Tume ya Utumishi wa Mahakama

Tume ya Utumishi wa Mahakama

Ghost Worker

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2016
Posts
1,412
Reaction score
1,869
Tume ilitangaza ajira 195 mwezi wa Aprili na miongoni mwa nafasi zingine ikasema kuna nafasi wazi 114 za Hakimu Mkazi II, wenye sifa waombe. Watu wameomba na Tume ikaitikia kwa kuita waombaji 300+ mwezi Oktoba (kwa nafasi ya uhakimu). Wengi tukavutwa na uwiano huo wa ushindani (nafasi 1 watu 3) pamoja na hadhi na heshima ya chombo hiki kinachoundwa na Katiba (Tume ya Utumishi wa Mahakama), tukamiminika toka kila kona ya nchi kwenda Karimjee kusailiwa licha ya hali zetu ngumu Kiuchumi, tukiamini ni mchakato wa kweli na wa haki.

La kushangaza jana 9/11/2020, Tume imeita wasailiwa 20 pekee kazini licha ya awali kutangaza nafasi 114 kwa nafasi hiyo na kusaili 300+. Huenda waliobaki out of 300+ walikosa sifa (Lakini Tume ingeujuza umma kuhusu hilo na kutoa Utaratibu wa kuwapata 94 waliosalia). Lakini pia huenda ni ukata hakuna pesa ya kuajiri wote 114 kama ilivyotangazwa.

Sasa kama hali ni hii palikuwa na haja gani kwa Chombo hiki nyeti kutangaza nafasi za ajira zinazokinzana na hali halisi ya uwezo wa idara ya Mahakama na kusumbua bure waombaji? Hatusemi kwamba ilikuwa lazima wote 300 tuajiriwe la, lakini ubabaishaji na mizengwe kwenye masuala nyeti kama haya unatia sana mashaka juu ya credibility ya mamlaka hizi za uajiri.
 
Tume ilitangaza ajira 195 mwezi wa Aprili na miongoni mwa nafasi zingine ikasema kuna nafasi wazi 114 za Hakimu Mkazi II, wenye sifa waombe. Watu wameomba na Tume ikaitikia kwa kuita waombaji 300+ mwezi Oktoba (kwa nafasi ya uhakimu). Wengi tukavutwa na uwiano huo wa ushindani (nafasi 1 watu 3) pamoja na hadhi na heshima ya chombo hiki kinachoundwa na Katiba (Tume ya Utumishi wa Mahakama), tukamiminika toka kila kona ya nchi kwenda Karimjee kusailiwa licha ya hali zetu ngumu Kiuchumi...

 
Back
Top Bottom