Tumeambiwa mapato ya TRA tozo zingine vipi?

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
16,054
11,567
Tumeambiwa TRA mwezi uliopita kuwa wamekusanya 1.31trl hongereni sana. Lakini kuna mapato mengine ya serikali amabayo hayapiti TRA mfano ada ya leseni za biashara hivi zinalipwa moja kwa moja halmashauri. Zipo ada za taasisi za serikali kama TCRA TFDA EWURA etc zote hizi zinatoza fedha na hizi fedha haziingii kwenye account ya TRA.

Zipo ada za wizara kama ada za kuuza vitu nje ambazo hulipwa wizarani moja kwa moja. Kuna ushuru wa mkaa na mbao ambao hulipwa moja kwa moja kwa wizara husika. Ipo mirabaha ya Madini ambayo hulipwa moja kwa moja wizarani, hizi fedha ni ngapi na zinatumikaje? Nasikia TCRA walikusanya 79b lakini wakatumia 76b zikiwemo 18b kwa ajili ya makongamano, mungu wangu haya makongamano tunalipia "participation fee".
 
mkuu umenikumbusha mfano PHARMAY COUNCIL zinaingiza karibia bilion 5 kwa mwaka sio hela ndogo hiyo
 
Back
Top Bottom