Tumechelewa kupambana na dawa za kulevya?

Oct 5, 2015
90
482
TUPAMBANE NA DAWA ZA KULEVYA KABLA PABLO ESCOBAR HAJAFUFUKA TANZANIA.

"Kuna wakati najiona kama Mungu kwa sababu naweza kuagiza mtu afe na akafa siku hiyo hiyo". Ni maneno ya mtu muhalifu tajiri kuliko wahalifu wote waliowahi kuishi juu ya uso wa dunia, Pablo Emilio Escobar Gaviria.

Pablo alizaliwa desemba 1,1949 huko mjini Rionegro nchini Colombia. Baba yake alikuwa mkulima na Mama yake mwalimu wa chekechea. Akiwa kijana wa makamu, Pablo alihamia jijini Medelin na kujihusisha na shughuri za ulinzi kwenye majumba ya starehe, huku akitumiwa pia kusafirisha dawa za kulevya ndani ya jiji la Medelin. Shughuri hizi zilipelekea kuacha Masomo katika chuo kikuu cha LatinoAmericana na kijikita kabisa kwenye biashara ya dawa za kukevya.

Pablo alianza kujiinua taratibu na kujijengea mtandao hadi kumiliki biashara ilioanza kuvuka mipaka ya Colombia. Mwaka 1976 Pablo na wenzake walikamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa kosa la biashara haramu ya dawa za kulevya. Hata hivyo mamlaka za kidola na kisheria za Colombia zilishachelewa kupambana na Pablo. It was too late.

PLATA O PLOMO!
Moja kati ya mbinu za kuimarisha biashara ya 'unga' ni kuwapa hongo watu waliopewa dhamana ya kupambana na biashara hiyo, viongozi wa kisiasa, majaji, mahakimu na polisi. Jambo hili linapofanikiwa basi biashara ya unga 'hufana'. Lakini hutokea baadhi ya wazalendo wanaokataa hongo hizo na kusisitiza mapambano dhidi ya biashara hii haramu.

Pablo alikuwa na kanuni ingine ya ku'deal' na wazalendo hao, aliwaua.
Ndipo ikajengeka dhana hii ya Plata o Plomo, (kihispaniola) maana yake Fedha au Risasi. Viongozi wa kisiasa, Majaji, mahakimu na polisi waliokataa hongo za Pablo waliuawa. Mwaka huo wa 1976 ndio ulikuwa mwanzo wa Pablo kujiona Mungu kwa kuanza kuua majaji walikuwa wakihusika na kesi zake.
It was too late.

Medelin Cartel! Mtandao mapana wa dawa za kulevya ndani ya jiji la Medelin uliratibu karibu asilimia 80 ya biashara za 'cocaine' ulimwenguni kote. Nchi za Marekani, Spain, Mexico, Peru, Bolivia ziliathirika zaidi.

Miaka 1980s ndio hasa kilele cha ukuu wa Pablo ulipodhihirika alipoonekana kwenye orodha ya Forbes ya watu matajiri duniani kwa kumiliki dola bilion 23 (Tsh trilioni 46) Hata hivyo utajiri wake haikuwa rahisi kukisia kwa kuwa fedha zake hazikuwapo kwenye mfumo rasmi.

Kaka yake, Roberto Escobar anasema, Pablo alitumia dola 2500 (Tsh milion 5) kila mwezi kwa ajili ya kununua rubber band za kufungua fedha, anaongeza kuwa kila mwaka, fedha takribani dola bilion 2.1 (Tsh trilion 4) zilipotea kwa kuliwa na panya kwenye maghala ya kuhifadhia.

SIASA ZA PABLO
Sio tu kwamba aliwahifadhi wanasiasa mfukoni mwake, Don Pablo alikuwa na ndoto za kuwa Rais wa Colombia. Akiwa mtu mwenye aidiolojia za kikomunisti, alishinda kiti cha uwakilishi wa jiji la Medelin mnamo mwaka 1984. Lakini kusudio kubwa halikuwa kutumika Colombia bali kujilinda mwenyewe.

Wakati huo, serikali ya Marekani ilikubaliana na serikali ya Colombia kuhamisha watuhumiwa wa dawa za kulevya na kwenda kuhukumiwa nchini Marekani. Hii ilitokana na ukweli kwamba Marekani ndio nchi iliyoathirika zaidi na biashara ya cocaine kutoka Colombia. Karibu tani 15 za cocaine kila siku ziliingizwa Marekani kwa mgongo wa matandao wa Medelin Cartel chini ya Pablo Escobar, El Tsar De La Cocaine, (mfalme wa cocaine), El Padrino (Lord, Bwana), El Magico (Mtu wa maajabu), El Patron (Baba).

Katika kila wamarekani watano waliothiriwa kwa matumizi ya Cocaine, wanne walikuwa wateja wa Pablo. Kwa hivyo Marekani iliweka nguvu kubwa kupambana na dawa za kulevya nchini Colombia, lakini suala la watuhumiwa kuhamishiwa na kuhukumiwa nchini Marekani, lilijenga chuki kwa wafanyabiashara wa dawa za kulevya na hata wananchi dhidi ya serikali yao. Ilikuwa bora kaburi nchini Colombia kuliko gereza nchini Marekani.

