Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 8,801
- 12,248
Nchi hii sasa karibu iwe jehanamu, hakuna raha! Viongozi wetu kutwa kucha wanahubiri vitisho hawataki tufurahi, tupashane habari, tuelimishane! Viongozi wetu wanataka tuwe mabubu, tujikunyate tukitembea na tukikaa. Viongozi wetu wanataka tuwaogope, tusiwahoji wala kuwajadili.
Tumechoka kutishiwa! Viongozi wetu hawataki tuwaze, tufikiri au kutoa mawazo mbadala. Viongozi wetu wanadhani kuwa wao pekee ndiyo wenye akili, wenye mawazo bora zaidi na hawakosei.
Tumechoka! Viongozi wetu hata siku moja hawatufariji wala kutuonea huruma kwa mateso tunayopata kutokana na majanga ya kimaumbile na yale yanatokana na uzembe wao au maamuzi yao ya hovyo.
Tumechoka!