Tumemruhusu Rais Magufuli kuikanyaga demokrasia, ameset 'precedence' hata kwa marais wajao

Kansigo

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
2,670
2,156
1. Alianza kuzima bunge live, tukapigapiga kelele tukanyamaza(si wanaharakati wala viongozi wa dini waliobodha kulishughulikia hili, wakaachiwa UKAWA na ACT, matokeo yake likawashinda). J. Kikwete hakuwa mjinga kuruhusu bunge live!

2. Akaja akaikanyaga katiba aliyoapa kuilinda kwa kuzuia mikutano ya vyama vya siasa na maandamano. Wanaharakati na viongozi wa dini wakawa kimya! Wanasiasa wamepigapiga kelele pia limewashinda

3. Baada ya hapo zikaja kauli za kibabe kuwatishia watakaojitokeza kuhoji (Atakayeleta fyoko fyoko atanitambua, mimi sijaribiwi,etc) tukamuacha!

4. Akaja na version ya uteuzi wa makada wa CCM kwenye kila nafasi, bila kujali professionalism wala uzoefu, kikubwa uwe kada. Tumepiga kelele tumenyamaza

5. Amesitisha mchakato wa upatikanaji wa Katiba mpya bila kumshirikisha yoyote. Hakuna hata anayejali hadi najiuliza kama kweli tulikuwa tunaihitaji katiba mpya au ilikuwa ni njia tu ya kumsumbua Kikwete coz tuliaminishwa na baadhi ya makanisa kuwa ni mbaya sana na hafai

6. Sasa Amekuja na mkakati wa kunyamazisha wanaomkosoa, kuanza kupambana na mitandao kama JamiiForums, kupambana na akina Lema na Lissu. Tutapiga kelele tutamwacha aendelee tu(hapa ndo tunaona unafiki wa viongozi wetu wa dini na wanaharakati ambao walikuwa so vocal kipindi cha JK, but awamu hii ni kama wamemwagiwa maji!

My worry ni kwamba Rais Magufuli anaset precedence (atakuwa ndo reference) ya uongozi Tanzania hata kwa viongozi watakaofuatia. Raisi ajaye naye akizuia shughuli za kidemokrasia hatutakuwa na uhalali wala nguvu kumpinga kwa kuwa huyu tumemuachia. Itakuwa ni unafiki wa hali ya juu kwa viongozi wa dini na wanaharakati kumsumbua raisi ajaye kwa kumuachia huyu afanye atakavyo
 
Huwa namshangaa sana ndugu rais anavyohubiri umoja na kufuta tofauti za kivyama wakati yeye ndio amezidi kuziweka mbele tofauti hizo kwa kubagua watanzania wengine na kujaza makada katika kila teuzi zake!

Sijui huwa anaongea kinyume??
 
Hili taifa ni la watu wanafiki saaaana,,,,tuna viongoz mbalimbali wa kidini,lakini hawathubutu hata kutoa ushaur ama tamko juu ya hali inavoendelea nchini,,
 
Umesema ukweli mtupu. Namshangaa anapojinasibu kumuiga Nyerere wakati Nyerere angekuwa hai leo angemshangaa
 
Sasa ameacha kusema mniombee maana anajiamini kuwa hakuna wa kumsumbua, hana aibu kabisa mpaka anasema hadharani bila aibu kuwa katiba nimeiweka pembeni nataka kunyoosha nchi, eti Muhimili wa Serikali umezama kwenda chini zaidi kuliko mihimili mingine, huu ni ulevi wa madaraka na ulimbukeni mkubwa
 
Hili taifa ni la watu wanafiki saaaana,,,,tuna viongoz mbalimbali wa kidini,lakini hawathubutu hata kutoa ushaur ama tamko juu ya hali inavoendelea nchini,,
Halafu ndio hao wanasema maisha katika awamu hii yamekuwa nafuu sana kwa sababu malengo ya ukusanyaji sadaka yaliyowekwa na kanisa yamefikiwa. Viongozi wengi wa dini nchi hii ni manyani wadhalilifu wanaotumikia matumbo yao kupotosha taifa.
 
Make a space kutengeneza strong evidence jukumu letu ni kumkosoa kwa sasa na ukosoaji wetu ukitimia ana lake siku kwa siku asije akapata sababu kuwa akuachiwa nafasi ya kufanya vizuri hata sasa nafasi kapewa yote lakini akuna cha maana alicho Fanya zaidi ya kualibu
 
Vipi manunuzi ya ndege, ugawaji wa fedha kama njugu, ahadi ya kuzipa mahakama mgawo aka cha juu ikiwa washitakiwa wakishindwa kesi za kodi na ujenzi wa Chato International Airport nje ya utaratibu wa manunuzi ya Serikali.
 
Back
Top Bottom