Kupinga Marekani kujihusisha na 'Masuala' ya Colombia ilikuwa moja ya sababu za Pablo kujiingiza kwenye siasa, ili kujipa ulinzi. Hata hivyo historia yake ya kukamatwa na dawa za kulevya mwaka 1976 iliwekwa wazi na waziri wa haki Mr. Rodrigo Lara Bonilla akisaidiwa na majasusi wa Marekani wa kitengo cha DEA (Drug Enforcement Agent).

Historia hiyo haikumruhusu Pablo kuendelea kuwa mwakilishi katika 'Congress' ya Colombia, ikamlazimu kujiuzulu. Siku chache baadae, waziri wa haki, Rodrigo Lara Bonilla aliuawa kwa risasi.

Huo ndio ulikuwa mwanzo wa ugaidi wa Pablo. Jamii ya Colombia na ya kimataifa ikamtambua kuwa utajiri wote wa Pablo umetokana na biashara haramu za cocaine.

Ndege 16, mahoteli, helicopter 6, nyambizi za kuendeshwa kwa rimoti, mashamba makubwa, vyote vilitokana na biashara ya cocaine. Ufadhili wake kwa vilabu vya soka, kudhamini michuano ya soka ya klabu bingwa za America '(copa libertardos'), nyumba alizowajengea wananchi Masikini na misaada mingine aliyotoa na kumfanya kupendwa na wananchi wa Medelin, vilitokana na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Siri za Pablo zikafichuka na kumfanya mtu asiye na furaha, bali chuki na visasi na zaidi ugaidi dhidi ya serikali.

UGAIDI
Pablo aliendesha shughuri zake za uhalifu kwa kuua mamia ya askari walitotumika kumdhibiti. Yeye alitumia waasi wa kikomunist wa M19, LPA na PLA waliokuwa wakipambana na serikali. Aliwadhamini kwa fedha nyingi na kuwatuma kuvamia ofisi mbalimbali za serikali, kuiba nyaraka na kuchoma moto ili kupoteza nyaraka muhimu. Waasi wa M19 walihusika pia kuvamia mahakama ya Medelin na kuua majaji na kuchoma moto nyaraka zilizohusu kesi za wafanyabiashara wa dawa za kulevya.

Watu karibu 50,000 waliuawa kwa mabomu na risasi, akiwamo mgombea Urais, Bw. Luis Galan aliyepigwa risasi baada ta kuonesha kwenye kampeni zake fikra za kuunga mkono jujudi za Marekani za kuwahamisha watuhumiwa wa kesi za 'unga'.

Ilikuwa bora kaburi Colombia kuliko Gereza Marekani.

THE CASTLE
Mwishoni mwa miaka ya 1980 na mwanzoni mwa miaka ya 1990, Jiji la Medelin halikuwa salama kwa maisha wa binadamu.

Ndipo Pablo akaitaka serikali kuacha kumfuatilia na ili watu wasindelee kuumia. Serikali ulionekana kama imeshindwa kumkamata mtu mmoja, tena asiyetaka kuhama nchini humo, adui mkubwa wa serikali asiyekimbia nchi, na asiyekamatika.

Baada ya mazungumzo na serikali na Pablo, wakafikia muafaka kwamba Pablo ajenge gereza lake, ajifungie huko nje ya jiji la Medelin na kisha machafuko yatulie. Pablo akajenga gereza lake, akafunga huko, akipata kila aina ya starehe ya dunia aliyoitaka. Halikuwa gereza, lilikuwa ni kasri, au kama alivyoita mwenyewe; El Castillo (The Castle).

Ujanja huo wa Pablo wa kutoroka mkono wa sheria, kwa kujifanya mfungwa huku alifaidi kila mema ya dunia na biashara zake haramu zikiendelea kiliwakera baadhi ya maofisa wa serikali na washirika wao wa marekani. Vita ikaibuka upya. Kitengo maalum cha kijeshi kilichotumwa na Rais Dr. Cesar Gaviria, kikiongozwa na Colonel Martinez kilivamia 'gereza' la pablo, wakisaidiwa na maadui wa kibiashara wa Pablo. Hata hivyo Pablo alikwisha jiandaa na kila kitu, tayari kulikuwa na handaki alilotumia kutoroka, na kutokomea zake.

Miaka miwili baadae, December 2, 1993, Pablo alizidiwa nguvu kwenye mashambulizi dhidi ya kikosi cha Search Bloc na kufariki dunia. Haijukikani ama alijiua au akikufa kwa risasi iliyorushwa na mmoja wa askari. Lakini binamu yake, Gustavo Gaviria aliwahi kusema, Pablo aliahidi kujipiga risasi ya sikio endapo akizidiwa na kushindwa kukimbia.

TANZANIA.
Kuna mengi ya kuandika kuhusu Tanzania. Labda tusubiri 'ombi' la Mh. Waziri wa afya, Ummy Mwaimu kutaka ofisi ya mkemia mkuu wa serikali kuanza utaratibu wa kuwapima vijanaqa vyuo na shule ili kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya, wakati huo huo tumeambiwa kuwa ofisi ya mkemi mkuu iliruhusu kemikali zinazotumiwa kuandaa dawa za kulevya kuingia nchini.

Vita hii ni ngumu, mtandao ni mkubwa. Sisi tusio na silaha tunawajibika kuelimisha jamii! Wenye silaha na sare wataamua kuungana nao au kupambana. lakini hadi leo jambo rahisi la kuchoma moto dawa 'zinazokamatwa' halijafanyika.

Hofu yangu ni endapo ile falsafa ya 'Plata O Plomo' imeanza kunoga Tanzania?

#Gracias
 
Back
Top Bottom