Tume ya uchaguzi NEC imeuza taarifa za wapiga kura kwa mgombea wa CCM!

Hiyo ni kampeni ya man to man, kitanda kwa kitanda na shuka kwa shuka.

CCM imejipanga vizuri kupitia kwa wajumbe wa nyumba kumi kumi. Hapo mtaani kwenu wote wana simu zenu.

Tafadhali usiichafue tume.

Hiyo ndiyo man to man.

Queen Esther

Salaam ndugu wana JF,

Leo nimeghafirika sana baada ya kupokea ujumbe wa maneno (SMS) kwenye namba yangu ya simu ambayo niliiandika siku najisajiri kwenye moja ya kituo cha kupigia kura kilichopo katika kata ya Makongo.

Kwa kifupi mimi pamoja na mke wangu tumejiandikisha kwenye kituo flani kilichopo kata ya Makongo ingawa si wakazi wa Makongo hivyo hakuna mahali pengine popote ambapo kuna taarifa kwamba tunaishi Makongo zaidi ya NEC.

Kama tujuavyo kwenye kujiandikisha kule tunaweka maelezo yetu binafsi ambayo huwezi ukashare na mtu mwingine katika hali ya kawaida, kama tujuavyo suala la PRIVACY ni suala nyeti sana na baadhi yetu tunalichukulia kwa uzito wa hali ya juu sana, lakini kilichotokea ni kwamba inaonekana Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wamegawa namba zetu kwa mgombea/wagombea wa CCM bila ridhaa yetu (Ushahidi ni message iliyoingia kwangu na kwa mke wangu).

Mimi na mke wangu (natumaini na wengine waliojiandikisha jimbo la KAWE) tumetumiwa ujumbe wa maneno ukiwa unatuomba tuhudhurie mkutano wa huyo mtumaji, na sms inaonekana imetumwa na KIPPI, baada ya kusearch nimeona jina la mtu anaitwa KIPPI WARIOBA ambaye ni mgombea ubunge jimbo la KAWE (CCM), kwa kweli nimeghafirika sana kwa sababu tume ya Taifa ya Uchaguzi ni chombo ambacho nimekiamini sana kwamba taarifa zangu zipo mahali salama lakini leo hii mgombea ubunge amepatiwa namba yangu bila ridhaa yangu.

Ninaomba wadau waliopo humu ndani walipigie kelele suala hili, pia kama kuna uwezekano wa kuishtaki tume, na pia Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Judge Lubuva alitolee maelezo imekuwaje mgombea huyu wa CCM akapata access ya namba za simu za watu waliopo katika jimbo lake bila ridhaa ya wahusika wenyewe?

Nimeambatanisha screenshot ya ujumbe huo kwa ushahidi zaidi, nimekasirika sana kwa kweli, huwezi amini maana nimeona kama mgombea ameweza kupewa namba yangu ya simu ambayo ipo kwenye database ya wapigakura wa NEC, je anashindwaje kupewa kura yangu bure hata kama sijampigia?

View attachment 291867

NB: "MODS NAOMBA HUU UZI MUUACHE ILI WATU WAJUE KINACHOENDELEA"

Cc: TCRA
 
nafikiri hili suala lisiishie hapa,hatua zaidi zichukuliwe hata idhihirike michezo inayofanywa na CCM & NEC
 
Wanawatumia Push mobile, wao push wanachukua data toka makampuni ya simu

Inamaana hao Push Mobile ndiyo wana utaalamu wa kujua huyu jamaa amejiandikishia Makongo ili Kipi Warioba amualike kwenye mkutano wake? Usirahisishe mambo kiasi hicho mkuu.
 
Nami ni mkazi wa Kawe, nimepokea sms hiyo kutoka kwa huyo ndugu. Niliipuuza japo sikufikiria mbali kama ulivoandika, kutolewa taarifa zetu.
 
Tumaini Makene please pitia huu uzi hizi taarifa msizipuuzie kabisa...mjulishe Mdee (coz ni jimboni kwake) na viongozi wa IT wa UKAWA. You never know it might be ndiyo maandalizi ya goli la mkono.
 
Last edited by a moderator:
Salaam ndugu wana JF,

Leo nimeghafirika sana baada ya kupokea ujumbe wa maneno (SMS) kwenye namba yangu ya simu ambayo niliiandika siku najisajiri kwenye moja ya kituo cha kupigia kura kilichopo katika kata ya Makongo.

Kwa kifupi mimi pamoja na mke wangu tumejiandikisha kwenye kituo flani kilichopo kata ya Makongo ingawa si wakazi wa Makongo hivyo hakuna mahali pengine popote ambapo kuna taarifa kwamba tunaishi Makongo zaidi ya NEC.

Kama tujuavyo kwenye kujiandikisha kule tunaweka maelezo yetu binafsi ambayo huwezi ukashare na mtu mwingine katika hali ya kawaida, kama tujuavyo suala la PRIVACY ni suala nyeti sana na baadhi yetu tunalichukulia kwa uzito wa hali ya juu sana, lakini kilichotokea ni kwamba inaonekana Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wamegawa namba zetu kwa mgombea/wagombea wa CCM bila ridhaa yetu (Ushahidi ni message iliyoingia kwangu na kwa mke wangu).

