu.
Umegonga penyewe ikulu.
Umeandika na umesomeka.
Yakini pasi utata.
Asiyeelewa kwake imekula.
::
Ha ha ha Umalenga ni fani ya Rutashobolwa
mie mwanafunzi
Umenena kweli Zion Daughter..
Nime-dedicate kwa Wapendanao wawe na hadhari
=
Mzee Mwanakijiji, kuna malenga wapya huku.
Tetra,
ni kweli tumependana
penzi letu linafana
tena linanoga sana
kwani tunaelewana
zaidi tumeshibana
na hata tukigombana
mbali h'tutafikishana.
ni kweli tumependana
si kama zombie wa Kongosho
kisa shamba la korosho
ni kweli tumependana
si kama mchaga wa lara 1
kutwa kuchwa kibaruani
ni kweli tumependana
si kama King'asti na Paw
ata kitukana apewi poo
ni kweli tumependana
zaidi ya babu Asprini
na wakeze themanini
ni kweli tumependana
zaidi ya ma Ngina na Mtambuzi
kamwe sitoki nje, hata niwe nje ya zizi
ni kweli tumependana mzabzab apate somo
la penzi liso kikomo!!!!:yo:
Rutashubanyuma .. Kuna mrithi huku aisieee njoooo broo!
Tumependana ndiyo!
Usinipe mgongo mapema,huo uamuzi una wakati wake haulazimishwi.
Ni muda gani mwafaka kupeana migongo?
Naam!!
Ni kweli tumependana,
Na tena tunapatana
Mioyo imeshikana
Kama kushika supana
Si penzi la kutegana
Ila kutegemeana!
Daima tunawazana
Umbali si kitu bwana
Huwa tunakumbukana
Kila tunapoagana
Simu tunapigiana
Na meseji zashindana!
Na hamu ikitubana
Ya mambo ya kushikana
Wallahi tunapeana
Ni hekaheka ee bwana!
Tukichoka twabebana
Na maji kumwagiana
Kisha tunarudiana
Hilo ni penzi mwanana!!
Kupenda tunapendana
Nisikieni vijana
Ni muhimu kushibana
Siyo kupigana
Wala hamtachokana
Mwisho mje kupigana
Tungo inaisha bwana
Yu wapi wangu mwanana!?
Na. MMM (Tarumbeta ya Kijiji)