Tumefahamu anakotupeleka Rais Magufuli sasa

Tumeshavuka udikteta sasa tupo Ufashisti

FASCIM
Is radical authoritarian rule characterized by dictatorial power
Forcible suppression of opposition and mobilization of society under a totalitarian ONE party state
Twafaaa
 
Mimi naomba aendelee kukaza kabisa ili mwisho wa siku hata CCM watambue kuwa UTAIFA ni bora kuliko UCHAMA. Until 2020 tutakuwa tunaongea lugha moja kama taifa na hii itakuwa msingi mzuri sana wa kuamua mustakabali wa taifa letu.

Ogoga sana kiongozi asiyependa criticism....yaani yeye anapenda kusifiwa tu hata kwenye mambo ya ajabuajabu! Kiongozi anayetengeneza mitandao ya kumsifia ili aje kuidhihaki jamii kuwa anapendwa!
 
Kwa kipindi chote cha urais wa JPM karibu mwaka mmoja na miezi nane kulikuwa na maswali mengi ni wapi anatupeleka Rais JPM. Kuanzia kisiasa, kiuchumi, kijamii na maendeleo kwa jumla watu walijiuliza mwelekeo wake. Alizuiya siasa ili afanye kazi za maendeleo na alisema anabana matumizi ili kuokoa fedha na aliahidi Tanzania ya viwanda.

Muda huo wote wachunguzi walikuwa wanatazama mwelekeo na viashiria vya azma yake. Kwa maoni yangu hakuna mpya na mwelekeo haujawekewa misingi. Anachokifanya ni kucheza na akili za watanzania na kupigiwa vifijo vya siasa za propaganda na wafuasi wake.

Kinachojidhihirisha kama taifa kuna malalamiko upande mmoja na upande wa pili kuna sifa zisizo mashiko, Bungeni kuna malalamiko ya ubaguzi wa kiitikadi, kwenye serikali kunalalamikiwa matumizi ya madaraka ya kukomowa wapinzani na kukosekana uvumilivu. Kuhusu ajira mianya imejificha bado na biashara zinadorora. Wananchi wanalilia ukata wa fedha na ugumu wa maisha.

Hali hio wenyewe wanaikataa na kusifia tu na hawataki kukosolewa kwa lolote. Misingi imekosekana ya kupigania kile alichokiamini Rais JPM huo ndio ukweli.

ANAKOTUPELEKA.

Kwa mnasaba wa maelezo hapo juu, Tanzania sasa inaelekea kwenye visasi vya ubaguzi na kukomoana, kukosa uvumilivu miongoni mwa watanzania na kukosa umoja wa dhati. Huku ndiko tunakoelekea.

Kwa bahati mbaya JPM na wasaidizi wake hawajaliona hilo na taratibu hii tabia inazoeleka miongoni mwa jamii.

Mifano iko mingi. Mara ngapi serikali imetowa kauli tata za kukatisha watu tamaa na kufanya mambo yasiyo shirikishi ? Kila kinachofanywa kina mnasaba wa kujitafutia sifa NA UMAARUFU TU NA KWA MUDA MFUPI UNAGUNDUWA DHAMIRA ZA KISIASA ZILIZOJIFICHA NYUMA YAKE. Lile la madawa ya kulevya, ufisadi, vyeti, na mekanikia yamepita na mwisho inaonekana kuwalenga watu fulani tu.
Mara ngapi kuna undumi la kuwili wa maamuzi ya serikali? mambo haya huacha mwanya wa ubaguzi na kukosesha umoja kama nilivyosema.

Kule bungeni ni ushahidi tosha wa kipimo cha Tanzania ilivyo. Kama spika imefika mahali anasikitikitia kususiwa futari UNADHANI KUNA NINI? HUO NDIO UHALISIA.

Tumetoka kwenye matatizo yaliyovumilika , sasa tunaelekea kwenye matatizo yanayolazimisha kupotea kwa uvumilivu. Huku ndiko anakotupeleka rais Magufuli.



Kishada.

Kishada hizi ndizo nyufa za kwenye msingi wa nyumba alizozizungumzia Mwl Nyerere, Mwl. alishatoa unabii kazi ya unabii inachukuwa muda mrefu kutokea. Mungu atuepushie mbali haya ya ubaguzi!
 
Huwez kumwelewa mpaka uondoe ukada ulio nao. Kama huwez tambua athali za kiongoz wa nchi kwa kukataza watu wa chama chake wasiende kumwona wa chama pinzani akiwa jela basi ujue una miwani ya ukada machoni. Kama huon ubaguz wa waz dhidi ya wapinzani kupitia mkuu wa nchi jua una matatizo makubwa ya kifikra. All in all nimemkubali mtoa hoja kwamba rais wetu anatupeleka kwenye taifa la kubaguana. tutaanza kuitana sisi wa chama fulan wale wa chama fulan badala ya kusema sisi watanzania. Tutafika huko hata kwenye mambo ya kitaifa
Mkuu huo wingi wa siasa za majukwaani katika kipindi ambacho watu wanatakiwa wawe wanafanya shughuli za maendeleo ndio sababu inayoifanya Afrika idumu kwenye umaskini.

Mambo ya kuwataka wananchi wawe wanakwenda kwenye mikutano ya hadhara katika ile miaka isiyokuwa na uchaguzi ni kutowatendea haki, ni kuwanyima uhuru wa kufanya shughuli za kimaendeleo. Ni kuwadharau pia, kwa maana ya wao kuwa ni watu wasiojua faida za kutafuta riziki.

Kwa wanasiasa siku zote watu huwa ni mtaji wa utajiri wao, kutokujielewa kwao ni faida ya wanasiasa, ambao huandaa kauli mbinu za kuombea fedha nje kwa kisingizio cha vuguvugu za kisiasa. Fedha ambazo kwa kiasi kikubwa huwa hazifanyiwi ukaguzi makini ndani ya vyama vyenyewe, na kutoka kwenye mamlaka za ukaguzi wa fedha.

Siasa zina kipindi chake, na jamii hiyo hiyo inayolishwa siasa, inao wajibu wa kujitafutia riziki.
 
Huwez kumwelewa mpaka uondoe ukada ulio nao. Kama huwez tambua athali za kiongoz wa nchi kwa kukataza watu wa chama chake wasiende kumwona wa chama pinzani akiwa jela basi ujue una miwani ya ukada machoni. Kama huon ubaguz wa waz dhidi ya wapinzani kupitia mkuu wa nchi jua una matatizo makubwa ya kifikra. All in all nimemkubali mtoa hoja kwamba rais wetu anatupeleka kwenye taifa la kubaguana. tutaanza kuitana sisi wa chama fulan wale wa chama fulan badala ya kusema sisi watanzania. Tutafika huko hata kwenye mambo ya kitaifa
Chukua fanta ntalipa
 
Back
Top Bottom