Mimi na mke wangu (natumaini na wengine waliojiandikisha jimbo la KAWE) tumetumiwa ujumbe wa maneno ukiwa unatuomba tuhudhurie mkutano wa huyo mtumaji, na sms inaonekana imetumwa na KIPPI, baada ya kusearch nimeona jina la mtu anaitwa KIPPI WARIOBA ambaye ni mgombea ubunge jimbo la KAWE (CCM), kwa kweli nimeghafirika sana kwa sababu tume ya Taifa ya Uchaguzi ni chombo ambacho nimekiamini sana kwamba taarifa zangu zipo mahali salama lakini leo hii mgombea ubunge amepatiwa namba yangu bila ridhaa yangu.

Ninaomba wadau waliopo humu ndani walipigie kelele suala hili, pia kama kuna uwezekano wa kuishtaki tume, na pia Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Judge Lubuva alitolee maelezo imekuwaje mgombea huyu wa CCM akapata access ya namba za simu za watu waliopo katika jimbo lake bila ridhaa ya wahusika wenyewe?

Nimeambatanisha screenshot ya ujumbe huo kwa ushahidi zaidi, nimekasirika sana kwa kweli, huwezi amini maana nimeona kama mgombea ameweza kupewa namba yangu ya simu ambayo ipo kwenye database ya wapigakura wa NEC, je anashindwaje kupewa kura yangu bure hata kama sijampigia?

View attachment 291867

NB: "MODS NAOMBA HUU UZI MUUACHE ILI WATU WAJUE KINACHOENDELEA"

Cc: TCRA
Usighazabike Bure na usiwe mwepesi kuhukumu na haswa inapojitokeza matukio kama haya kwani kwa ukuaji wa technolojia na haswa kwa kasi tunayokwenda nayo yenye mwelekeo wa uwazi yote yanawezekana hata bila ya tume kuhusika na kwa ushuhuda tu ni kwamba leo familia nyingi zimeingia matatizoni na haswa zile ambazo ni BBC. yawezekana kabisa ww umekuwa na mtazamo hasi au aleji na ccm
 
Mkuuu kwani mitandao ya simu haibaki na record kuwa mamba yako inaexist?
Hapa NEC hawahusiki.. kama ulikuwa hujui ndio ujue kuwa Push Mobile wanafanya advertisement kupitia sms
Mkuu nadhani hujamuelewa mleta maada. Yeye alijiandikisha katika moja ya vituo vya huko Makongo, ingawa haishi Makongo. Kama ingekuwa ni Push Mobile, bila shaka wange target watu waishio Makongo kwa kuangalia taarifa za matumizi ya simu kupitia minara ya Karibu (kwa uelewa wangu mdogo). Kutokuwapo kwake Makongo na akatumiwa sms kuhusu mkutano wa mgombea wa CCM wa eneo alilojiandikisha, amehusisha na wale waliobeba taarifa zake za kituo cha kujiandikisha.
 
Hata mimi nimepata sms hiyo leo hii...Sasa ina maana gani???au ni kwamba kurA zetu zote zitaenda...CCM tutake tusitake kutokana na hizo information ambazo wanazo????
 
Hiyo ni kampeni ya man to man, kitanda kwa kitanda na shuka kwa shuka.

CCM imejipanga vizuri kupitia kwa wajumbe wa nyumba kumi kumi. Hapo mtaani kwenu wote wana simu zenu.

Tafadhali usiichafue tume.

Hiyo ndiyo man to man.

Queen Esther

Elewa we kiumbe, huyu jamaa haishi Makongo.kwa hiyo hakuna habari ya mjumbe hapo.
 
nimesoma maelekezo yako vyema,ila ukija kwenye ujumbe unakuta jina limeseviwa kippi. Katika hali ya kawaida ukituma push sms haijisave jina ila inaonyesha majina kamili ya yule aliye kutumia ila kwako ww hapo inaonyesha umesave hiyo number,huo ni uongo wa kutaka kutuaminisha kwa sababu sote tunajua push sms zinakuwa vipi,
pili hata kama ungekuwa hujasevu hiyo number tulitegemea tuone number ya simu yamtumaji ila haijatokea hivyo

ombi langu naomba tcra kutumia vyema sheria ya mtandao kuwakamata watu kama hawa wanaopotosha na kudanganya umma

---->>yaelekea alipopa SMS ikabidi atafute Namba ya mtuma SMS kwamba ni Nani?,alipokosea ni aliiserve Namba kwa hill jina!,then wakati sasa anatafuta jinsi ya kutoa habari,katika maelezo aka screenshot -->>hivyo jina tayari lilikuwa tayari limesha ji-syncronize!
Nadhani ndilo lililotokea!
 
Nimesearch hilo jina mkuu, anaitwa KIPPI WARIOBA, ni Mgombea Ubunge wa CCM Kawe! Jiulize amepata wapi namba yako ya simu, na taarifa kwamba unaishi jimbo la KAWE.

Kiongozi mimi nadhani hizo taarifa hawazitoi NEC.

Wakati wa kujiandikisha kulikuwa na wajumbe wenye kuwakilisha vyama vyao. Kituo nilipojiandikisha mimi nilimwona mjumbe akinakili kwa ki-wiziwizi majina na namba ya simu hasa wakati yule kalani anakuhoji.

Mie nimejiandikishia kituo eneo bunge la Kibamba na niliona hilo
 
Kama ni hivyo basi...CCM wanafanya jambo baya sana?..Dhuluma kubwa sana juu yetu sisi WATANZANIA????????
 
Nilicho kifanya nimecopy huu ujumbe nimemtumia Halima Mdee kama ilivyo atusaidie kwenda tume kupata majibu Juu ya haya mambo number zetu wamezipataje?
 
Back
Top Bottom