Tume ya Usuluhisi na Uamuzi (CMA) - Ushauri

Tume ya Usuluhisi na Uamuzi (CMA) - Ushauri

ThnkingAloud

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2017
Posts
594
Reaction score
607
Serikali ilipoanzisha Tume ya Usuluhishi na Uamuzi kusimamia mashauri yanayohusiana na ajira iliunda sheria ya ajira na mahusiano kazini pamoja na kanuni na miongozo yake kwa lengo la kuhakikisha mashauri hayachukui muda mrefu kushughulikiwa na Tume kwa sababu yanauhusiano wa karibu na ajira na maisha ya wafanyakazi pamoja na familia zao.

Cha ajabu ni kuwa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi imekuwa ikitumika kama kichaka cha kuchelewesha mashauri ya ajira kwa makusudi kwa Tume kushindwa kufuatilia kwa karibu kila shauri na sababu za ucheleweshwaji wake ili kuondoa changamoto zilizopo kuhakikisha lengo la serikali linafikiwa.. Yapo mashauri ndani ya Tume ya Usuluhishi na Uamuzi yamekaa zaidi ya miaka miwili mpaka mitatu bila kusikilizwa kwa sababu zisizokuwa na msingi.

Jambo hili linapunguza imani ya waathirika kwa Tume na serikali kwa ujumla wake.

Ninauomba uongozi wa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ufuatile kwa karibu mwenendo wa mashauri yote ili kuondoa chamngamoto zinazosababisha ucheleweshwaji wa kusikilizwa mashauri na kutoa maamuzi kwa wakati.

Hii itasaidia kuongeza kuaminika kwa Tume na serikali kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom