Tumechoka na vitisho, tumechoka kutishiwa, tumechoka

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,784
12,226
Nchi hii sasa karibu iwe jehanamu, hakuna raha! Viongozi wetu kutwa kucha wanahubiri vitisho hawataki tufurahi, tupashane habari, tuelimishane! Viongozi wetu wanataka tuwe mabubu, tujikunyate tukitembea na tukikaa. Viongozi wetu wanataka tuwaogope, tusiwahoji wala kuwajadili.

Tumechoka kutishiwa! Viongozi wetu hawataki tuwaze, tufikiri au kutoa mawazo mbadala. Viongozi wetu wanadhani kuwa wao pekee ndiyo wenye akili, wenye mawazo bora zaidi na hawakosei.

Tumechoka! Viongozi wetu hata siku moja hawatufariji wala kutuonea huruma kwa mateso tunayopata kutokana na majanga ya kimaumbile na yale yanatokana na uzembe wao au maamuzi yao ya hovyo.

Tumechoka!
 
Na unakosea kuwaita viongozi, viongozi hawana sifa walizonazo viongozi.
Ukiwatizama wakiwa wanaadress umma ni ni kuamrisha kwa kwenda mbele kutisha. Sheria na miongozo inayowekwa si ya kutatua changamoto bali .....kukomesha, kuzuia, kudhibiti,...........
 
Mawazo mbadala ya umbea, uongo, unafiki, na udhalimu?
Hayo kaa nayo tu.

Ni lini mlileta mawazo mbadala kwamba nchi ifanaye jambo flani ili iendelee kisha mkakamatwa?

Au mawazo mbadala ni mambo ya kichawi na roho mbaya kwa nchi ndo mnataka yaruhusiwe?

Mawazo yenu ni kusema vibaya serikari na kuizushia uongo pamoja na chuki ndo tuyaite mbadala, kama ni hayo kaeni nayo tu,
Mkishindwa mjiue
 
Wacha ujinga fanya Kazi ule Bata. Hizo ndoto za MCHANA zitakuwehua wewe
Naanzaje Kula bata wakati wakenya Kila siku wananitsha hali ya kiongozi wangu!mpaka nimuone siwaamini wote.hivi unawezaje kuvumilia eti wanadai yupo kwao hospital,kwa jinsi tuliivyowaulia miradi yao km Bomba la mafuta hoima,sgr northern corridor.sasa parachichi tunapeleka ulaya,SA bila wao kuhusika.nataka kumuona siamini mtu asilani.sitaki Kura bata mpaka aonekane
 
Umetishiwa na nani, au sababu ufisadi mliozoea ndiyo unaita unyanyasaji.Hii ni 🇹🇿 mpya kama uadilifu umekushinda hama nchi.
 
Back
Top Bottom