Tume ya uchaguzi NEC imeuza taarifa za wapiga kura kwa mgombea wa CCM!

WE ARE ANONYMOUS

JF-Expert Member
Mar 23, 2015
217
282
Salaam ndugu wana JF,

Leo nimeghafirika sana baada ya kupokea ujumbe wa maneno (SMS) kwenye namba yangu ya simu ambayo niliiandika siku najisajiri kwenye moja ya kituo cha kupigia kura kilichopo katika kata ya Makongo.

Kwa kifupi mimi pamoja na mke wangu tumejiandikisha kwenye kituo flani kilichopo kata ya Makongo ingawa si wakazi wa Makongo hivyo hakuna mahali pengine popote ambapo kuna taarifa kwamba tunaishi Makongo zaidi ya NEC.

Kama tujuavyo kwenye kujiandikisha kule tunaweka maelezo yetu binafsi ambayo huwezi ukashare na mtu mwingine katika hali ya kawaida, kama tujuavyo suala la PRIVACY ni suala nyeti sana na baadhi yetu tunalichukulia kwa uzito wa hali ya juu sana, lakini kilichotokea ni kwamba inaonekana Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wamegawa namba zetu kwa mgombea/wagombea wa CCM bila ridhaa yetu (Ushahidi ni message iliyoingia kwangu na kwa mke wangu).

Mimi na mke wangu (natumaini na wengine waliojiandikisha jimbo la KAWE) tumetumiwa ujumbe wa maneno ukiwa unatuomba tuhudhurie mkutano wa huyo mtumaji, na sms inaonekana imetumwa na KIPPI, baada ya kusearch nimeona jina la mtu anaitwa KIPPI WARIOBA ambaye ni mgombea ubunge jimbo la KAWE (CCM), kwa kweli nimeghafirika sana kwa sababu tume ya Taifa ya Uchaguzi ni chombo ambacho nimekiamini sana kwamba taarifa zangu zipo mahali salama lakini leo hii mgombea ubunge amepatiwa namba yangu bila ridhaa yangu.

Ninaomba wadau waliopo humu ndani walipigie kelele suala hili, pia kama kuna uwezekano wa kuishtaki tume, na pia Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Judge Lubuva alitolee maelezo imekuwaje mgombea huyu wa CCM akapata access ya namba za simu za watu waliopo katika jimbo lake bila ridhaa ya wahusika wenyewe?

Nimeambatanisha screenshot ya ujumbe huo kwa ushahidi zaidi, nimekasirika sana kwa kweli, huwezi amini maana nimeona kama mgombea ameweza kupewa namba yangu ya simu ambayo ipo kwenye database ya wapigakura wa NEC, je anashindwaje kupewa kura yangu bure hata kama sijampigia?

KIPPI.jpg


NB: "MODS NAOMBA HUU UZI MUUACHE ILI WATU WAJUE KINACHOENDELEA"

Cc: TCRA

Wengineo:

Aisee kweli NEC mnauza taarifa mimi Mke wangu kajiandikisha Makongo Secondary lakini tunaishi Ubungo. Ajabu nae katumiwa sms na huyo Kipi. Hafanyi kazi huko alijiandikisha ili apate kitambulisho inakuwaje apate namba ya Mke wangu??? NEC mnauza information zetu.


Nami ni mkazi wa Kawe, nimepokea sms hiyo kutoka kwa huyo ndugu. Niliipuuza japo sikufikiria mbali kama ulivoandika, kutolewa taarifa zetu.

Hata mimi nimepata sms hiyo leo hii...Sasa ina maana gani???au ni kwamba kurA zetu zote zitaenda...CCM tutake tusitake kutokana na hizo information ambazo wanazo????


Na mimi nimepata hiyo message inatoka kwa KIPPI, ni kama ameniongezea hasira hasa nikikumbuka baba yake alivyotugeuka kwenye suala la Katiba.

Hata mimi nimetumiwa hiyo taarifa
 
nimeshangaa uyu kipi kajuaje namba yangu baada ya kipokea ujumbe huu kumbe ...
 
Kile walichokuwa wanatafuta CCM sasa wamekipata kama mkuu wa IT aliondoshwa pengine huyu aligoma kutoa taarifa za wapiga kura sasa aliyeingia yuko kwa kazi maalumu na kama yule aliyetolewa alikuwa kusikojulikana kwa mda halafu akarudishwa kukabidhi ofisi. Hii inamanisha kuwa taarifa zetu wapiga kura ziko CCM ndio maana wanajidai watashinda kwa kishindo fuatilia kauli ya Magufuli 95% msikie nape hapo unapata jibu something Fish is going ON hii haikubaliki
 
Wanawatumia Push mobile, wao push wanachukua data toka makampuni ya simu
 
Just imagine walikuwa kimya siku zote lakini baada ya jamaa wa IT kuondolewa mpaka Nape katoka alikojificha kuna kitu si cha kawaida pengine kila kituo kura zishapigw utokana na namba zetu za kadi then tutaambiwa kwamba. MAGUFULI kashinda kwa kishindo this matter should be taken seriously by opposition vinginevyo. UKAWA chali hata mkipiga kura vp.
 
Usiongee usichokijua, namba yangu ya simu sikuisajiri nikiwa MAKONGO, sehemu pekee ambayo nimeinclude namba ya simu inayoonesha nipo MAKONGO ni TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI.

Mkuuu kwani mitandao ya simu haibaki na record kuwa mamba yako inaexist?
Hapa NEC hawahusiki.. kama ulikuwa hujui ndio ujue kuwa Push Mobile wanafanya advertisement kupitia sms
 
nimeshangaa uyu kipi kajuaje namba yangu baada ya kipokea ujumbe huu kumbe ...

Jimbo langu ni kawe, Mkuu jana nimepata habar kwa jamaa angu wa kibamba kwamba ccm siku iz wanapita wananunua namba cm na majina
 
Mkuuu kwani mitandao ya simu haibaki na record kuwa mamba yako inaexist?
Hapa NEC hawahusiki.. kama ulikuwa hujui ndio ujue kuwa Push Mobile wanafanya advertisement kupitia sms

Hivi unaelewa hata unachokiandika?? Then hiyo mitandao ya simu imejuaje kwamba mimi ni mkazi wa MAKONGO? Nimekuambia sikuisajiri namba nikiwa MAKONGO, wala hakuna fomu yoyote niliyojaza nikaandika kwamba naishi Makongo au Kawe zaidi ya NEC. Miaka ya nyuma kote nilikuwa mkoani, sehemu pekee ambayo nili include namba ya simu ni wakati wa kujiandikisha wakati nipo Makongo, na ujumbe umetoka kwa mgombea Ubunge wa jimbo la pale nilipojiandikisha, upo hapo?
 
Hii nchi hii inakila kiashiria kwamba inakwenda kupasuka. Nisuala la muda tu. Nchi zote zilizopasuka zilisababishwa na watawala wao kung'ang'ania madarka wakati wananchi wamewachoka.
 
Back
Top Bottom