Tumefahamu anakotupeleka Rais Magufuli sasa

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,141
2,000
Kwa kipindi chote cha urais wa JPM karibu mwaka mmoja na miezi nane kulikuwa na maswali mengi ni wapi anatupeleka Rais JPM. Kuanzia kisiasa, kiuchumi, kijamii na maendeleo kwa jumla watu walijiuliza mwelekeo wake. Alizuiya siasa ili afanye kazi za maendeleo na alisema anabana matumizi ili kuokoa fedha na aliahidi Tanzania ya viwanda.

Muda huo wote wachunguzi walikuwa wanatazama mwelekeo na viashiria vya azma yake. Kwa maoni yangu hakuna mpya na mwelekeo haujawekewa misingi. Anachokifanya ni kucheza na akili za watanzania na kupigiwa vifijo vya siasa za propaganda na wafuasi wake.

Kinachojidhihirisha kama taifa kuna malalamiko upande mmoja na upande wa pili kuna sifa zisizo mashiko, Bungeni kuna malalamiko ya ubaguzi wa kiitikadi, kwenye serikali kunalalamikiwa matumizi ya madaraka ya kukomowa wapinzani na kukosekana uvumilivu. Kuhusu ajira mianya imejificha bado na biashara zinadorora. Wananchi wanalilia ukata wa fedha na ugumu wa maisha.

Hali hio wenyewe wanaikataa na kusifia tu na hawataki kukosolewa kwa lolote. Misingi imekosekana ya kupigania kile alichokiamini Rais JPM huo ndio ukweli.

ANAKOTUPELEKA.

Kwa mnasaba wa maelezo hapo juu, Tanzania sasa inaelekea kwenye visasi vya ubaguzi na kukomoana, kukosa uvumilivu miongoni mwa watanzania na kukosa umoja wa dhati. Huku ndiko tunakoelekea.

Kwa bahati mbaya JPM na wasaidizi wake hawajaliona hilo na taratibu hii tabia inazoeleka miongoni mwa jamii.

Mifano iko mingi. Mara ngapi serikali imetowa kauli tata za kukatisha watu tamaa na kufanya mambo yasiyo shirikishi ? Kila kinachofanywa kina mnasaba wa kujitafutia sifa NA UMAARUFU TU NA KWA MUDA MFUPI UNAGUNDUWA DHAMIRA ZA KISIASA ZILIZOJIFICHA NYUMA YAKE. Lile la madawa ya kulevya, ufisadi, vyeti, na mekanikia yamepita na mwisho inaonekana kuwalenga watu fulani tu.
Mara ngapi kuna undumi la kuwili wa maamuzi ya serikali? mambo haya huacha mwanya wa ubaguzi na kukosesha umoja kama nilivyosema.

Kule bungeni ni ushahidi tosha wa kipimo cha Tanzania ilivyo. Kama spika imefika mahali anasikitikitia kususiwa futari UNADHANI KUNA NINI? HUO NDIO UHALISIA.

Tumetoka kwenye matatizo yaliyovumilika , sasa tunaelekea kwenye matatizo yanayolazimisha kupotea kwa uvumilivu. Huku ndiko anakotupeleka rais Magufuli.Kishada.
 

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,332
2,000
Mleta uzi me sijakuelewa labda urudie tena Mada yako

Huwez kumwelewa mpaka uondoe ukada ulio nao. Kama huwez tambua athali za kiongoz wa nchi kwa kukataza watu wa chama chake wasiende kumwona wa chama pinzani akiwa jela basi ujue una miwani ya ukada machoni. Kama huon ubaguz wa waz dhidi ya wapinzani kupitia mkuu wa nchi jua una matatizo makubwa ya kifikra. All in all nimemkubali mtoa hoja kwamba rais wetu anatupeleka kwenye taifa la kubaguana. tutaanza kuitana sisi wa chama fulan wale wa chama fulan badala ya kusema sisi watanzania. Tutafika huko hata kwenye mambo ya kitaifa
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
7,153
2,000
Hakuna jambo baya sana kama serikali iliyoko madarakani kuendeshwa kisiasa.Kiuhalisia Magufuri sio mwanasiasa bali ni mtendaji aliebebwa na utendaji wake kuingia katika siasa.Hili ni tatizo.Tatizo linaanzia pale mtendaji na wanasiasa wanapokutana katikati.Ni lazima mambo yatazidi kuwa magumu zaidi kwa serikali hiyo.
 

