Tumekwisha Tanzania! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tumekwisha Tanzania!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lekanjobe Kubinika, Jan 14, 2011.

 1. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mkuchika na Wasira kwa nyakati tofauti wamenukuliwa na vyombo vya habari wakipumua kwamba "Wale wanaodhani Uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha utarudiwa wasahau kwani uchaguzi ulishafanyika kwa kufuata kanuni zilzopo, CCM ndio wameshinda. Mwenye kutengua matokeo haya na mahakama tu, serikali haina uwezo wa kutengua"

  Inaashiria kuwa ni kauli rasmi ya serikali na kwamba serikali hiyo inaenzi uchakachuaji. Sasa serikali ikishasema hayo raia ufanyeje? Maana mahakama inaagizwa kufuata kilichoamuliwa na serikali. Rejea kesi ya Mtikila kudai mgombea binafsi. Pamoja na Mtikila kushinda mahakamani bado serikali ikakata rufaa na hatimaye wakaamua kugoma kabisa kuruhusu, badala yake wakaandika mswada mpya wa kuzuia hilo.

  Serikali yetu ipo kulinda mabavu ya watawala na sio haki za wanyonge. Lugha zao nzuri wakati wa uchaguzi na ni chungu ghafla uchaguzi ukiisha.
   
 2. TATIANA

  TATIANA JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 4,103
  Likes Received: 472
  Trophy Points: 180
  Miaka yote hukuwa unajua serikali yako inaongozwa na watu wenye upeo gani?
   
 3. coscated

  coscated JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,500
  Likes Received: 250
  Trophy Points: 180
  mahakama ikikaa kimya nitashangaa maana sheria na kanuni hazikufuatwa kwa kuwa uchaguzi ulishirikisha idadi ndogo ya madiwani/wapiga kura.
   
 4. m

  mzambia JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  na bado!
   
 5. n

  nyantella JF-Expert Member

  #5
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Mahakama haitasema hadi kesi ipelekwe.
   
 6. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #6
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ndugu zangu naomba niwaweke sawa kuhusu uchaguzi wa meya jiji la Arusha. Ni kweli taratibu zote zilifuatwa katika uchaguzi ule. Uchaguzi ulifanyika baada ya kuahirishwa kutokana na sintofahamu ya mjumbe mmoja ambaye ni mbunge wa viti maalumu kupitia Tanga na ni katibu wa CCM mkoa wa Arusha ambaye ni Mary Chitanda. Kutokana na hilo, ufafanuzi ulipatikana kuwa mjumbe yule ni halali kupiga kura. Utata ule ukawa umekwisha. Ulipowadia wakati wa kupiga kura CDM waliotoka nje kwenda kujadili katika hotel Equator iliyopo mkabala na halmashauri ya Arusha maana ilionekana wale diwani mmoja wa TLP tayari alishanunuliwa na CCM, wakiwa katika kikao hicho wenzao CCM waliendelea na uchaguzi wakisema CDM wamesusia uchaguzi ule na hapo ndipo walipopigwa bao la kisigino na CCM kwani walikwisha saini kwenye orodha ya waliohudhuria kikao kile.
  Baada ya hilo, CDM iligundua CCM wamewazidi ujanja na ndipo walipojenga hoja unazozisikia hadi leo. Kiukweli CDM wakubali kuwa umeja wamepoteza kwa kuzidiwa fitna kidogo na CCM. CCM ilikuwa na wajumbe 16, na mmoja wa TLP 17. CDM 14 na 1 wa TPL 15, CDM wana mapandikizi yao mawili ndani ya CCM hivyo ingewaongezea kura hadi 17. Hivyo ukiangalia kura ambayo ingeamua nani awe meya ni za wale wanafiki wawili wa CCM na mmoja wa TLP basi na si vinginevyo.
  Mwisho, kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ilikaa na kujadili na nilifanikiwa kuiona nakala ya kikao hicho mara baada ya kumalizika ilikuwa inajieleza kabisa na CDM hawana mlango wa kutokea katika hilo.
  Ikiwa kweli CDM wanadhamira ya kutengua matokeo basi wangeenda mahakamani kisha wangeandamana kushinikiza kesi isikilizwe haraka hapo ningeona kuna logic. Viongozi wote wa CDM wanalijua hili kwa mapana na marefu na ndiyo maana hawataki kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi wa meya kwa kuwa kila kitu kipo wazi tena kwa ushahidi.
  Mwisho, naungana na wale wote wanaosema kuwa matokeo ya umeya yatabadilishwa na mahakama pekee kwa kuwa suala hilo ni kisheria. CDM fungueni kesi kupinga matokeo na acheni blah blah za majukwani.
  Nyumba haichomwi kwa maji ya moto.
  Nakaribisha hoja tofauti na ukweli huu, ukihitaji zaidi niPM nikujuze ABC. Habari hii nimeiandika bila kuegemea upande wowote ule.
   
 7. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #7
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ama!!
   
 8. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Maelezo yako ingawa kwa kiasi fulani yana ukweli lakini kuna upotoshwaji wa hali halisi; kwanza hakuna namna ambayo chadema inavyoweza kumkubali huyo mbunge wa Tanga kuwa diwani wa Arusha, ikumbukwe katika ccm tofauti na vyama vingine, wagombea wa viti maalum wanapigiwa kura katika mkoa maalum. Mbali na hayo chadema ilitaka kupeleka wabunge wake wa viti maalum Hai ikashindikana. Tukiliacha hilo, kuna hili la Mkurugenzi kuwa ndiye msimamizi wa uchaguzi. Ni dhahiri jambo hilo halikubaliki. Kisheria Mkugenzi ni katibu wa kikao hivyo hawezi kuhudumia kote kote.
   
Loading...