Cheche Mtungi
JF-Expert Member
- Nov 14, 2010
- 2,619
- 775
Haya yalitamkwa na Katibu Muu Wizara ya Elimu tena ni Prof Mh Sifuni Mchome
Na jana tarehe 19/11 2013
1---Hivi Mh Rais haoni kama hapa tunaiua hii nchi?
2---Wasaliti wakubwa wa nchi hii ni wasomi wetu,hawajiamini na hawatujali kabisa sisi watanzania na watoto wetu.
3---Ina maana hawajui chanzo cha watoto wetu kufeli?
4---Wanashindwa kabisa kubaini matatizo ya walimu wetu?
Naomba niwakumbushe walipokosea
1---Waliajiri walimu ambao hawana viwango katika miaka ya nyuma hasa kuanzia miaka ya 1997 hadi sasa hasa walimu wa shule za msingi
2---Wamesahau kuboresha maslahi ya hao walimu wabovu walioajiriwa katika miaka niliyotaja hapo juu
3---Wamesahau kuboresha miundombinu ya Shule kama nyumba za walimu,maabara na madawati
4---Kuingiza siasa kwenye Elimu, kulazimisha kubadilisha matokeo ya wanafunzi badala ya kufanyia kazi changamoto zilizopo.
Hata mfumo wa elimu yetu pia tunashindwa kuamua nini tufanye? nani ameturoga?au ni ujinga wetu?wasomi wetu mlioko madarakani hata hili la elimu pia linawashinda?sasa tutaweza hata kuwa na ndoto za kwenda sayari ya Mars kama wanavyofanya wenzetu huko ulaya na marekani?
La mwisho nawaomba sana CCM msichezee akili za watoto wetu,mmeharibu kila kitu kwenye nchi hii,mmemilikishana kila kitu,kuanzia viwanja vya mipira,maeneo ya wazi,viwanda,migodi na biashara zote,basi tuachieni elimu ili angalau tuapate pa kutokea sisi maskini,au mnataka tuendelee kuwa watumwa wenu hadi lini?
Mungu atubariki na atupe uelewa hasa 2014 na 2015.
Imeandikwa tarehe 01 Novemba 2013
Mfumo wa Elimu Sekondari wafumuliwa
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, imefumua mfumo wa upangaji alama katika mitihani ya elimu ya sekondari, ambapo sasa mtihani wa mwisho utakuwa na asilimia 60 ya matokeo yote huku daraja sifuri likifutwa.
Kutokana na mabadiliko hayo, mfumo wa tathmini endelevu (CA), unaopima maendeleo ya mwanafunzi akiwa shuleni, ndio utatumika kumpa mwanafunzi asilimia 40 zilizobaki na atapaswa kujua alichopata katika alama hizo kabla ya kuingia kwenye mtihani wa mwisho.
Akitangaza mabadiliko hayo jana Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome, alisema mabadiliko hayo yataanza na wanafunzi wanaoanza mtihani wa kidato cha nne Jumatatu.
Profesa Mchome alisema katika mabadiliko hayo, Wizara imeweka utaratibu wa jinsi mwanafunzi atakavyopata asilimia 40 ya mtihani wa mwisho, kutokana na kazi atakazokuwa amefanya tangu alipojiunga sekondari.
Kwa kidato cha nne, asilimia 15 kati ya 40, mwanafunzi atatakiwa azipate katika mtihani wa Taifa wa kidato cha pili; huku katika matokeo ya mtihani wa kidato cha tatu, kwa mihula yote miwili, atatakiwa awe na asilimia 10, kila muhula akipata alama tano.
Mtihani wa Majaribio (mock) kwa kidato cha nne, mwanafunzi atatakiwa apate asilimia 10 na kazi za mradi alama tano. Kwa mujibu wa Profesa Mchome, matokeo ya kidato cha sita kwa sasa yanafuata mfumo huo na utaendelea kama muundo wa sasa ulivyo.
Mfumo huo utatumika hadi kwa wanafunzi wa kujitegemea ambao alama zao zitatokana na matokeo ya mitihani ya awali.
Madaraja mapya
Profesa Mchome alisema kuanzia sasa kwa vidato vya nne na sita, alama za ufaulu katika masomo zitaanzia A, B+,B, C, D, E na F, ambapo mwachano wa alama kati ya kundi moja hadi jingine utafanana kwa kidato cha nne na cha sita.