Laface77

JF-Expert Member
Jul 9, 2008
2,116
2,000
Na kwa bahati mbaya sana watanzania tumekubali kuingizwa katika mtego huu wa chuki ma visasi!
 

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,166
2,000
......

ANAKOTUPELEKA.

Kwa mnasaba wa maelezo hapo juu, Tanzania sasa inaelekea kwenye visasi vya ubaguzi na kukomoana, kukosa uvumilivu miongoni mwa watanzania na kukosa umoja wa dhati. Huku ndiko tunakoelekea.
Kinachoni ogofya ni hii roho ya kisiasa ambayo naamini anataka kuipandikiza nchini, itafika pahala mwana CCM kuhudhulia msiba wa mwana CUF au Chadema itaonekana ni kama usaliti, baadhi ya indicators ni kama hizi zinazoanza kujionyesha kwa mfano Lema akiwa mahabusu wana CCM kwenda kumjulia hali inasemekana mkuu hakupenda, au watu wakiandamana kumpongeza Rais kwa kazi nzuri anazofanya, basi Intelligensia yetu haigundui hatari yeyote lakini Wapinzani kukaa kufanya kazi zao za Kisiasa ni dhambi. Unajua ni kwanini naogopa sana? Naogopa kwasababu kuna habari kwamba paka ukimfungia chumbani ukaanza kumuadhibu bila kumpa upenyo wa kujiokoa usipokua makini anaweza kukuua vibaya.
 

Masanva Aya

JF-Expert Member
Aug 16, 2016
448
1,000
Tanzania ya leo si moja tena, tuna Watanzania Watanganyika na Watanzania Watanzania.... watu wanapata kiki kwa kulenga watu/kundi na si mfumo, na Watanzania wanaojaribu kuaminishwa na kundi flani kwamba wao ndo hasa Watanzania ndo wale wanaowapa kiki na maandamano ya kuunga mguu (sijui mkono )viongizo wao. na ukiwa na mawazo mbadala wewe ni zaidi ya SHETANI Tanzanaia... Watanganyika Watanzania ndo wenye mawazo ya kuhoji tunapoenda.

wale naojiona Watanzania wa kweli kutotaka kuhoji, kumbukeni Pongezi, ushabiki na sifa kwa viongozi wao zipo jikoni..... zikiiva mzinywe...
 

adden

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
5,479
2,000
we njaa inakusumbua inaonyesha hukupewa ht mualiko wa idd na demu wako amekupiga chini unakuja kuleta shombo zako hapo
 

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,141
2,000
Tanzania ya leo si moja tena, tuna Watanzania Watanganyika na Watanzania Watanzania.... watu wanapata kiki kwa kulenga watu/kundi na si mfumo, na Watanzania wanaojaribu kuaminishwa na kundi flani kwamba wao ndo hasa Watanzania ndo wale wanaowapa kiki na maandamano ya kuunga mguu (sijui mkono )viongizo wao. na ukiwa na mawazo mbadala wewe ni zaidi ya SHETANI Tanzanaia... Watanganyika Watanzania ndo wenye mawazo ya kuhoji tunapoenda.

wale naojiona Watanzania wa kweli kutotaka kuhoji, kumbukeni Pongezi, ushabiki na sifa kwa viongozi wao zipo jikoni..... zikiiva mzinywe...

Kiufupi tunatoka katika matatizo yanayovumilika, tunaelekea katika matatizo yasiyovumilika. Keep my words.

Vyenginevyo JPM na uongozi wake ubadilike.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom