Tumelala giza tumeamka bado hakuna umeme !.

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,933
31,178
Jana Arusha kutwa nzima hakuna umeme,usiku umeme ulirejea saa 7 asubuhi saa 1:43 wamekata.

Tumeshindwa kupasi nguo,vyakula kwenye fridge vimeharibika,tumelipia Dstv full package hatuna tunaweza kutazama.

Kipindi kuelekea Christmas 🎄 majumbani ukiwa mtupu.

Tunajuwa Makamba alihujumu TANESCO hukumchukulia hatua stahiki.

Umempachika Dotto Unaibu Waziri Mkuu na Nishati lakini hakuna cha maana zaidi ya misafara na mbwembwe ambazo hazitusaidii Watanganyika.
 
Mimi niliwahi kusema humu kwamba katika vitu vitakavyoivua nguo hii serikali na kui expose jinsi ilivyo utupu wake ni hili tatizo la umeme.

Kuna vitu unaweza kupiga porojo na blaa blaa, ila kuna vitu vinawagusa watu direct na hata urembe vipi ukweli unabaki pale pale. Hili la umeme halina porojo! Ni ama umeme upo au haupo.
 
mlimnanga sana yule jamaa sasa kinawapata kiberiti alichowasha kimezima!.. mkamuita dictator mlifikiri nchi hii inatakiwa iongozwe soft soft!.
hata hivyo shangazi alishagasema vinampwaya viatu vyakaka!.
nchi inaongozwa na wenye pesa zao amabao wanataka mambo yao yapite ili biashara zao zifanyike!.

alipowagusa hao watu wakubwa mkaanza kusema "haki za binadamu haki za binadamu!"
mmesahau kuna watu walikimbia nchi..?
kama walikuwa ni wenye haki kwanini walikimbilia mafichoni..?
hamtafumbuka macho msipokubali kufumbuliwa!
mmkikaa kimdebwedo hata visivyoliwa vitaliwa.
 
Wapi huko?

Jana Njiro nimetoka misele saa 11 nimeacha umeme haujarudi, nafika nyumbani napo hamna umeme 😀😀
Nikalala zangu, nikaja shtuka saa 8 umerudi.

Leo tunao huku misele, home sijui.
 
Jana Arusha kutwa nzima hakuna umeme,usiku umeme ulirejea saa 7 asubuhi saa 1:43 wamekata.

Tumeshindwa kupasi nguo,vyakula kwenye fridge vimeharibika,tumelipia Dstv full package hatuna tunaweza kutazama.

Kipindi kuelekea Christmas 🎄 majumbani ukiwa mtupu.

Tunajuwa Makamba alihujumu TANESCO hukumchukulia hatua stahiki.

Umempachika Dotto Unaibu Waziri Mkuu na Nishati lakini hakuna cha maana zaidi ya misafara na mbwembwe ambazo hazitusaidii Watanganyika.
Mkome mlishangilia kifo cha Dkt Magufuli
 
We msukuma tulia
Update kwanza ussd
mlimnanga sana yule jamaa sasa kinawapata kiberiti alichowasha kimezima!.. mkamuita dictator mlifikiri nchi hii inatakiwa iongozwe soft soft!.
hata hivyo shangazi alishagasema vinampwaya viatu vyakaka!.
nchi inaongozwa na wenye pesa zao amabao wanataka mambo yao yapite ili biashara zao zifanyike!.

alipowagusa hao watu wakubwa mkaanza kusema "haki za binadamu haki za binadamu!"
mmesahau kuna watu walikimbia nchi..?
kama walikuwa ni wenye haki kwanini walikimbilia mafichoni..?
hamtafumbuka macho msipokubali kufumbuliwa!
mmkikaa kimdebwedo hata visivyoliwa vitaliwa.
 
Wapi huko?

Jana Njiro nimetoka misele saa 11 nimeacha umeme haujarudi, nafika nyumbani napo hamna umeme 😀😀
Nikalala zangu, nikaja shtuka saa 8 umerudi.

Leo tunao huku misele, home sijui.
Niko INTELI huku, kuja ugide bia.
 
mlimnanga sana yule jamaa sasa kinawapata kiberiti alichowasha kimezima!.. mkamuita dictator mlifikiri nchi hii inatakiwa iongozwe soft soft!.
hata hivyo shangazi alishagasema vinampwaya viatu vyakaka!.
nchi inaongozwa na wenye pesa zao amabao wanataka mambo yao yapite ili biashara zao zifanyike!.

alipowagusa hao watu wakubwa mkaanza kusema "haki za binadamu haki za binadamu!"
mmesahau kuna watu walikimbia nchi..?
kama walikuwa ni wenye haki kwanini walikimbilia mafichoni..?
hamtafumbuka macho msipokubali kufumbuliwa!
mmkikaa kimdebwedo hata visivyoliwa vitaliwa.
Kuna watu walikua wanasema wanataka maendeleo ya watu na sio vitu, leo ndio hao hao wanalia na mgao wa umeme. CHUMA aendelee kupumzika kwa amani
 
Back
Top Bottom