Mfumo huo ni tofauti na zamani, ambapo alama za masomo ya kidato cha nne ilikuwa A, B, C, D na F, wakati kidato cha sita ilikuwa A, B, C, D, E, S na F.
"Katika alama hii ya B, kundi la kwanza la B litakuwa la wanafunzi waliopata alama kuanzia 50 hadi 59 na lingine la B+ litakuwa la waliovuka wigo wa B na kufikia wa 60 hadi 74," alisisitiza Mchome.
Alisema pamoja na kuwa na mwachano wa alama 26, alama A kwa miaka mingi imekuwa ikianzia 75 hadi 100, ambapo waliofaulu kwa kiwango hicho walikuwa wachache na hivyo Serikali imeona hakuna haja ya kubadili alama hiyo, badala yake juhudi ziendelee kuongeza kiwango cha ufaulu, ili kupata wanafunzi wengi zaidi katika daraja hilo.
Alama C yenye maana ya ufaulu mzuri itaanzia 40 hadi 49, D ambayo ni ufaulu hafifu itaanzia 30 hadi 39, E ufaulu hafifu sana itaanzia 20 hadi 29 na F ufaulu usioridhisha, itaanzia 0 hadi 19.
Muundo wa madaraja
Daraja la kwanza kwa mujibu wa mfumo huo mpya, daraja la kwanza ambalo ni la kundi la wanafunzi walio na ufaulu, uliojipambanua na bora sana. Daraja la pili litakuwa kundi la ufaulu mzuri sana na daraja la tatu, kundi la ufaulu mzuri na wa wastani.
Daraja la nne litakuwa kundi la ufaulu hafifu na daraja tano litakuwa la ufaulu usioridhisha. Mtihani kidato cha 4 Wakati huo huo, jumla ya watahiniwa 427,906 ambao kati yao 367,399 ni watahiniwa wa shule na 60,507 wa kujitegemea wanatarajiwa kufanya mtihani wa kidato cha nne kuanzia Novemba 4 hadi 21.
Mchome alisema idadi hiyo ya watahiniwa ni pungufu ya watahiniwa 53,508, sawa na asilimia 11.1 ikilinganishwa na 481,414 walioandikishwa kufanya mtihani huo mwaka jana.
Source:http://www.habarileo.co.tz/index.ph...8190-mfumo-wa-ufaulu-kwa-sekondari-wafumuliwa
Na jana tarehe 19/11 2013
Sitta aiumbua Wizara ya Elimu
Jumatano
Novemba 20, 2013
Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii imetangaza rasmi kuzikataa alama mpya za mitihani ya sekondari zilizotangazwa hivi karibuni na Serikali na kuitaka alama zilizotumika mwaka jana kupanga matokeo ya mtihani wa kidato cha nne zitumike mwaka huu.
Kama hiyo pia imeitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuwasilisha ripoti ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuchunguza chanzo cha watoto wengi kufeli mtihani wa taifa wa kidato cha nne mwaka 2012.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Margaret Sitta aliwaleza waandishi wa habari jana kwamba kamati hiyo imejiridhisha kuwa mchakato wa kupata alama mpya zilizotangazwa haukuwashirikisha wadau muhimu ikiwamo Baraza la Mitihani nchini (Necta) "Ilikuwa haifahamu chochote juu ya alama hizo".
Sitta alisema Necta haikupewa fursa ya kujadili mabadiliko hayo kiundani na kusema kuwa wameitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhakikisha mchakato huo unafika kwa wadau wote wa elimu.
"Tumebaini kuwa wadau muhimu hawakufikiwa na wizara. Tumewaeleza wazi kuwa matokeo ya mwaka huu watumie alama za miaka ya nyuma hadi hapo tutakapohakikisha jambo hili limeeleweka vyema na kufikia wadau wote," alisema Sitta.
Alifafanua kwamba kamati hiyo imebaini mpaka sasa mchakato huo haujakamilika, hivyo ni vigumu kuendelea na matumizi ya alama hizo mpya za ufaulu.
"Tumeiomba wizara kuwasilisha ripoti yote ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu Pinda ili tuweze kuijadili kwa kina," alisema na kuongeza:
"Tunataka kuijadili hiyo ripoti kwa kina ili kupata ufumbuzi wa matatizo yanayoikabili sekta ya elimu."
Alisema kuwa mpaka sasa wizara hiyo imeshindwa kuiwasilisha ripoti hiyo katika kamati yake. "Badala yake wamekuwa wakituletea maelezo ambayo ni vigumu kwa kamati yangu kuweza kujadili utekelezaji wake," alisema.
"Tunasisitiza ni lazima wizara ituletee ripoti ili tuweze kuyafanyia kazi mapendekezo yake, kinyume chake itakuwa ngumu kujadili matatizo mbalimbali yanayoikabili sekta ya elimu."
Alisema kuna umuhimu kwa ripoti hiyo kufikishwa mapema katika kamati hiyo kwa maelezo kuwa udhaifu ukijulikana mapema kuna faida.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome akitangaza uamuzi huo mapema mwezi huu, alisema uamuzi wa kubadilisha mfumo huo umechukuliwa kutokana na changamoto
Alama zilizokuwa zikitumiwa awali na Baraza la Mitihani la Taifa (Necta), katika kupanga matokeo hayo, kwa Kidato cha Nne ni A=80-100, B=65-79, C=50-64, D=35-49, F 0-34 kwa upande wa Kidato cha Sita, A=80-100, B=75-79, C=65-74, D=55-64, E=45-54, S=40-44 na F= 0-39.
Alama mpya zilizotangazwa ni A=75-100, B+=60-74, B=50-59, C=40-49, D=30-39, E=20-29 na F=0-19. Alama hizo ni kwa kidato cha nne na sita.
Kwa utaratibu huo, A ilitafsiriwa kuwa ni ufaulu uliojipambanua, B+ ni ufaulu bora sana, B ufaulu mzuri sana, C ufaulu mzuri, D ufaulu hafifu, E ufaulu hafifu sana na F ufaulu usioridhisha.
Katika utaratibu huo, mtihani wa mwisho ulitarajiwa kuwa na alama 60 na alama 40 zitokane na alama za Maendeleo ya Mwanafunzi Shuleni (Continuous Assessment-CA).
Mwaka jana baada ya Serikali kufuta matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne, Necta ilitumia CA ya 30 huku mtihani wa mwisho ukiwa na alama 70.
Source: Sitta aiumbua Wizara ya Elimu - Kitaifa - mwananchi.co.tz
1---Hivi Mh Rais haoni kama hapa tunaiua hii nchi?
2---Wasaliti wakubwa wa nchi hii ni wasomi wetu,hawajiamini na hawatujali kabisa sisi watanzania na watoto wetu.
3---Ina maana hawajui chanzo cha watoto wetu kufeli?
4---Wanashindwa kabisa kubaini matatizo ya walimu wetu?
Naomba niwakumbushe walipokosea
1---Waliajiri walimu ambao hawana viwango katika miaka ya nyuma hasa kuanzia miaka ya 1997 hadi sasa hasa walimu wa shule za msingi
2---Wamesahau kuboresha maslahi ya hao walimu wabovu walioajiriwa katika miaka niliyotaja hapo juu
3---Wamesahau kuboresha miundombinu ya Shule kama nyumba za walimu,maabara na madawati
4---Kuingiza siasa kwenye Elimu, kulazimisha kubadilisha matokeo ya wanafunzi badala ya kufanyia kazi changamoto zilizopo.
Hata mfumo wa elimu yetu pia tunashindwa kuamua nini tufanye? nani ameturoga?au ni ujinga wetu?wasomi wetu mlioko madarakani hata hili la elimu pia linawashinda?sasa tutaweza hata kuwa na ndoto za kwenda sayari ya Mars kama wanavyofanya wenzetu huko ulaya na marekani?
La mwisho nawaomba sana CCM msichezee akili za watoto wetu,mmeharibu kila kitu kwenye nchi hii,mmemilikishana kila kitu,kuanzia viwanja vya mipira,maeneo ya wazi,viwanda,migodi na biashara zote,basi tuachieni elimu ili angalau tuapate pa kutokea sisi maskini,au mnataka tuendelee kuwa watumwa wenu hadi lini?
Mungu atubariki na atupe uelewa hasa 2014 na 2015.