Tume ya Uchaguzi tunaomba ufafanuzi kwenye hili

Mtoa post umetoa hii bandiko kimhemio unahitaji darasa hasa,

Pili kupitia bandiko lako hili unamponza kijana wawatu kwa kosa la kujiandikisha mara mbili, na hapo ni lazima alidanganya kimepotea (kumbe anacho ili tu arekebishe Taarifa zake hicho kituo cha kupigia kura au hiyo picha yake ya mwanzo)

SangaweJr
Amezaliwa mwaka 1999, mwaka 2015 angepataje kitambulisho? Kabla hujacomment jitahid kusoma kitu kwa umakin

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una maana kama nikibadili makazi mara nane nitakuwa na vitambulisho nane? Provided tu nikisema vya awali vimepotea
Tumia ubongo Mzee sio kamasi uta print vipi kingine wakati amebadili makazi kutoka 2015 now 2020 na kumbuka hili zoezi lilikuwa kuboresha taarifa za wapiga kura na kuandikisha wapya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo kijana huenda kajiandiksha mara mbili katika vituo tofauti kitu ambacho ni kinyuny cha sheria hata hivyo atafutwa kituo cha awali na kubaki kituo kimoja tu baada ya data kuchakatwa na mfumo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ngojeni niwaambie kitu

Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ni pamoja na kubadirisha kitambulisho Chako endapo utahama Makazi sababu hayo Makazi utakayo hamia Hautaweza kupiga Kura na kitambulisho cha mahali ulikotoka

Mimi jamaa yangu alikua anakaa Tabata
Amehamia Gongo la mboto
Alikua na kadi ya kupiga Kura (Nzima kabisa) inaonesha Tabata Alienda kuboresha amerudi inaonesha Gongo la Mboto

Hiyo Scenarios ya Yusuph inaweza kuta ina Ingia hapo ni maswala ya picha tuu
Ok, je unalizungumziaje swala la huyo kijana kuwa na namba mbili tofauti za hivyo vitambulisho? Kuboresha siyo ishu hata uboresheje namba yako ni ile ile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vp namba yako ilibadilika?
Hapo suala ni dogo kutokusalimisha kitambulisho chake alipoenda kubadili kituo cha kupigia kura!

Mm nimebadili kituo nikapewa kadi mpya na ile ya zamani wamebaki nao wao; Pia kujiandikisha kwangu sikuweka alama za vidole tofauti na wale wasionacho kbsa au waliopoteza Ila kama ulipoteza ya zamani na bado ukabadilisha kituo bado bado watakupa kingine tu maana ww zitakazoenda ni taarifa mpya!

Labda tuilaumu tume kwa kutokutoa somo, Kwa hapa ni jambo ambalo halizuiliki kama hatujapewa elimu ya uandikishaji

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vp kuhusu serial number?
Sioni tatizo kabisa hapo kwa hoja zifuatazo
Moja akina yusuph ni wengi sana,mfano nikikutajia Nina language na ubini wangu harafu uingie facebook usechi hili jina utapata almost watu 100 ambao tuna jina moja na ubini wa kufanana,


Mbili huenda muhusika alijiandikisha kwa mara ya kwanza kituo A lakini wakati wa maboresho amejikuta yuko kituo hivo akapewa kitambulisho kingine na hivyo kumfanya kuwa na vitambulisho viwili,chadema akili zenu ziko wapi?

Mfano nzuri ni Mimi ,uchaguzi wa 2015 nilijiandikisha nikiwa mkoani Moro,wakati wa maboresho mwaka huu nimejiandikishia shinyanga hivyo kunifanya niwe na vitambulisho viwili

Hizi hili nalo linahitaji tochi wenzangu chadema

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
UZI HAUJAELEWEKA KWA WALIO WENGI.

HOJA, KWA UMRI WA HUYO DOGO ANATAKIWA AWE NA KITAMBULISHA KIMOJA TUU CHA MWAKA HUU.

HICHO CHA MWANZO ALIKIPATA KWA SHERIA IPI YA TUME ILHALI ALIKUA NA MIAKA 16 Tuu?

Goli La Mkono Moja Wapo Ndio Hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu samahani sana ila leo nimekudharau sanaa kama ni kweli na ww ni msomi basi bora mimi niliyeishia la saba B
Hili nalo linahitaji tume ya uchaguzi kusema kweli wewe soma vizuri hapo chini utagundua hapo kuna cha zamani na cha sasa! Hapo ni wazi hapo kimoja kimebadilishwa kinarudishwa na amepewa kipya ambacho amehamia kituo kipya cha kupigia kura!

Mwanzo alikuwa kituo kingine na sasa amebadilisha makazi hivyo amejiandikishia kwenye kituo kipya na automatically kituo cha mwanzo jina lake halitokuwepo bali litatokea kituo cha sasa alicho jiandikisha upya!

Hapo mbona hakuna kipya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilichokiona hapo kwa dogo, kafanya uhamisho kutoka kata ya Kwembe kwenda kata ya Mbezi. Kadi ya zamani automatically ilitakiwa kubaki Kwa BVR OPERATOR ili irudishwe tume ya Taifa ya uchaguzi.

Je! Hiyo kadi ya zamani inarejeshwa tume kwa nia njema au haramu. Hapo ndipo tuhoji. Pili umri wa dogo wakati anajiandikisha 2015 umri wake ulikuwa ni miaka 16 pungufu ya miaka 2 ya miaka 18 ya umri wa kisheria kuweza kupiga kura. Sasa ni vyema ufafanuzi ukatolewa kuondoa mkanganyiko wa umri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa kwanini cha zamani amebaki nacho?

Sent using Jamii Forums mobile app

Amebaki nacho kimakosa!maana mwingine anaweza sema amepoteza kumbe anacho nyumbani lakini ukweli ni kwamba jina lake litaonekana kituo kimoja tuu alicho jiandikisha mwisho!

Awezi piga kura mara mbili maana jina lake halitatokea mara mbili....

Hicho kingine hakitumiki kabisa
 
Mtoa post umetoa hii bandiko kimhemio unahitaji darasa hasa,

Pili kupitia bandiko lako hili unamponza kijana wawatu kwa kosa la kujiandikisha mara mbili, na hapo ni lazima alidanganya kimepotea (kumbe anacho ili tu arekebishe Taarifa zake hicho kituo cha kupigia kura au hiyo picha yake ya mwanzo)

SangaweJr

Kimsingi awezi kupiga kura mara mbili maana jina lake kule litafutwa litatokea kituo kipya!
 
Wacha uongo wewe!
Hivi unafkiri watu wote ni wajinga kama unavyodhani wewe? Kama huo upuuzi unaouzungumzia wewe kada wa lumumba ni kweli, kwa nini alibadilisha kituo wakati wa kujiandikisha kwa mara ya pili?

Ukibadilisha kituo na jina lako linahamia kwenye kituo kipya alicho jiandikisha upya! Kamwe uwezi poga kura mara mbili!

Halafu punguza jaziba hapa tunafanya mjadala huru
 
Kimsingi awezi kupiga kura mara mbili maana jina lake kule litafutwa litatokea kituo kipya!
Huyo dogo ana kadi mbili za mpiga kura zenye number tofauti, ina maana kama amehama makazi alienda kijiandikisha kama mpiga kura mpya. Badala ya kurekebisha taarifa.

Au amefanya kwa makusudi ili kujaribu aone kama inawezekana.( amefanikiwa sababu zoezi linafanyika offline) data zikiingizwa kwenye system ya NEC atajulikana dogo asijione mjanja.

Ninapo sema offline namaanisha ukienda kujiandikisha kituo A. Ukaondoka kwenda kituo B kuhakiki taarifa zako huwezi zipata ndani ya huo muda wa uandikishaji hadi urudi kituo A ndio utakuta taarifa zako. Ndio maana kunauwezekano mkubwa kaweza kujiandikisha mara mbili.
 
View attachment 1368813

Huyu mtu mmoja kwanini ana vitambulisho viwili ?
Mimi nilipigwa Picha na baada muda mpigapicha ananiambia kitambulisho changu kimetoka vibaya mara akatoa kingine nikamuuliza mbona vyote vinafanana hakuwa na majibu ya kunitosheleza.
Nikamuuliza hiki kingine unapeleka wapi akanijibu hivi vyote vilivyoharibika tunavipeleka tume nikamwomba register aiandeke akaniambia hawana register.Vitambulisho nilivyoviona pale ni vingi sana.
Kuna Uzi niliandika Jumamosi ktk hoja mchanganyiko kuhusu hili tukio nililokutana nalo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom